Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-05-10 17:04:15    
Mwana-kiwanda aliyefanikiwa kusafirisha magari yenye hataza ya China katika soko la kimataifa

cri
Soko la magari nchini China limekuwa na maendeleo ya kasi katika miaka ya karibuni, magari ya makampuni maarufu ya kimataifa yakiwemo Volkswagen na Ford yameshaingia kwenye soko la magari la China. Katika wakati ambao makampuni mengi ya kimataifa yananuia kukuza soko la magari la China, mwanakiwanda mmoja kijana anasafirisha magari yenye hataza ya China yanayozalishwa katika kiwanda alichokiongoza katika nchi zaidi ya 30 kwa kutumia muda wa miaka minane tu. Mwanakiwanda huyu ndiyo mkurugenzi mkuu wa kampuni ya magari ya Chery Bw. Yin Tongyao.

Mwaka 1984 Bw. Yin Tongyao alihitimu masomo yake katika chuo kikuu na kufanya kazi katika kampuni ya kwanza ya magari ya China. Mwaka 1995, muda si mrefu baada ya kampuni hiyo kuingia ubia na kampuni ya Volkswagen, Bw. Yin Tongyao aliamua kuondoka katika kampuni hiyo ya magari, alirejea kwao mkoa wa Anhui na kuanzisha kampuni inayozalisha magari yenye hataza ya China yenyewe akishirikiana na wenzake 7. alipozungumzia kuhusu kufikia uamuzi huo, Bw. Yin Tongyao alisema kuwa kampuni nyingi za China zinapokuwa na nguvu kidogo huwa zinafuata njia ya ubia na makampuni makubwa ya nchi za nje ili kupata uungaji mkono wa mitaji na teknolojia. Lakini sekta ya magari ya China ikitaka kuwa na maendeleo ya miaka mingi hazina budi kuvunjilia mbali ukiritimba wa teknolojia ya makampuni ya kimataifa, iwe na magari yenye hataza ya China yenyewe. Anafananisha kuanzisha kampuni ya magari ya China kama kupanda kilele cha mlima wa Zhumulangma, kufanya ubia na makampuni makubwa ya kimataifa ni kama kupanda mlima kwa kupitia mtelemko wa upande wa kusini, ambao hauna mwinuko mkali lakini kuzalisha magari yenye hataza ya China ni kama kupanda mlima huo kwa kupitia mtelemko wa upande wa kaskazini ambao umeinama zaidi. Alisema,

"Nilipita njia ya mtelemko wa upande wa kusini, ninaona njia hiyo haina maana, kwani baada ya kufika kwenye kilele, bendera iliyoko juu siyo bendera ya taifa la China bali ni bendera za nchi nyingine. Sisi tunachagua njia ya upande wa kaskazini, bendera tunayoichomeka juu ni bendera ya taifa la China."

Kampuni ya magari ya Chery ilisajiliwa rasmi mwaka 1997 ikiwa na mitaji ya Yuan za Renminbi bilioni 1.7, lakini mwezi Desemba mwaka 1999 baada ya kupita miaka miwili, magari yenye nembo ya "Fengyun" yalianza kuzalishwa, ambayo yanalingana na ubora wa magari yaliyozalishwa katika kampuni kubwa za magari za kiubia, lakini bei yake ni pungufu ni zaidi ya 30%, na yakapendwa na watu. Mwaka 2004, idadi ya magari ya Chery yaliyouzwa yalikaribia elfu 90 na kampuni hiyo ilichukua moja ya nafasi kumi za mbele hapa nchini. Ili kuwa na teknolojia muhimu yenye hataza ya China yenyewe, kampuni ya Chery inazingatia sana kuvutia wataalamu hodari. Bw Yin alisema,

"Wataalamu bora wa magari siyo wengi hapa nchini, hivyo sisi tunajitahidi kuwavutia katika kampuni yetu, nilitumia uhusiano wa wenzangu niliosoma nao katika chuo kikuu, uhusiano wa wenzagu wa kazini na kuomba msaada kwa viongozi wetu ili mradi tunajitahidi sana kukusanya wataalamu hodari katika kampuni ya Chery."

Moja ya mafanikio aliyopata Bw. Yin Tongyao katika mpango wake kuhusu wataalamu ni kumpata Dr. Xu Min, ambaye alitoka kwao na alikuwa mtaalamu wa injini wa kampuni ya General Motors Co. na kampuni ya magari ya Ford nchini Marekani. Mwaka 2002 Dr. Xu Min aliporejea kwao kuwaona jamaa zake alialikwa na Bw. Yin Tong kujiunga na kampuni ya Chery, hivi sasa miongoni mwa watafiti kiasi cha 500 wa kampuni ya Chery, kuna wataalamu makumi kadhaa waliowahi kufanya kazi katika makampuni maarufu ya kimataifa yakiwemo Volkswagen na Ford. Kuzalisha magari yenye hataza ya China ni kazi ngumu, Dr. Xu alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa tukitaka kuwa na magari yetu, sharti kwanza tuwe na teknolojia husika, katika kipindi cha mwanzoni, kampuni ya Chery ilipitia wakati mgumu kujifunza. Alisema,

"Mwanzoni tulikutana na shida kubwa. Tulikwenda kuyashawishi makampuni maarufu ya kimataifa kufanya ushirikiano na kampuni yetu na kufanya kazi pamoja nao, baada ya kupita miezi mitatu, waliona uwezo wetu uliongezeka haraka."

Baada ya jitihada za miaka kadhaa, kampuni ya Chery ilipata mafanikio muhimu katika utafiti wa injini, kampuni ya Chery ilitia mitaji ya Yuan bilioni 2 kwa ujenzi wa mradi wa kipindi cha kwanza wa kiwada cha pili cha injini, ambacho kilianza kuzalisha injini mwezi Machi mwaka huu. Injini zinazozalishwa katika kiwanda hicho zimefikia kiwango cha kigezo cha utoaji hewa wa magari cha No. 4 cha Ulaya. Hatua hiyo inaonesha kuwa kampuni ya Chery imekuwa na teknolojia ya kutoka utafiti, kufanya majaribio na uzalishaji wa injini za kiwango cha juu kabisa duniani, na hii ndiyo sababu kwa makampuni makubwa ya kimataifa ya uuzaji wa magari kugombea nafasi ya uwakala wa uuzaji wa magari ya Chery duniani.

Katika nafasi moja iliyojitokeza kwa bahati, Bw. Yin Taongyao aliona uwezo wa ushindani wa magari ya Chery katika soko la magari la kimataifa. Mwaka 2001, mfanya biashara mmoja kutoka Syria baada ya kuona magari ya Chery katika barabara za jiji la Beijing, alijitahidi na kuonana na Bw. Yin Tongyao na kuomba nafasi ya wakala wa uuzaji wa magari ya Chery nchini Syria. Baada ya jitihada za miaka minne, hivi sasa maduka ya magari ya Chery yameongezeka na kufikia 22 nchini Syria, na magari yaliyouzwa huko yamezidi 5000.

Katika ukumbi wa maonesho ya kampuni kubwa kabisa ya uuzaji wa magari nchini Syria, magari ya Chery yanaoneshwa pamoja na magari maarufu ya Benz na BMW. Hivi sasa kuna magari mengi ya Chery katika barabara kubwa za Damascus, mji mkuu wa Syria. Mtu mmoja mwenye gari la Chery alimwambia mwandishi watu wa habari kuwa injini ya gari la Chery ina nguvu sana, tena inatumia mafuta kidogo na vipuri vyake ni rahisi kupatikana

Idhaa ya kiswahili 2005-05-10