Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-05-17 15:11:04    
Guangxi inakuza maendeleo ya uchumi kwa kutumia ubora wa huko

cri

Mkoa unaojiendesha wa kabila la wazhuang, ambao uko katika sehemu ya kusini magharibi ya China, ni mkoa pekee nchini unaopakana na nchi za Asia ya kusini mashariki kwenye nchi kavu na pwani. Mwaka 1992 serikali ya China iliamua kuuchukulia mkoa wa Guangxi kuwa njia ya kutokea baharini kwenye sehemu ya kusini magharibi ya China.

Upande wa mashariki ya mkoa wa Guangxi ni sehemu iliyoendelea kiuchumi nchini China, upande wa kusini magharibi wa mkoa huo ni mpaka wenye urefu wa kilomita zaidi ya elfu moja kati ya China na Vietnam, hivyo mkoa wa Guangxi umekuwa na ubora wa kijiografia. Naibu mkuu wa mkoa huo Bw. Guo Shengkun alisema,

"Kijiografia, mkoa wa Guangxi una hali yake bora na umekuwa moja ya sehemu muhimu inayounganisha China na Asia ya kusini mashariki."

Habari zinasema kuwa hivi sasa mkoani Guanxi kuna miji 12 na bandari 21 zenye forodha. Barabara mbili kati ya barabara tatu za China zinazokwenda kwenye nchi za Asia ya kusini mashariki kupitia Vietnam ziko mkoani Guangxi. Mbali na hayo, kuna usafirishaji mwepesi wa baharini na angani kati yake na nchi za Asia ya kusini mashariki.

Mji wa Dongxing ni moja ya miji ya mkoa huo yenye forodha, ambao unatazamana na mji wa Mangjie kwenye kando mbili za mto Beilun. Mwandishi wetu wa habari katika mji wa Beilun aliona kuwa kila hata kabla ya kupambazuka kuna mamia kadhaa ya watu wanaosubiri kwenye forodha wakitaka kwenda nchi ya nje. Wafanyakazi wa forodha ya Dongxing walisema kuwa wakazi hao wana maduka kwenye mtaa wa Mangjie nchini Vietnam, watu hao wanaharaka ili kutaka kuwahi kufungua maduka yao mepema. Mkazi ajulikanaye kwa jina la Liao Xin, ambaye alifungua duka lake miaka mitano iliyopita, alimwambia mwandishi wetu wa habari,

"Kila siku tunafanya hivyo, forodha inafunguliwa kila siku mnamo saa mbili, kwa kawaida tunafika hapa kupanga mstari saa 12." Bw. Liao alisema kuwa katika mji wa Dongxing kuna watu zaidi ya elfu 1 wanaofanya biashara katika nchi ya nje. Vivyo hivyo, idadi ya watu wa Vietnam wanaofanya kazi katika mji wa Dongxing pia kubwa. Wafanyabiashara wa China na Vietnam wa kando mbili za mto Beilun wanaruhusiwa kwenda na kurudi bila matatizo yoyote. Hivi sasa forodha ya Dongxing imekuwa moja ya forodha muhimu kwenye nchi kavu, ambayo idadi ya watu wanaopita inachukua nafasi ya tatu nchini, na thamani ya biashara na nchi za nje ilizidi Yuan za Renminbi bilioni 2 kwa mwaka.

Dongxing ni moja ya mifano ya miji iliyopata maendeleo ya biashara ya mpakani. Hivi sasa bidhaa muhimu za mkoa wa Guangxi zinazosafirishwa kwa nchi za Asia ya kusini mashariki ni pamoja na nguo, vyombo vya umeme na mitambo, wakati Guangxi inanunua mazao ya mengi ya kilimo na mali-ghafi zinazotumika viwandani.

Miaka mitatu iliyopita China na Umoja wa Nchi za Asia ya Kusini Mashariki zilisaini mkataba wa kanuni za ushirikiano wa uchumi na kuanzisha eneo la biashara huria kati ya China na umoja huo, jambo ambalo limeleta fursa mpya ya maendeleo kwa mkoa wa Guangxi. Ili kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na nchi za Asia ya kusini mashariki, mkoa wa Guangxi unaboresha miundo-mbinu na mazingira ya uwekezaji, hususan mawasiliano na mkoa huo.

Kutokana na kuwa sura ya ardhi ya mkoa wa Guangxi ni yenye matatizo mengi, hivyo tokea zamani mawasiliano yalikuwa suala linalokwamisha maendeleo ya uchumi wa Guangxi. Hivyo kuboresha mawasiliano kulikuwa suala muhimu linalotakiwa kutatuliwa haraka. Takwimu zinaonesha kuwa katika miaka ya karibuni mkoa wa Guangxi ulitenga fedha nyingi kuimarisha ujenzi wa miundo-mbinu ya mkoa huo, katika mwaka jana Guangxi iliwekeza karibu Yuan bilioni 1.3 katika ujenzi wa barabara. Naibu mkuu wa mkoa wa Guangxi Bw. Guo Shengkun alisema,

"hivi sasa tunafungua mlango zaidi kwa nchi za nje hususan kuimarisha ujenzi wa mawasiliano ili tuwe na njia pana na yenye usalama na ufanisi mkubwa inayounganisha mkoa wa Guangxi na nchi za Asia ya kusini mashariki na kukuza maendeleo ya uchumi."

Katika miaka ya karibuni, hali bora ya mkoa wa Guangxi imeleta maendeleo ya biashara ya nje na uwekezaji, vilevile imehimiza maendeleo ya sekta za utalii na huduma. Hivi sasa mkoa wa Guangxi umetembelewa na watalii wengi kutoka nchi za nje, hususan kutoka nchi za Asia ya kusini mashariki. Takwimu inaonesha kuwa katika mwaka jana, idadi ya watalii waliotembelea Guangxi ilifikia milioni 1.15 na kuwa na pato la dola za kimarekani milioni 300. Kwa upande mwingine mkoa wa Guangxi umekuwa njia muhimu kwa watalii wa China wanaotembelea nchi za Asia ya kusini mashariki, wastani wa idadi ya watalii wa China wanaotembelea nchi za nje kwa kupitia mkoa wa Guangxi umezidi watu laki 5 kwa mwaka.

Habari zinasema kuwa mkoa wa Guangxi unachangia maendeleo ya uchumi kwa njia mbalimbali zikiwa ni pamoja na kuandaa semina ya lugha za kigeni bila malipo. Mwezi Novemba mwaka 2004, maonesho ya biashara ya kwanza ya China na Umoja wa Nchi za Asia ya Kusini Mashariki yalifanyika huko Nanning, mji mkuu wa mkoa wa Guangxi, ambayo yalileta fursa mpya kwa mkoa huo kujionesha kwa nchi za nje.

Idhaa ya kiswahili 2005-05-17