Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-05-18 19:13:29    
Kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana kati ya China na Latin Amerika na kusukuma mbele maendeleo kwa pamoja

cri

Mwenyekiti wa Baraza la mashauriano ya kisiasa la China Bwana Jia Qinglin ambaye yuko ziarani nchini Colombia tarehe 17 alasiri alitoa hotuba kwenye Baraza la juu la bunge la Colombia akisema kuwa, kuimarisha ushirikiano kati ya China na Latin Amerika si kama tu kunasaidia kuinua hadhi ya kila upande duniani, bali pia kunasaidia zaidi amani, utulivu na maendeleo ya dunia.

Katika hotuba yake Bwana Jia Qinglin alisifu sana uhusiano uliopo kati ya China na Latin Amerika. Anaona kuwa, baada ya kuingia karne ya 21, viongozi wakuu wa China na nchi za Latin Amerika wanatembeleana mara kwa mara, uaminifu wa kisiasa unaongezeka siku hadi siku, hasa mwelekeo wa ongezeko la ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara unawafurahisha watu, na uhusiano kati ya China na Latin Amerika umeingia katika kipindi kipya cha maendeleo.

Bwana Jia anaona kuwa, hivi sasa uhusiano kati ya China na Latin Amerika uko katika kipindi kizuri kabisa cha kihistoria, ambao unakabiliwa na fursa ya kihistoria ya kuendelea zaidi. Ingawa hivi sasa kuna ushindani ni mkali duniani, lakini ushirikiano kati ya China na Latin Amerika una mustakbali mzuri. Alisema:

China na nchi za Latin Amerika zote ni nchi zinazoendelea ambazo zinakabiliwa na shinikizo la ushindani. Kwa nchi zinazoendelea, jambo muhimu zaidi ni kutafuta njia inayosaidia kupanua ushirikiano wa kunufaishana, ili kutumia fursa na kupata maendeleo kwa pamoja.

Wakati huo huo Bwana Jia Qinglin alisema:

China inapenda kufuata kanuni za kuwa na usawa na kunufaishana na kupata maendeleo kwa pamoja, ili kuendeleza siku hadi siku uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na nchi za Latin Amerika pamoja na Colombia. Amesema serikali ya China inafanya juhudi kusukuma mbele ushirikiano kati ya pande hizo mbili katika sekta mbalimbali, na kuyaunga mkono mashirika ya China yenye nguvu na sifa nzuri kwenda Colombia na nchi nyingine za Latin Amerika kuanzisha viwanda na kuwekeza vitega uchumi, pia inayataka mashirika ya Latin Amerika kuja China kuanzisha shughuli zao.

Bwana Jia anatumai kuwa China na Latin Amerika zitapeana mikono, kutumia fursa, kupanua ushirikiano na kuimarisha maingiliano ili China na Latina Amerika ziwe marafiki wa kutegemeana siku zote, na kuwa wenzi wa ushirikiano wa kunufaishana kiuchumi na kufanya maingiliano katika sekta ya utamaduni wa aina tofauti, ili kuhimiza kwa pamoja shughuli za amani na maendeleo ya dunia.

Bwana Jia Qinglin pia alifahamisha hali kuhusu maendeleo ya uchumi na jamii ya China na hali kuhusu "Sheria ya kupinga kufarakanisha taifa" iliyopitishwa hivi karibuni kwenye bunge la umma la China.

Katika hotuba yake, Bwana Jia Qinglin pia alieleza matumaini yake ya kuongeza mawasiliano na ushirikiano kati ya China na Colombia. Alisema:

Ziara yangu inalenga kuongeza mawasiliano, kuongeza maelewano, kuzidisha urafiki, kuhimiza ushirikiano na kutekeleza maoni ya pamoja waliyopata rais Hu Jintao na rais Alvaro Uribe kuhusu kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana kati ya China na Colombia.

Idhaa ya Kiswahili 2005-05-18