Katika siku za majira ya Spring mwezi Mei, mpango wa wanafunzi wa wa vyuo vikuu vya China kujitolea kwenda katika sehemu ya magharibi ya China umeanzishwa. Tangu mwezi wa Machi, Kamati Kuu ya umoja wa vijana ulipokea simu nyingi kutoka kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, ambao walikuwa na matumaini makubwa ya kutoa mchango katika sehemu ya magharibi ya China. Wanafunzi hao walisema kuwa, wanataka kufanya kazi katika sehemu ya magharibi ya China.
Katika miaka kadhaa iliyopita, wanafunzi waliojitolea wa vyuo vikuu walikwenda kwenye vijiji na wilaya mbalimbali za sehemu ya magharibi ya China ambazo uchumi wa sehemu hiyo bado uko nyuma nchini China. Wanafunzi hao walifanya kazi mbalimbali zikiwemo mambo ya elimu, afya, kilimo, kuwasaidia wakulima maskini na ujenzi wa vituo vya vijana. Wanafunzi hao ni nguvu kubwa ya kuendeleza uchumi na jamii ya sehemu ya magharibi.
Mafanikio yaliyopatikana katika sehemu ya magharibi ya China yalionesha kuwa, sehemu ya magharibi ya China ilitoa nafasi kubwa kwa wanafunzi kuongeza uwezo na kuanza kazi zao.
Mwaka 2005, wanafunzi waliojitolea wa vyuo vikuu elfu 11.3 walikwenda kwenye vijiji 300 vya sehemu ya magharibi ya China ili kufanya kazi za misaada katika mambo ya elimu, afya, kilimo, ujenzi na uendeshaji wa vituo vya vijana.
Mpango wa kutoa huduma katika sehemu ya magharibi ya China una maana kubwa, unahitaji vijana wengi wenye uwezo na nia kubwa ya kujenga taifa. Wanafunzi waliojitolea wa vyuo vikuu vya China wana juhudi kubwa ya kujenga taifa, hivyo wanataka kufanya kazi katika sehemu ya magharibi ya China, ili kuwasaidia watu wanaoishi katika sehemu hiyo.
Mwanzoni mwa miaka 20 ya karne hii, wachina wanapaswa kutumia fursa kubwa ya kimkakati. Maisha ya vijana wa China yanapaswa kulingana na mustakabali wa taifa. Vijana wa China wanapaswa kujitahidi kusoma, kutoa mchango kwa taifa na kufanya kazi katika sehemu zinazohitaji misaada nchini China.
Idhaa ya kiswahili 2005-05-18
|