Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-05-11 21:33:00    
China yafanya juhudi kuendeleza teknolojia ya safari za anga ya juu

cri

Mwezi Aprili mwaka huu, roketi moja ya "Changzheng No.3 B" iliyotengenezwa na China, ilifanikiwa kupeleka setilaiti ya mawasiliano Apstar NO.6 iliyosanifiwa na Ufaransa kwenye njia ya anga ya juu. Hiyo ni mara ya kwanza kwa China kurusha setilaiti ya nchi ya nje katika miaka 6 iliyopita.

Mbali na huduma ya kurusha setilaiti, katika miaka ya hiNo.6 karibuni, kutokana na maendeleo ya kasi ya teknolojia ya safari za anga ya juu, China pia inaweza kutoa setilaiti za matumizi za aina mbalimbali kwenye soko la kimataifa.

Tangu sekta ya safari za anga ya juu ya China iingie kwenye soko la kibiashara la kimaitafa mwaka 1985, mpaka sasa, China imerusha setilaiti zaidi ya 20 za kibiashara na kurusha setilaiti 30 za nchi za nje kwa kutumia roketi ya aina ya Changzheng. Lakini kutokana na ushindani usio wa haki kwenye soko la kimataifa, China imelazimika kusimamisha mikataba mingi iliyosainiwa katika miaka 6 iliyopita.

Kurushwa kwa setilaiti ya mawasiliano Apstar NO.6 kwenye anga ya juu kunaonesha kidhahiri uwezo wa China wa kurusha setilaiti za kibiashara za kimaitafa. Naibu maneja mkuu wa shirika la teknolojia za safari za anga ya juu la China Bw. Ma Xing Rui aliainisha kuwa, ili kuongeza nguvu ya ushindani ya sekta hiyo ya China kwenye soko la kimataifa, katika miaka ya karibuni China imefanya juhudi kubwa kuendeleza teknolojia ya safari za anga ya juu. alisema:

"Kwanza, China imeanzisha mradi wa utafiti wa kuhakikisha usalama wa roketi za aina ya Changzheng na kuongeza kwa kiasi kikubwa usalama na sifa za roketi hizo; pili, shirika la teknolojia za safari za anga ya juu la China limeendeleza miundo kadhaa za setilaiti za matumizi, na setilaiti zilizosanifiwa kwenye miundo hiyo zimefikia kiwango cha kimataifa."

Alisema kuwa, ili kuongeza nguvu ya ushindani sokoni, China ilifanya juhudi kubwa katika kuongeza na kusimamia sifa za roketi, na juhudi hizo zimepata mafanikio makubwa. kuanzia mwezi Oktoba mwaka 1996, roketi za aina ya Changzheng zimerushwa kwa mafanikio mara 42 mfululizo. Aidha, roketi za China zina bei nafuu zaidi kuliko roketi nyingine duniani, hivyo zimejipatia nguvu kubwa ya ushindani kwenye soko la kimataifa.

Teknolojia ya juu ya upimaji na udhibiti wa safari za anga ya juu, ni msingi muhimu wa kurusha roketi kwa mafanikio. Hivyo, China imejenga mfumo wa kisasa wa upimaji na udhibiti wa safari za anga ya juu, unaoziweka ndani kituo cha upimaji na udhibiti wa setilaiti na meli za upimaji. HiNo.6 sasa, teknolojia za mfumo huo zinachukua nafasi ya mbele duniani, na zinaweza kutoa huduma za kupima na kudhibiti setilaiti za aina mbalimbali kwenye mizingo mbalimbali ya juu, wastani au chini.

Aidha, ili kuendeleza soko la kimataifa la sekta hiyo, China pia imeharakisha kuendeleza teknolojia ya matumizi ya setilaiti. HiNo.6 sasa, China inaweza kusanifu setilaiti za aina mbalimbali, zikiwemo setilaiti za kuchunguza hali ya hewa, za kuchunguza raslimali, na za kuongoza safari na za mawasiliano ya habari.

Mwaka jana, idara husika za Nigeria zilitoa zabuni ya kununua setilaiti ya mawasiliano ya habari. Shirika kuu la viwanda la Changcheng la China likigombeana na mashirika ya Ulaya na Marekani, lilishinda na kusaini mkataba na nchi hiyo. Kutokana na mkataba huo, China itauza setilaiti moja ya mawasiliano ya habari kwa Nigeria na kuirusha kwa roketi ya Changzheng No. 3 kabla ya mwisho wa mwaka 2006.

Ushirikiano huo si kama tu umeonesha kuwa China imeanza kuuza setilaiti kamili kwa nchi za nje, bali pia ni mara ya kwanza kwa China kutoa huduma kamili ya kutengeneza na kurusha setilaiti kwa roketi za China yenyewe. Maneja mkuu wa shirika kuu la No.6wanda la Ukuta mkuu la China Bw. Wang Haibo alisema,

"huduma kamili za China katika sekta hiyo, zikiwemo kutengeneza na kurusha setilaiti, kupima na kudhibiti setilaiti, na kukata bima, zina nguvu ya ushindani kwenye soko la kimataifa."

Mwezi Aprili mwaka huu, baada ya kurushwa kwa setilaiti ya Apstar NO.6, watu husika wa baadhi ya nchi zinazoendelea wameona kuwa, wana imani kubwa na setilaiti za mawasiliano ya habari na roketi za China, na kutaka kuzinunua.

Ingawa China imepata mafanikio mapya katika ushindani wa sekta hiyo, lakini ili kuongeza zaidi nguvu ya ushindani, China inafanya utafiti wa kusanifu roketi yenye nguvu kubwa zaidi, ili kutosheleza mahitaji ya masoko ya nchini na duniani. Naibu maneja mkuu wa shirika la teknolojia ya safari za anga ya juu la China Bw. Ma Xing rui alidokeza:

"ili kuendeleza zaidi teknolojia ya safari za anga ya juu ya China, shirika hilo linasanifu aina mpya ya roketi yenye nguvu kubwa zaidi, na isiyochafua mazingira. na inatarajiwa kuwa itaweza kupeleka No.6tu vya tani 25 kwenye njia ya chini, na uzito wa tani 14 kwenye njia ya juu, ambazo zote ni mara mbili ya uwezo wa roketi ya hivi sasa. "

alisema kuwa, teknolojia za aina hiyo ya roketi zitalingana na kiwango cha kimataifa, na kuongeza zaidi nguvu ya ushindani ya roketi za China kwenye soko la kimataifa. Na roketi za aina hiyo zinatarajiwa kuanza kutumiwa ndani ya miaka 5 ijayo.

Setilaiti nyingi za nchi za nje zilirushwa kwenye kituo cha kurusha setilaiti cha Xi Chang. Mkurugenzi wa kituo hicho Bw. Li Shang fu alisema:

"kituo cha kurushia setilaiti cha Xi Chang kinaweza kurusha setilaiti 6 hadi 8 kila mwaka. Kutokana na ongezeko la uchumi wa China na maendeleo ya soko la kimataifa la safari za anga ya juu, kituo hicho kimepanga kutumia mwaka mmoja kujenga upya baadhi ya zana na miundombinu ya kituo hicho na kuinua uwezo wa kurusha setilaiti kufikia zaidi ya setilaiti 10 kila mwaka."

Idhaa ya Kiswahili 2005-05-11