Viongozi wa nchi 6 za Afrika za Libya, Sudan, Misri, Nigeria, Chad na Gabon pamoja na katibu mkuu wa Umoja wa nchi za kiarabu Amr Musaa tarehe 16 wamekutana huko Tripoli, mji mkuu wa Libya wakifanya majadiliano kuhusu suala la Darfur la Sudan. Hii ni hatua nyingine kubwa inayochukuliwa na nchi za Afrika kwa ajili ya kuondoa mgogoro wa Darfur la Sudan baada ya mkutano wa wakuu wa nchi 5 za Afrika uliofanyika nchini Libya.
Sehemu ya Darfur iko magharibi ya Sudan. Tokea mwezi Februali mwaka 2003, vurugu za vita za sehemu hiyo zilisababisha vifo na majeruhi ya watu wengi. Chini ya usuluhishi wa jumuiya ya kimataifa, serikali ya Sudan na jeshi la upinzani zilifanya mazungumzo mara kwa mara, ambayo bado hayajaweza kupata maendeleo halisi kwa ajili ya kukomesha vita.
Ofisa moja wa ubalozi wa Sudan nchini Misri tarehe 15 alipohojiwa kwenye simu na mwandishi wa habari wa Shirika la habari la Xinhua alisema kuwa, mkutano wa wakuu wa tarehe 16 ni hatua nyingine kubwa inayochukuliwa na nchi za Afrika katika kuondoa mgogoro wa Darfur. Mkutano huo utasisitiza kupinga nguvu za nje kuingilia kati mambo ya ndani ya Sudan kwa kisingizio cha suala la Darfur, na kusisitiza kuwa lazima suala hilo litatuliwe ndani ya Umoja wa Afrika.
Habari zinasema kuwa, mkutano huo utajadili hasa namna ya kuisaidia Sudan kukabiliana na hali mpya baada ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kupitisha azimio No.1593. Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa tarehe 31 Machi lilipitisha azimio la No.1593 la kuamua kuwa maofisa wa kijeshi na kiserikali wa Sudan na wanamgambo na wapinzani waliofanya uhalifu wa kivita na kupinga binadamu katika sehemu ya Darfur watahukumiwa kwenye mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai. Baadaye serikali ya Sudan ilitangaza kulipinga kabisa azimio hilo. Nchi kadhaa za Afrika ikiwemo Misri zinaona kuwa, kama sheria italindwa kwa haki, idara za sheria za Sudan zinaweza kuwahukumu watuhumiwa walifanya uhalifu wa vita katika sehemu ya Darfur, lakini siyo suala hilo liwasilishwe kwenye mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai.
Zaidi ya hayo, mkutano huo pia utajadili namna ya kuboresha hali ya usalama ya sehemu ya Darfur. Hali ya sehemu hiyo bado ni mbaya kwa hivi sasa, ambapo watoaji misaada ya kibinaadamu wanashambuliwa mara kwa mara, hata lilitokea tukio la kuwateka nyara watu wa kikosi cha Umoja wa Afrika cha kufanya usimamizi wa kusimamisha vita. Inatazamiwa kuwa mkutano huo wa wakuu wa nchi 6 za Afrika utalihimiza jeshi la upinzani la Darfur lifanye ushirikiano na serikali ya Sudan, ili kuhakikisha kazi ya utoaji misaada ya kibinaadamu inaweza kufanyika bila vikwazo.
Katibu mkuu wa Umoja wa nchi za kiarabu Bwana Amr Musaa tarehe 15 huko Cairo aliwaambia waandishi wa habari kuwa, safari hii amealikwa na kiongozi wa Libya Muamar Gadhafi, anaona hili ni jaribio moja muhimu la Umoja wa nchi za kiarabu kushiriki kwenye utatuzi wa suala la Afrika. Msemaji wa Bwana Musa pia alisema kuwa, ushirikiano kati ya Umoja wa nchi za kiarabu na Umoja wa Afrika ni muhimu sana kwa pande hizo mbili, na pande hizo mbili zinatumai kuwa mkutano huo utakuwa hatua kubwa inayoweza kuondoa mgogoro wa Darfur.
Tarehe 11 Mei, huko Tripoli, chini ya usuluhishi wa kiongozi wa Libya Muammar Gadhafi, wajumbe wa makundi mawili ya upinzani ya Darfur na serikali ya mtaa ya Darfur walisaini makubaliano yasiyo rasmi kuhusu kusimamisha vita na utoaji misaada ya kibinaadamu, ambapo makundi hayo mawili yametoa taarifa ya pamoja ikisema kutaka kurudisha mazungumzo ya amani na serikali ya Sudan. Ni matumaini kwa, mkutano wa wakuu wa nchi 6 za Afrika unaofanyika tarehe 16 utaleta fursa mpya katika kuondoa mgogoro wa Darfur.
Idhaa ya Kiswahili 2005-05-16
|