Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-05-13 15:48:37    
Watu wa fani mbalimbali wa Italia waikumbuka vita dhidi ya ufashisti.

cri

Baada ya miaka 60 kupita, vita kuu ya pili ya dunia si kama tu haijasahaulika, bali pia imeongezewa maana mpya na wapenda amani. Lakini hadi leo, ufashisti bado upo, hasa nchini Italia ambako ndiyo chanzo chake, wajanja wachache wa kisiasa wanajaribu kupotosha mambo na kuwasahaulisha binadamu historia. Je binadamu wanapaswa kuichukulia vipi vita kuu ya pili ya dunia?

Mkuu wa chuo kikuu cha John Kabert cha Rome Bwana James F. Creagan alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari alisema:

"Mjomba wangu alikuwa mmoja wa askari wa Marekani waliopambana vita katika Saleno nchini Italia, walikaribishwa sana na wananchi wa Italia. Mimi naona kuwa, vita dhidi ya ufashisti duniani ni vita ya wananchi wa nchi mbalimbali zikiwemo China na Italia kupigania uhuru."

Katika vita hiyo, askari wengi vijana walitoa mhango. Katika makaburi ya jeshi la Marekani la Sicily kwenye kitongoji cha Rome, askari zaidi ya elfu kumi wa Marekani walizikwa huko waliokufa katika medani ya Italia wakati wa vita kuu ya pili. Mwandishi wetu wa habari alimkuta askari mstaafu wa vita kuu ya pili Bwana Joseph Bevilacqua aliyefika huko kwa makusudi kutoka Marekani kutoa heshima yake kwa wenzake waliokufa. Alisema kuwa, watu wote waliozikwa kwenye makaburi hayo walikuwa ni vijana wenye umri kuanzia miaka 18 hadi 25. Wakati huo dunia nzima ilipigana vita takatifu dhidi ya ufashisti, vijana hao waliondoka nyumbani na kusafiri kwa mbali kufika huko bila ya kujua hatima yao.

Bw. Joseph aliona kuwa ingawa vita dhidi ya ufashisti ni ya haki, lakini vita yenyewe imemwachia kovu la moyo. Alisema kwa sababu aliwahi kushuhudia ukatili ulivyo wa vitahiyo anapinga kabisa mgogoro wa aina yoyote ya kijeshi.

Askari mstaafu wa Uingereza Bwana Fewell alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari alionesha kuwa na mawazo sawa na Bw. Joseph. Bw. Fewell aliwahi kushiriki katika vita ya kisiwa cha Sicily, alikamatwa na jeshi la Ujerumani, na kutiwa mdani ya kambi ya matekwa ya Nazi kwa miaka miwili. Aliona kuwa, ni mtu aliyewahi kushiriki tu katika vita ndiye anayethamani amani.

Lakini jambo linalowaumiza zaidi askari hao wastaafu ni kwamba, katika miaka ya karibuni, katika nchi za Ujerumani, Japna na Italia, wajanja wachache wa kisiasa walijaribu kupotosha historia, na kuwapa heshima wafashisti.

Profesa wa historia wa chuo kikuu cha Saint John cha Rome Bwana David Miller aliainisha kuwa, nchini Italia , katika miaka ya karibuni wajanja wachache wa kisiasa wanajaribu kuwasahaulisha watu wa vizazi vipya historia ya ufashisti kutokana na maslahi yao binafsi ya kisiasa. Lakini watu lazima wakumbuke historia kwa ajili ya maendeleo ya Italia.

Ni jambo la kufurahisha kwamba, baada ya kumalizika kwa vita kuu ya pili, watu wa kawaida wa Italia walioteseka vya kutosha vitani siku zote wanajihadhari na ufashiti. Hivi karibuni, vituo vikuu vya televisheni vya Italia vimeonesha vipindi vingi kuhusu vita kuu ya pili, washiriki na walioshuhudia vita hiyo pia wamewafahamisha vijana mambo halisi ya zamani kwa kupitia vyombo vya habari.

Mchambuzi maarufu wa mambo ya kisiasa wa Italia Bwana Franco Pavoncello alisema kuwa, maumivu makubwa yaliyosababishwa na vita kwa binadamu yamewapa wajibu wapenda amani, kwamba lazima wawakumbushe watu wa vizazi vijavyo maafa makubwa yaliyoletwa na ufashisti kwa binadamu.

Idhaa ya kiswahili 2005-05-13