Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-05-17 15:13:25    
Mazungumzo kati ya serikali ya Korea ya Kaskazini na Korea ya Kusini yameanza tena

cri

Mazungumzo yaliyosimamishwa kwa karibu mwaka mmoja kati ya serikali ya Korea ya Kaskazini na Korea ya Kusini yameanza tena tarehe 16 katika mji wa Gaesong nchini Korea ya Kaskazini. Wachambuzi wanaona kuwa kuanza tena kwa mazungumzo hayo ni dalili nzuri kwa kuanzisha tena mazungumzo ya pande sita wakati suala la nyuklia la peninsula ya Korea linapokuwa la utatanishi.

Matokeo ya mazungumzo hayo kati ya serikali mbili yanaathiri moja kwa moja utatuzi wa suala la nyuklia la peninsula ya Korea na hali ya siasa ya penisula la Korea. Mazungumzo ya nchi hizo mbili kuhusu siasa, uchumi na maeneo ulinzi wa kijeshi yalisimama mwezi Julai mwaka jana. Hivi karibuni jumuyia ya kimataita inazidi kuhimiza mazungumzo ya pande sita yaanzishwe tena, wakati huo Korea ya Kaskazini tarehe 14 ilijitokeza kutaka kurudisha mazungumzo na Korea ya Kusini. Watu wanaona kuwa kitendo hicho cha Korea ya Kaskazini ni juhudi za kulegeza hali ya wasiwasi ya penisula la Korea na pia ni kitendo kinachoashiria kuwa Korea ya Kaskazini inajisogeza karibu na mazungumzo ya pande sita.

Mkuu wa ujumbe wa Korea ya Kusini Bw. Rhee Bong-jo alieleza kuwa katika mazungumzo yaliyofanyika tarehe 16 Korea ya Kusini ilieleza zaidi wasiwasi kuhusu hali ya penisula ya Korea na kuihimiza Korea ya Kaskazini irejee kwenye mazungumzo ya pande sita. Korea ya Kusini inasema kuwa kama Korea ya Kaskazini ikirejea kwenye mazungumzo ya pande sita, Korea ya Kusini itatoa "pendekezo muhimu" ambalo litasaidia utatuzi wa suala la nyuklia la Korea ya Kaskazini. Ofisa mmoja wa Korea ya Kusini ambaye hakutaka jina lake litajwe alidokeza kuwa "pendekezo" hilo litazingatia zaidi msimamo wa Korea ya Kaskazini. Ingawa Korea ya Kaskazini haikugusia suala la nyuklia, lakini ilisikiliza kwa makini msimamo wa Korea ya Kusini.

Kuhusu mazungumzo ya serikali mbili, Marekani imeonesha msimamo wake. Tarehe 16 msaidizi wa waziri wa mambo ya nje wa Marekani ambaye pia ni mjumbe wa kwanza wa mazungumzo ya pande sita Bw. Christopher Hill alisema kuwa Marekani inaunga mkono mazungumzo ya serikali mbili za Korea na Kaskazini na Korea ya Kusini, na alitumai kuwa mazungumzo hayo yataleta mazingira mazuri ya kuanzisha tena mazungumzo ya pande sita, na pia alisema kuwa kutokana na ubinadamu, Korea ya Kusini inapaswa kutoa msaada wa mbolea ya chumvichumvi kwa Korea ya Kaskazini.

Bw. Hill amemaliza tu safari yake ya pili katika muda mfupi uliopita kwa ajili ya usuluhishi wa suala la nyuklia la peninsula ya Korea, kuanzisha tena mazungumzo kati ya serikali mbili ni lengo lake muhimu katika safari zake. Vyombo vya habari vya Korea ya Kusini vilisema kwamba baada Korea ya Kaskazini kupendekeza kufanya tena mazungumzo na Korea ya Kusini tarehe 14, Bw. Hill aliyefika punde nchini Korea ya Kusini tarehe 16 alizungumza na waziri wa mawasiliano wa Korea ya Kusini Bw. Ban Ki-moon, baada ya mazungumzo alisema kuwa anatumai mazungumzo ya pande sita yataendelea, na Marekani inafanya juhudi kufanikisha lengo hilo.

Wachambuzi wanaona kuanzisha tena mazungumzo ya pande sita ni vigumu sana. Kwa hivi sasa ambapo msingi wa mazungumzo bado upo mazungumzo ya pande sita kama hayataweza kurudishwa hakika itasababisha hali mbaya ya suala la nyuklia la peninsula ya Kaskazini. Hivi sasa pande tatu kati ya pande sita, nchi za China, Korea ya Kusini na Russia zinaendelea kufanya juhudi ili kuhimiza mazungumzo ya pande sita yafanyike na jumuyia ya kimataifa inatarajia mazungumzo hayo yanaweza kufanyika mapema.

Idhaa ya kiswahili 2005-05-17