Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-05-19 16:42:00    
Maeneo kumi ya kiuchumi nchini China

cri

1. Eneo la kiuchumi la Kaskazini Mashariki mwa China: Eneo hilo ni pamoja na mikoa ya Heilongjiang, Jilin, Liaoning na sehemu ya mashariki ya mkoa wa Mongolia ya Ndani. Katika sehemu hiyo kuna maliasili nyingi na ardhi kubwa yenye rutuba.

2. Eneo la kiuchumi lililoko kando ya Bahari ya Bo kaskazini mwa China: Eneo hilo ni pamoja na miji ya Beijing na Tianjin, mikoa ya Hebei na Shandong. Sehemu hiyo ni kituo cha China, na huko kuna mafundi wengi na mashine za kisasa. Viwanda vyenye kiwango cha juu cha teknolojia vimeendelezwa huko..

3. Delta ya kiuchumi ya Mto Changjiang: Eneo hilo ni pamoja na mji wa Shanghai, mikoa ya Jiangsu na Zhejiang. Katika sehemu hiyo kuna watu wengi wenye kiwango cha juu cha elimu, na viwanda vya usindikaji vimepata maendeleo makubwa. Eneo hilo litakuwa kituo kikubwa cha kiuchumi, ufunguaji mlango, elimu na habari za kiuchumi na kibiashara.

4. Eneo la kiuchumi la pwani lililoko kusini mwa China. Eneo hilo ni pamoja na mikoa ya Guangdong, Guangxi, Fujian na Hainan. Eneo hilo ni sehemu ya kwanza inayofungua mlango kwa nchi za nje. Ufunguaji mlango wa miaka 10 umeliwekea eneo hilo msingi thabiti.

5. Eneo la kiuchumi la sehemu ya katikati ya Mto Manjano: Eneo hilo ni pamoja na mikoa ya Shanxi, Shaanxi, Henan, na sehemu za kati na magharibi za mkoa wa Mongolia ya Ndani. Sehemu hiyo ina maliasili nyingi ya makaa ya mawe, ambayo inachukua asilimia 80 ya maliasili yote ya makaa ya mawe nchini China.

6. Eneo la kiuchumi la sehemu ya juu ya Mto Manjano: Eneo hilo ni pamoja na mikoa ya Gansu, Ningxia na Qinghai. Katika eneo hilo kuna tofauti kubwa ya kiwango cha maji mitoni. Hivyo maliasili ya maji ni nyingi, na vituo vya kuzalisha umeme kwa nguvu ya maji vitaendelea kujengwa huko.

7. Eneo la kiuchumi la sehemu ya katikati ya Mto Changjiang: Eneo hilo ni pamoja na mikoa ya Hunan, Hubei, Jiangxi na Anhui. kituo cha viwanda vinavyotegemea uchukuzi kwenye mito na matumizi ya maji na kituo cha kilimo vitajengwa huko.

8. Eneo la kiuchumi la sehemu ya juu ya Mto Changjiang. Eneo hilo ni pamoja na mikoa ya Sichuan, Guizhou na Yunnan. Kituo cha viwanda vinavyotumia nishati nyingi na viwanda vya kemikali kitajengwa huko.

9. Eneo la kiuchumi la mkoa wa Xinjiang: Eneo hilo linachukua moja kwa sita ya eneo lote la China, na lina maliasili nyingi za mafuta na madini. Kituo cha viwanda vya mafuta na kemikali ya mafuta na kituo cha ufugaji na usindikaji husika kitajengwa huko.

10. Eneo maalum la kiuchumi la Mkoa wa Tibet: Kutokana na hali ya hewa na sehemu ya kijiografia, maendeleo ya uchumi wa eneo hilo ni madogo. Hivyo eneo hilo linahitaji uugaji mkono wa nchi nzima na sera ya taifa, ili kuharakisha maendeleo na ujenzi huko na kuanzisha mfumo wa kisasa wa kiuchumi.

Idhaa ya Kiswahili 2005-05-19