Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-05-11 22:30:32    
Shughuli za utafiti katika mradi wa kwanza wa utafiti kwenye mabahari ya dunia

cri
Shughuli za utafiti katika mradi wa kwanza wa utafiti kwenye mabahari ya dunia zinafanyika hivi sasa kwenye upande wa magharibi wa bahari ya Pasifiki. Kikundi cha utafiti wa sayansi cha China kimepata takwimu za uchunguzi pamoja na sampuli za madini na mazingira ya chini ya bahari, na kuweka chupa nne zinazoelea juu ya maji zenye ujumbe wa salamu za wachina kwa watu wa duniani.

Shughuli hizo za utafiti zilizoendelea kwa siku karibu 300 kwenye mabahari ya dunia zilianza kutoka mji wa Qingdao tarehe 2 mwezi Aprili,. Siku yake ya pili meli ya utafiti inayojulikana kama "Bahari No. 1" ilitoa nanga na kuelekea sehemu iliyonuiwa, ambapo watu wa kikundi hicho walifanya mazoezi ya kikazi ya aina mbalimbali. Tarehe 5 mwezi Aprili meili hiyo iliingia kwenye bahari ya Pasifiki bila matatizo yoyote.

Baada ya kusafiri kwa wiki moja, meli ya utafiti ya "Bahari No. 1" ili wasili kwenye sehemu ya kazi tarehe 10 mwezi Aprili, saa nane usiku walianza kukagua mfumo wa winchi na mfumo wa kupiga picha chini ya bahari kama kuna vijitundu vinavyoweza vya kupenyeza maji, kazi hiyo ilimalizika mnamo saa 12 jioni ya siku ya pili, ambapo kazi ya kuchukua sampuli chini ya bahari ilianza. Hadi usiku wa tarehe 15, kikundi cha utafiti cha sayansi kilimaliza kazi za kuchimba sehemu kadhaa chini ya bahari kwa kufuata mpango uliowekwa.

"Tarehe 13 mwezi Aprili, watu waliojisikia kizunguzungu kutokana na mawimbi makubwa ya baharini walirudia katika hali ya kawaida, na watu wote waliokuwamo katika meli hiyo walifurahi." Kamishna wa kamati ya muda ya chama ya meli hiyo Bw. Zhang Baoming alisema.

Katika siku zile upepo ulikuwa mkubwa na kufikia nyuzi 7 na ulifikia nyuzi 8 katika baadhi ya nyakati, hali hiyo ilileta msukosuko kubwa kwa meli hiyo kuweza kutia nanga kwenye sehemu inayotakiwa na kufanya shughuli za uchunguzi.

Tarehe 16 mwezi Aprili, sherehe fupi ya kuweka kwa mara ya pili chupa zinazoelea juu ya maji ya bahari ilifanyika baada ya chupa ya kwanza iliyowekwa kwenye maji ya bahari siku chache baada ya kufunga safari ya kuelekea kwenye sehemu ya kufanya uchunguzi na utafiti. Kwa kuangaliwa na wachunguzi na wanamaji wa meli hiyo, mwanasayansi wa kwanza Bw. Wang Chunsheng, mkuu wa meli Bw. Lu Huisheng na kamishna Zhang Baoming walitupa chupa 3 kwenye maji ya bahari, ambazo zitaelea kwenye maji ya bahari zikichukua ujumbe wa salamu na kusafiri katika nchi baadhi duniani.

Kutokana na kuwa hivi sasa hewa inayozungukazunguka bado iko katika sehemu ya kazi ya upande wa magharibi wa bahari ya Pasifiki, hivyo meli ya "Bahari No. 1" itachagua sehemu mwafaka ya kufanya uchunguzi na utafiti kwa kipindi kijacho.

Idhaa ya Kiswahili 2005-05-11