Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-05-18 20:57:07    
Kuchemsha minofu ya nyama ya ng'ombe pamoja na papai

cri

Mahitaji

Papai moja, minofu ya nyama ya ng'ombe gramu 200, yai moja lililokorogwa, kiasi kidogo cha vipande vya vitunguu saumu, pilipili, mchuzi wa chaza, chumvi, unga wa mahindi na mvinyo wa mchele, maji bakuli mbili.

Njia

1. Weka minofu ya nyama ya ng'ombe ndani ya bakuli moja halafu tia chumvi, unga wa mahindi na yai lililokorogwa, korogakoroga mpaka zichanganyike sawasawa, halafu ukate minofu ya nyama ya ng'ombe iwe vipande.

2. Kata papai liwe vipande, pasha moto vitie ndani ya sufuria yenye mafuta, korogakoroga kisha vipakue.

3. Pasha moto tena, tia vipande vya vitunguu saumu na pilipili, korogakoroga halafu tia vipande vya minofu ya nyama ya ng'ombe korogakoroga, mimina mchuzi wa chaza, maji na mvinyo wa mchele.

4. Baada ya kuchemsha, mimina maji ya wanga, tia vipande vya papai. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.