Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-05-12 16:10:08    
Hali ya nyuklia ya pennisula ya Korea yawe ya utatanishi

cri

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Korea ya Kusini tarehe 11 alitangaza kuwa, Korea ya Kaskazini hivi karibuni imemaliza kazi ya kuondoa fimbo 8000 zilizokwisha kutumika kuzalisha nishati ya nyuklia kutoka kwenye zana za nyuklia huko Ongbyon, na kusema kuwa itaendelea kuchukua hatua za lazima ili kupanua ghala la silaha za nyuklia kwa lengo la kujilinda kutokana na hali ya hivi sasa. Hii ni hatua mpya iliyochukuliwa na Korea ya Kaskazini kupambana na Marekani kuhusu suala la nyuklia, na imeleta utatanishi zaidi katika hali ya nyuklia ya Pennisula ya Korea.

Kufualitiwa kwa hatua hiyo ya Korea ya Kaskazini kunatokana na sababu kuwa, kutokana na makisio ya Marekani, Korea ya Kaskazini imepata silaha 5 hadi 8 za nyuklia. Kama Korea ya Kaskazini ikiendelea na shughuli hiyo, bila shaka itaweza kupanua zaidi ghala lake la silaha za nyuklia. Aidha, afisa wa Marekani asiyetaka kutajwa jina lake aliwahi kutangaza kuwa, huenda Korea ya Kaskazini inajiandaa kufanya majaribio ya nyuklia. Ingawa hatua hiyo haijathibitishwa, lakini wasiwasi upo. Kutokana na hali hiyo, hatua hiyo iliyotangazwa na Korea ya Kaskazini imeleta utatanishi katika suala la nyuklia la pennisula ya Korea.

Lakini wachambuzi wanaona kuwa, bado ni mapema kubaini kama Korea ya Kaskazini kweli itachukua hatua halisi kama ilivyotangaza. Kwanza, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo siku hiyo pia alitaja mkataba wa kimsingi wa nyuklia kati ya Korea ya Kaskazini na Marekani, ambao ulifikiwa kwa mazungumzo ya moja kwa moja kati ya nchi hiyo na serikali ya Clinton ya Marekani. Ingawa serikali ya Bush ya Marekani imesisitiza mara kwa mara kuwa haitashughulikia suala hilo kwa kufuata njia ya serikali ya Clinton, lakini Korea ya Kaskazini inashikilia kuwa njia hiyo itasaidia kutatua suala hilo.

Aidha, Korea ya Kaskazini ilikataa fununu ya majaribio ya silaha ya nyuklia kupitia gazeti la Rodong Sinmun, na kulaani kuwa kitendo hicho cha Marekani ni propaganda inayopinga Korea ya Kaskazini. Baadhi ya wachambuzi wameona kuwa, majaribio ya silaha ya nyuklia ni hatua ya mwisho kwa Korea ya Kaskazini, kama hatua hiyo ikitekelezwa kihalisi, bila shaka itavuka kikomo cha uvumilivu wa pande mbalimbali. Hivyo Korea ya Kaskazini inachukua tahadhari kuhusu suala la majaribio hayo, na kuweka mkazo katika suala la fimbo zilizokwisha kutumika kuzalisha nishati ya nyuklia, hatua hiyo inalenga kujiongeza nguvu ya kufanya usuluhishi.

Baada ya kuchukuliwa kutoka kwenye zana za nyuklia, fimbo hizo zilizokwisha kutumika kuzalisha nishati ya nyuklia bado zinahitaji muda wa miezi 2 hadi 3 kupoa kabla ya kushughulikiwa tena. Hivyo miezi kadhaa ijayo ni kipindi muhimu kwa suala hilo, Korea ya Kaskazini inaweza kutumia kipindi hicho kuchagua hatua zake kwa mujibu wa jisi Marekani itakavyokuwa.

Marekani inataka suala hilo litatuliwe mapema kwa mazungumzo ya pande 6. Baada ya kukwama kwa mazungumzo hayo, hivi karibuni Marekani imelegeza msimamo wake. Lakini bado haijaondoa uwezekano wa kulifikisha suala hilo kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, na kutangaza kuwa Marekani ina nguvu kubwa ya kuzuia mpango wa nyuklia wa Korea ya Kaskazini. Kutokana na migongono kati ya pande hizo mbili kuongezeka, mwelekeo wa suala hilo bado haujakuwa wazi.

Jumuiya ya kimataifa inatazamia kurejeshwa mapema kwa mazungumzo ya pande 6, na hivi karibuni pande mbalimbali zimeongeza nguvu ya kufanya usuluhishi.

Wachambuzi wanaona kuwa, sababu ya kimsingi ya kukwama kwa utatuzi wa suala hilo ni kutoaminiana kati ya Marekani na Korea ya Kaskazini. Kama pande husika, hasa Korea ya Kaskazini na Marekani, zikiweza kujizuia, na kuchukua hatua zenye unyumbufu kwa udhati na uaminifu, mazungumzo ya pande sita yanaweza kurejeshwa.

Idhaa ya Kiswahili 2005-05-12