Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-05-11 15:27:37    
Mabishano yatokea tena ndani ya serikali ya Israel kuhusu "mpango wa upande mmoja"

cri

Hivi karibuni, waziri wa mambo ya nje wa Israel Bw. Shalom alisema kuwa kama Hamas itashinda katika uchaguzi wa kamati ya utungaji sheria ya Palestina utakaofanyika mwezi Julai mwaka huu, Israel itafikiria upya utekelezaji wa mpango wa upande mmoja. Msimamo huo aliounesha Bw. Shalom mara ulipingwa na waziri wa ulinzi wa Israel Bw. Shaul Mofaz na wengine, akasema kuwa vyovyote matokeo ya uchaguzi huo yatayokuwa, mpango wa upande mmoja lazima utekelezwe. Kauli hizo tofauti zimeleta mabishano kuhusu mpango wa upande mmoja ambao unatakiwa kuanza kutekelezwa karibuni.

Waziri wa mambo ya nje wa Israel, Bw. Shalom alisema maneno hayo ya kushitusha alipokuwa akikutana na waziri wa mambo ya ndani wa Palestina tarehe 9. Alisema kuwa "hakutakuwa na mantiki" kama Hamas ikishinda katika uchaguzi huo wa kamati ya utungaji sheria ya Palesina, kwani mtu yeyote wa Israel asingependa kuona sehemu waliyoondoka inakuwa "nchi ya kifalme ya Hamas".

Maneno aliyosema Bw. Shalom akiwa waziri wa mambo ya nje wa Israel mara yalisababisha mawazo mengi, na watu wengi wanaona kuwa msimamo wa serikali ya Israel kuhusu utekelezaji wa mpango wa upande mmoja pengine utakuwa wa kigeugeu. Upande wa Palestina unashutumu kwamba msimamo huo ni kisingizio cha Israel kuchelewesha kuondoa jeshi lake kutoka Palestina.

Lakini waziri mkuu wa Israel Bw. Sharon mnamo tarehe 9 alipohojiwa na waandishi wa habari alisema kuwa matokeo ya uchaguzi wa kamati ya utungaji sheria hayataathiri utekelezaji wa mpango wa upande mmoja. Hata hivyo alisema, kutokana na kuwa tarehe 25 mwezi Julai ni siku ya huzuni kwa sababu ya kubomolewa kwa sinagogi takatifu la Wayahudi, ili kuzingatia hisia hizo amekubali kuahirisha utekelezaji wa mpango wa upande mmoja hadi katikati ya mwezi Agosti mwaka huu. Tarehe 10 mwezi huu waziri wa ulinzi wa Israel Bw. Mofaz alisema kuwa anakubaliana na Bw. Sharon, kwamba vyovyote matokeo ya uchaguzi wa kamati ya utungaji sheria yatavyokuwa Israel itaondoa makazi ya Wayahudi kutoka sehemu ya Gaza na ukingo wa magharibi wa Mto Jordan.

Bw. Shalom anakukwa kigeugeu kuhusu utekelezaji wa mpango wa upande mmoja. Mwanzoni alikuwa mmoja wa wapinzani wa mpango huo, kisha pole pole alisimama kwenye msimamo wa Sharon. Mwezi Februari mwaka huu, kabla na baada ya Sharon na mwenyekiti wa mamlaka ya utawala wa Palestina Bw. Abass kukutana, Bw. Shalom alimgeuka Sharon na kusema kuwa atafanya awezavyo kuzuia utekelezaji wa mpango huo. Msimamo wake huo ulikuwa mgumu kueleweka kwa watu wengi. Vyombo vya habari vya Israel vilibashiri kuwa mabadiliko ya msimamo wake yanatokana na kuwa Sharon alijitokeza mbele sana katika makutano ya kihistoria na Abass wakati Bw. Shalom aliyeandaa mkutano huo alipuuzwa.

Wachambuzi wanaona kuwa maneno ya Bw. Shalom ya hivi karibuni pia yameonesha kuwa mvutano kati yake na Sharon unaendelea, na vilevile yameonesha kuwa anataka kujipendekeza kwa wapiga kura wa mrengo wa kulia, ili kujiandaa uchaguzi mkuu wa Israel utakaofanyika mwaka kesho.

Lakini aidha kutokana na mtizamo wa mazingira ya kimataifa au kutokana na maslahi ya Israel, utekelezaji wa mpango wa upande mmoja umekuwa kama "mshale uliofyatuliwa" hautaweza kurudishwa tena, hata kama Shalom atakuwa na upinzani wa namna gani mpango huo wa upande mmoja utatekelezwa tu bila mabadiliko yoyote.

Idhaa ya Kiswahili 2004-05-11