Hali ya hatari ilionekana tena tarehe 18 katika sehemu ya Gaza. Siku hiyo, watu wenye silaha wa Palestina walirusha mabomu kadhaa kwenye makazi ya Wayahudi yaliyoko katika sehemu ya Gaza na jeshi la Israel liliwajibu watu hao wa Palestina kwa makombora kwa mara ya kwanza tangu mwezi Februari mwaka huu, vita viliposimamishwa kati ya pande hizo mbili. Waziri mkuu wa Israel Bw. Ariel Sharon alitishia na kusema kuwa kama mamlaka ya Palestina haitachukua hatua mara moja kuwazuia watu wenye silaha wa Palestina wasishambulie makazi wa Wayahudi, basi Israel itarejesha vitendo vya kijeshi katika sehemu ya Gaza. Kusimamishwa kwa vita kati ya Palestina na Israel kulikodumu kwa zaidi ya miezi mitatu kumekutana na hatari.
Migogoro mfululizo iliyotokea siku hiyo imesababisha tena hali hatari kati ya Palestina na Israel. Kundi la Hamas siku hiyo liliishutumu Israel kukiuka mkataba wa kusimamisha vita na kutishia kuendelea kuzishambulia kwa mabomu shabaha za Israel. Waziri mkuu wa Israel Ariel Sharon na waziri wa ulinzi Shaul Mofaz walishauriana kwa dharura na kuamua kutoa onyo kali kwa mamlaka ya Palestina na kuitaka Palestina ichukue hatua mara moja na kuzuia mashambulizi ya watu wenye silaha wa Palestina, ama sivyo Israel itarejesha vitendo vya mashambulizi katika sehemu ya Gaza. Habari zinasema kuwa Bw. Sharon na makamanda waandamizi wa Israel wanatazamiwa kuitisha mkutano tarehe 19 na kuendelea kushauriana kuhusu hali ya Gaza.
Tangu mwezi Februari mwaka huu, pande mbili Palestina na Israel zilipotangaza kusimamisha vita kati yao, kusimamishwa vita kumekutana na hatari kwa mara kadhaa. Tarehe 9 mwezi Februari, yaani siku ya pili baada ya kufikiwa makubaliano ya kusimamisha vita, jeshi la Israel lilimwua kijana wa Palestina na watu wenye silaha wa Palestina wakayapigia mabomu mara moja makazi ya Wayahudi yaliyoko katika sehemu ya Gaza kwa kulipiza kisasi. Tarehe 25 mwezi huo, Tel-Aviv ilikumbwa na mabomu ya kujiua na kuondoa hali tulivu iliyodumu kwa muda mfupi. Tarehe 9 mwezi Aprili, askari wa Israel waliwaua vijana watatu wa Palestina kusini mwa sehemu ya Gaza na kusababisha ghadhabu kubwa za Wapalestina na wanamgambo wa Palestina walipiga mabomu kwenye makazi ya Wayahudi ili kulipiza kisasi.
Jambo linaostahili kufuatiliwa ni kuwa baada ya kutokea kwa kila mgogoro, ingawa pande mbili Palestina na Israel zote zilitishia upande mwingine, lakini zote zilidhibiti kiasi cha kulipiza kisasi ili zisije zikabeba lawama ya kuharibu usimamishaji wa vita. Tarehe 18, hali hatari ilionekana tena katika sehemu ya Gaza, lakini pande zote mbili hazikutaka kufanya mgogoro huo uwe mbaya zaidi. Jeshi la Israel linaona kuwa Hamas kushambulia makazi ya Wayahudi, hakulengi shabaha za Israel, kuna lengo la kuiuchukiza mamlaka ya Palestina na kupinga hukumu iliyofanywa na mahakama ya Palestina kuhusu kufuta matokeo ya uchaguzi wa sehemu ya Rafah. Katika uchaguzi huo uliofanyika mapema ya mwezi huu, Hamas lilipata ushindi mkubwa katika sehemu ya Rafah, lakini mahakama ya Palestina tarehe 17 ilifuta matokeo ya uchaguzi huo kutokana na upigaji kura usio wa haki na kutaka upigaji kura ufanywe tena.
Jeshi la Israel lilieleza kuwa ingawa jeshi hilo litakuwa macho zaidi kwa kupandishwa ngazi kwa hali hatari, lakini linatumai kuwa mamlaka ya Palestina itachukua hatua ya kwanza, na kudhibiti kitendo cha wanajeshi wa Palestina. Kwa hiyo mashambulizi ya makombora yaliyofanywa na jeshi la Israel tarehe 18 dhidi ya watu wenye silaha wa Palestina ni kutoa onyo tu kwa watu hao.
Idhaa ya kiswahili 2005-05-19
|