Mwenyekiti wa baraza la mashauriano ya kisiasa ya China Bw. Jia Qinglin tarehe 15 alimaliza ziara rasmi ya kirafiki nchini Cuba, na kuelekea Bogotá, kuanza ziara yake nchini Colombia.
Cuba ni nchi iliyoanzisha uhusiano wa kidiplomasia na China mapema zaidi katika nchi za Latin-America. Katika miaka 45 iliyopita tangu kuanzishwa kwa uhusiano kati ya nchi hiyo mbili, uhusiano huo umepata maendeleo makubwa. Katika miaka ya karibuni, urafiki na uhusiano wa kisiasa kati ya nchi hizo mbili umekuwa ukiimarishwa siku hadi siku. Safari hii, Bw. Jia Qinglin kwa nyakati tofauti alifanya mazungumzo na mwenyekiti wa kamati ya mambo ya Cuba Bw. Fidel Castro, naibu mwenyekiti wa kwanza wa kamati ya mambo ya nchi ambaye pia ni naibu mwenyekiti wa kwanza wa mkutano wa mawaziri Bw. Raul Castro Ruz na spika wa bunge la Cuba Bw. Ricardo Alarcon de Quesada. Kutembeleana mara kwa mara kati ya viongozi wa ngazi ya juu wa China na Cuba kumezidisha urafiki wa jadi na ushirikiano wa kunufaishana kati ya nchi hizo mbili.
Huu ni mwaka wa 45 wa uhusiano kati ya China na Cuba, viongozi wa pande mbili wote wameeleza matumaini yao ya kuimarisha urafiki wa jadi na ushirikiano wa kirafiki katika maeneo mbalimbali . Alipofanya mazungumzo na spika Ricardo Alarcon de Quesada, Bw. Jia Qinglin alisema kuwa, nia hasa ya ziara yake nchini Cuba ni kutekeleza maoni muhimu yaliyofikiwa kati ya pande mbili kuhusu kukuza uhusiano wa nchi hizo mbili, kuzidisha ushirikiano wa kunufaishana katika maeneo mbalimbali. Ameainisha kuwa, hata hali ya kimataifa itabadilika namna gani, China siku zote inatumai kuwa, kukuza uhusiano wa kirafiki na ushirikiano kati yake na Cuba kunaambatana na maslahi ya msingi ya wananchi wa nchi hizo mbili, kutasaidia kulinda amani ya dunia, kuhimiza maendeleo ya pamoja na kusukuma mbele maendeleo ya binadamu.
Kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana katika maeneo mbalimbali hasa sekta ya uchumi na biashara ni lengo kuu la ziara ya Jia Qingling. Katika miaka ya karibuni, ushirikiano kati ya China na Cuba katika eneo la uchumi na biashara umepata mafanikio makubwa. Mwaka 2004, thamani ya biashara kati ya China na Cuba ilifikia dola za kimarekani milioni 500, ikiongezeka kwa asilimia 47 kuliko mwaka uliotangulia. Safari hii, viongozi wa nchi hizo mbili wamebadilishana maoni kuhusu jinsi ya kuimarisha ushirikiano huo. Bw. Fidel Castro alisema Cuba itajifunza uzoefu wa China katika kukuza uchumi, na kuzidisha ushirikiano kati yake na China. Alisema kuwa, mafanikio makubwa iliyoyapata China katika kuendeleza uchumi ni ya kufurahisha, na ni mchango mkubwa kwa maendeleo ya uchumi wa dunia. Amesema Cuba inapenda kuzidisha ushirikiano na China katika uchumi na biashara, mawasiliano, bidhaa za kuokoa nishati na zana za matibabu na sekta nyingine, ili kuhimiza uhusiano wa nchi hizo.
Katika ziara yake, Bw. Jia Qinglin pia alibadilishana maoni na viongozi wa Cuba kuhusu mambo yanayozihusu pande mbili.
Aidha, Bw. Jia Qinglin alitembelea chuo kikuu cha Havana, na kukagua mradi wa ushirikiano wa kufundisha Kichina. Japokuwa mradi huo ulianzishwa miezi michache tu iliyopita, lakini umepata mafanikio. Bw. Jia Qinglin pia alikutana na wafanyakazi na wachina wanaoishi nchini Cuba na kuwahimiza watoe mchango mkubwa zaidi katika kuimarisha uhusiano kati ya China na Cuba.
Idhaa ya kiswahili 2005-05-17
|