Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-05-13 16:41:51    
Sanamu za Udongo

cri

  

Udongo unaweza kufinyangwa kuwa sanamu. Siku za zamani, watoto wa vijijini walipenda sana kufinyanga sanamu. Kama wangekuwa na sanamu za udongo wangefurahi mno.

Sanamu za udongo zina maumbo kemkem: ya wachezaji opera, maisha ya kila siku, ndege na wanyama. Sanamu za kienyeji zinawasaidia watoto kufahamu ulimwengu na kuwapa mwamko wa elimu ya awali.

  

Njia ya kutengeneza sanamu za udongo ni rahisi. Kwanza fundi anachanganya udongo wa kunatanata na mchanga (sehemu moja kwa kumi), anakanda udongo na kutengeneza sanamu. Baada ya kuzianika na kuzikausha kivulini, zinapelekwa kuchomwa kwenye tanuri. Wakati wa mchezo wa kufinyanga sanamu, watoto wanatia udongo uliokandwa ndani ya kalibu, kisha wanazigongagonga kalibu ili sanamu zitoke.

  

Mafundi wa kutengeneza sanamu wameadimika siku hizi. Fundi Zhang Junshi mwenye umri wa miaka 68 kutoka Wilaya ya Peixian, Jimbo la Jiangsu alianza kutengeneza sanamu tangu utotoni mwake na hadi leo yungali anashughulikia sanaa hiyo. Sanamu alizotengeneza zina maumbo ya kupendeza ya waumini wa dini, wahusika wa hekaya, wahusika wa riwaya, ndege, samaki na wadudu. Sanamu za wahusika 108 wa riwaya ya "Kando ya Maji" ambazo zilitengenezwa na Zhang ziliingizwa kwenye maonyesho ya sanaa ya jadi yaliyoandaliwa na Wizara ya Utamaduni.

Idhaa ya Kiswahili 2005-05-13