Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-05-18 20:25:56    
Mkutano wa nchi za Afrika kuhusu suala la Darfur wafanyika

cri

Mkutano mdogo wa wakuu wa nchi za Afrika kuhusu suala la Darfur nchini Sudan ulifunguliwa jana usiku huko Tripoli, mji mkuu wa Libya. Viongozi wa nchi walioshiriki kwenye mkutano wanatoka Libya, Sudan, Ethiopia, Nigeria, Chad na Eritrea pamoja na maofisa kutoka Umoja wa Afrika na Umoja wa Nchi za Kiarabu.

Mkutano huo was siku mbili, una ajenda tatu. Ya kwanza ni kujadiliana kuhusu kuihimiza serikali ya Sudan irejeshe upya mazungumzo ya amani pamoja na majeshi yanayoipinga serikali yaliyoko kwenye sehemu ya Darfur. Toka nusu ya pili ya mwaka jana, kutokana na kuhimizwa na Umoja wa Afrika, serikali ya Sudan ilifanya maduru matatu ya mazungumzo ya amani na majeshi mawili makubwa yanayoipinga serikali nchini humo, lakini ufanisi ulikuwa mdogo sana, na hivi sasa mazungumzo hayo yamekwama. Kabla ya kufanyika kwa mkutano huo, katibu mkuu wa Umoja wa Afrika Bw. Amr Moussa alitoa taarifa ikisema kuwa kutokana na kukwama kwa mazungumzo ya amani, hali ya wasiwasi mkubwa kwenye sehemu ya Darfur haiwezi kupungua, hivyo jukumu kubwa zaidi la mkutano huo wa wakuu wa nchi ni kuweka utaratibu wa mazungumzo ya amani. Alitoa wito wa kutaka pande zote husika ziwe na moyo wa dhati na kurejea kwenye mazungumzo. Makamu wa kwanza wa rais wa Sudan Bw. Ali Mohammed Taha tarehe 10 mwezi huu alisisitiza kuwa serikali ya Sudan imejiandaa vya kutosha kwa mazungumzo mapya ya amani.

Ya pili, mkutano utajadili namna ya kuikabili hali mpya baada baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kupitisha azimio la No. 1593 mwezi Machi mwaka huu. Kutokana na azimio hilo, maofisa wa serikali na jeshi, wanamgambo wa jeshi linaloiunga mkono serikali na wanamgambo wanaoipinga serikali ambao wanatuhumiwa kwa makosa ya kivita na kupinga ubinadamu watafunguliwa mashtaka kwenye mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai. Kufuatia azimio hilo, serikali ya Sudan ilitangaza "kupinga kabisa" azimio hilo, ikiona kuwa azimio hilo limekiuka mamlaka ya Sudan na litatatanisha zaidi hali ya sehemu ya Darfur. Sudan na baadhi ya nchi za Afrika zinaona kuwa juu ya msingi wa kanuni ya haki za kisheria, idara ya sheria ya Sudan ina haki na inapaswa kuwafungulia mashtaka watu waliofanya makosa kwenye sehemu ya Darfur.

Ya tatu, kujadili namna ya kuboresha hali ya usalama ya sehemu ya Darfur. Kabla ya kufanyika kwa mkutano huo, pande husika zilionesha juhudi za kuharakisha mchakato wa amani. Kwa kusuluhishwa na rais Gadhafi wa Libya, wawakilishi wa serikali ya sehemu ya Darfur na majeshi mawili yanayoipinga serikali tarehe 11 mwezi huu walisaini azimio la Tripoli la kusimamisha mapigano.

Serikali ya Sudan tarehe 14 mwezi huu ilitangaza kuwa kuhusu suala la Darfur itaanzisha kamati tatu za sheria, tathmini ya fidia na ugawaji wa maeneo ya mikoa.

Wachambuzi wanaona kuwa baada ya kuandaa mkutano wa wakuu wa nchi tano kuhusu suala la Darfur mwezi Oktoba mwaka jana, mwaka huu Libya imeandaa tena mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika, jambo ambalo linaonesha nia yake ya kujaribu kutatua suala la Darfur ndani ya Umoja wa Afrika. Lakini suala la Darfur limekuwepo kwa muda mrefu uliopita, hivyo utatuzi wake siyo rahisi. Aidha majeshi mawili yanayoipinga serikali kukataa kushiriki kwenye mkutano huo kutaathiri ufanisi wa mkutano.

Idhaa ya Kiswahili 2005-05-17