Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-05-11 20:19:22    
China yajenga kituo cha kwanza cha kushughulikia takataka za vyakula

cri
Takataka za vyakula huwa ni vyakula vilivyobaki na kutupwa na mikahawa, kwa kuwa takataka za aina hiyo zina mafuta mengi na ni rahisi kuoza, hivyo ni vigumu kuzishughulikia. Ili kutatua tatizo hilo, hivi karibuni wanasayansi wa China wameanzisha kituo cha kwanza cha kushughulikia takataka za vyakula kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya baiolojia. Kituo hicho kinaweza kubadilisha takataka za vyakula kuwa malighafi za kutengenezea mbolea.

Hapa China takataka za vyakula zinachukua nusa ya takataka zote, na takataka za vyakula hutumiwa kama chakula cha nguruwe, lakini kwa kuwa takataka za aina hiyo zina bakteria wengi, nyama ya nguruwe wanaokula takataka hizo sio salama kwa binadamu. Aidha, kama takataka za vyakula zikitunzwa kwa muda mrefu, inzi, mbu na bakteria wanazaliana kwenye takataka hizo, hali ambayo itaathiri mazingira.

Kadiri teknolojia ya kisasa ya baiolojia inavyoendelea, wanasayansi wa China wamepata utatuzi wa suala la takataka za vyakula ambalo limeisumbua miji ya China kwa miaka mingi. Mtaa wa Shangdi uliopo mjini Beijing hivi karibuni ulianzisha kituo cha kushughulikia takataka za vyakula. Kituo hicho kinaweza kushughulikia tani 1.2 ya takataka za vyakula kwa siku, ambazo ni jumla ya takataka za vyakula kutoka kwenye mikahawa 27 midogo na ya wastani mtaani humo kwa siku.

Teknolojia hiyo ya kushughlikia takataka za vyakula ilivumbuliwa na Kampuni ya Teknolojia ya Baiolojia ya Jia Bowen ya Beijing. Mhandisi mkuu wa kampuni hiyo Bw. Xia Yuqiao alifahamisha kuwa, kituo hicho kinashughulikia takataka za vyakula kwa kutumia vijidudu, alisema:

"Tulivikusanya vijidudu hivyo kutoka kwenye milima ya Mkoa wa Si Chuan, na vijidudu hivyo vya kimaubile ni mchanganiko wa aina mbalimbali za vijidudu, kama vikiwekwa kwenye mazingira fulani yenye unyevu na ujoto mwafaka, vinaweza kuumua chakula na kukibadilisha kuwa aina nyingine za vijidudu."

Mwandishi wetu wa habari aliona matanuri 6 kwenye kituo kicho? ambayo yanadhibitiwa kwa kompyuta, ambayo inabadilisha kiwango cha joto ndani ya matanuri hayo; wafanyakazi wanamimina takataka za vyakula kwenye matanuri hayo, na kuweka baadhi ya vijidudu na pumba za ngano kwa kufuata kipimo fulani. Mfanyakazi wa kituo hicho Bw. Li Wenlong alimwambia mwandishi wa habari akisema:

"Tunachanganya vijidudu na pumba za ngano, halafu tunaweka mchaganyiko huo kwenye matanuri hayo yenye joto kali. Baada ya takataka za vyakula zilizomo ndani ya matanuri kuumuka kwa saa nne na nusu au tano, takataka hizo zitakanushwa, halafu zitatolewa."

Alisema kuwa vijidudu vya aina hiyo vitaongezeka kwa kiasi kibuwa katika mazingira mwafaka, wakati vijidudu hivyo vinapoongezeka vinakula takataka za vyakula. Mwandishi wa habari aliona unga weneye rangi ya dhahabu na harufi ya mafuta kutoka kwenye matanuri hayo, na unga huo ndio vijidudu vya aina mpya, na ni malighafi nzuri ya kutengenezea mbolea. Alipougusa unga huo alihisi unga huo haugandi na ni safi sana.

Inafahamika kuwa kama unga huo, yaani vijidudu vya aina mpya ukitiliwa chembechembe ndogo kadhaa, utakuwa mbolea nzuri. Naibu msimamizi mkuu wa Kampuni ya Teknolojia ya Baiolojia ya Jia Bowen ya Beijing alifahamisha kuwa, kwa kuwa vijidudu hivyo vinapoozesha takataka, vinatumia nguvu nyingi, ndiyo maana mbolea iliyotengenezwa kwa kutumia vijidudu vya aina hiyo itafanya kazi kubwa katika kukuza mimea na kuongeza uwezo wake wa kujikinga dhidi ya magonjwa.

"Baada ya vijidudu vya aina hiyo kuingia ardhini, vitaongezeka kwa kasi kubwa kama kutakuwa na ujoto mwafaka, na vijidudu hivyo vitazingira mizizi ya mimea na kuvizuia virusi visiingie kwenye mizizi. Aidha, vijidudu vya aina hiyo vinapoongezeka, mazingira ya sehemu zilizo karibu na mizizi yataboreshwa, na vijidudu hivyo vitahimiza ukuaji wa mizizi, na kuufanya mfumo wa mizizi ustawi, na mimea yenye mifumo mizuri ya mizizi hustawi."

Matokea ya majaribio yameonesha kuwa baada ya kutumia mbolea hiyo, uzalishaji wa stroberi utaongezeka kwa asilimia 30, uzalishaji wa matufaa utaongezeka kwa tani 3 kwa hekta, na utamu wa matunda hayo pia utaongezeka.

Mbali na hayo, teknolojia hiyo mpya pia imetatua suala la hali ya usafi kwenye mikahawa, ambalo lilikuwepo kwa muda mrefu. Bw. Ge Ping, ambaye anaendesha mkahawa mmoja kwenye mtaa wa Shangdi, alimwambia mwandishi wa habari kuwa kabla ya kuanzishwa kwa kituo hicho cha kushughulikia takataka za vyakula, mkahawa wake haukuweza kushughulikia takataka za vyakula kabla ya wateja wote hawajaondoka, na takataka hizo zilikuwa zinatoa harufu mbaya kutokana na kutunzwa kwa siku nzima, hali ambayo iliathiri mazingira ya mkahawa, naye alikuwa ana wasiwasi kuhusu hali hiyo. Baada ya kuanzishwa kwa kituo hicho kwenye mtaa huo, kituo hicho kinapaleka magari kwenye kila mkahawa wa mtaa huo kukusanya takataka mara mbili au tatu kwa siku.

"Hivi sasa, gari la kituo cha takataka linakuja mara tatu kwa siku kukusanya takataka, hali ya takataka kutoka harufu mbaya kutokana na kutunzwa kwa muda mrefu haipo tena , na mazingira ya jiko la mkahawa wangu yameboreshwa kwa kiasi kikubwa."

Baada ya kukikagua kituo hicho, wataalamu wanakubaliana kuwa njia hiyo ya kushughulikia takataka za vyakula si kama tu inahakikisha usafi wa mazingira na usalama wa chakula, bali pia inazifanya raslimali zitumiwe tena, yaani kubadilisha takataka kuwa mbolea ambayo inawezakuongeza uzalishaji wa kilimo.

Habari zinasema kuwa njia hiyo ina mustakbali mzuri nchini China. Serikali ya Beijing itaeneza njia hiyo ili kuboresha mazingira ya mji kwa kukaribisha Michezo ya Olympiki ya mwaka 2008; na jiji la Shanghai na Wuhan na majiji mengine ya China pia yatajenga vituo vya takataka za vyakula kama kile cha Beijing.

Idhaa ya Kiswahili 2005-05-11