Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-05-11 21:09:35    
Kupika vipande vya kuku pamoja na pilipili hoho

cri

Mahitaji

Nyama ya kidari cha kuku gramu 300, tango moja, kitunguu saumu gramu 5, unga wa tangawizi gramu 10, vipande vya vitunguu maji gramu 10, pilipili hoho gramu 15, mchuzi wa soya gramu 20, chumvi gramu 3, mvinyo wa kupikia gramu 10, siki gramu 5, ute wa yai gramu 15, supu ya kuku gramu 25, mafuta yaliyokwisha chemshwa gramu 50.

Njia

1. Kausha mafuta yaliyoko kwenye nyama na uondoe manyoya yaliyobaki kwenye nyama ya kuku, ondoa ngozi, kisha ipigepige kwa mgongo wa kisu iwe laini, ikate iwe vipande vya mraba kwa ukubwa wa sm 2 kila kimoja, na kuviweka kwenye bakuli. Kata tango liwe vipande vipande. Tia chumvi, mchuzi wa soya na ute wa yai, korogakoroga ili vitu hivyo vichanganyike sawasawa, na ikate pilipili hoho kuwa vipande vyenye urefu wa cm 2.

2. Pasha moto, gramu 100 za mafuta yaliyokwisha chemshwa hadi yawe na joto la nyuzi 60 hivi, tia pilipili hoho hadi iwe na rangi nyekundu-kahawia, tia vipande vya nyama ya kuku, korogakoroga mpaka vigawanyike, kisha tia kitunguu saumu, tangawizi na vitunguu maji na kumimina mchuzi wa sosi, siki, mvinyo wa kupikia, supu ya kuku, tia chumvi, sukari, tikisa na korogakoroga, halafu tia vipande vya tango. Mpaka hapo, kitoweo hiki kinakuwa tayari kupakuliwa na kuliwa.