Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-05-23 14:09:35    
Historia ya Ukimwi (2)

cri

Novemba mwaka 1983, kwa mara ya kwanza WHO ilifanya mkutano kuhusu UKIMWI mjini Geneva, na kutathmini hali ya ugonjwa huo duniani. Hii inamaanisha kuwa uchunguzi kuhsu UKIMWI ulikuwa umeanza kote duniani. Ripoti iliyotolewa baada ya mkutano huo ilieleza kuwa UKIMWI umetokea nchini Marekani, Canada, nchi 15 za Ulaya, Haiti, Australia, Zaire na baadhi ya nchi za Latin Amerika, na nchini Japan pia kulikuwa na watu wachache.

Kwa kweli kabla na baada ya mkutano huo, uchunguzi ulidhihirisha kuwa ugonjwa huu ulikuwa umekwisha enea barani Afrika kwa muda mrefu, ila tu wenyeji waliuita ugonjwa huo kuwa ni "ugonjwa kukonda", wanasayansi waligundua ugonjwa huo katika nchi za Rwanda na Zaire na sehemu ya kati ya Afrika.

Taasisi moja ya uchunguzi wa magonjwa ambayo ni maarufu nchini Ufaransa ilipata virusi vya ugonjwa huo na kuvipeleka kwenye kituo cha udhibiti wa maambukizi ya magonjwa nchini Marekani. Baada ya miezi kadhaa taasisi hiyo iliipatia virusi hivyo kwa jina la LAV kwa ufupisho, na iliomba hataza ya ugunduzi. Kisha baadaye ilipeleka virusi hivyo kwenye taasisi ya uchunguzi wa saratani ya Marekani. Maingiliano hayo yangestahili kusifiwa kutokana na maingiliano mazuri kwa ajili ya kupambana kwa pamoja dhidi ya ugonjwa huo, lakini haikutegemewa kuwa maingiliano hayo yalikuwa chanzo cha mgogoro wa hataza ya ugunduzi wa virusi kati ya wanasayansi wa Ufaransa na Marekani.

Tarehe 22 Aprili, mwaka 1984 mwanasayansi mmoja wa kituo cha udhibiti maabukizi ya magonjwa nchini Marekani alitangaza matokeo ya uchuhguzi wa taasisi ya Ufaransa akisema "tumepata virusi vya UKIMWI".

Lakini siku ya pili taasisi ya uchunguzi wa saratani ya Marekani ilitangaza kuwa imepata virusi vya UKIMWI na kuvipatia jina la HTLV-III kwa ufupisho na pia ilipata hataza ya ugunduzi.

Watu walipofurahia mafanikio ya ugunduzi huo wa virusi walijiuliza, je, eti vitusi vya LAV na HTLV-III ni virusi vya aina moja?

Mwishoni mwa mwaka 1984, watu wenye virusi vya UKIMWI walifikia 3064, na kati yao watu 1292 walikufa. Ongezeko la wagonjwa na wengi waliokufa lilisababisha mtafaruku katika jamii. Askari polisi waliposhughulika na wasaidikiwa UKIMWI walivaa barakoa na mipira ya mikono, wenye nyumba za kupangisha waliwafukuza wapangaji wagonjwa wa UKIMWI na maofisa wa huduma za jamii wa Marekani waliwasiliana na wagonjwa kwa simu bala ya ana kwa ana. Mahangaiko hayo yalienea haraka, watu wanaona ugonjwa huo lazima uchukuliwe hatua lakini hawakujua nini la kufanya.

Mwanzoni mwa mwaka 1985, baada ya kufanya uchunguzi wanasayansi walithibitisha kuwa virusi vya LAV na HTLV-III ni virusi vya aina moja, ila tu majina tofauti.

Mwezi Machi mwaka huo, aina moja ya dawa ya maji inayothibitisha virusi hivyo iligunduliwa nchini Marekani. Kwa kutumia dawa hiyo kwenye tone la damu inaweza kugundua kama mtu huyo ana virusi vya LAV au HTLV-III mwilini.

Tokea Ukimwi ugunduliwe, wanasayansi hawaachi juhudi za kutafuta dawa za kutibu au kudhibiti ugonjwa huo. Katika mchujo wa dawa za aina nyingi, moja iitwayo AZT iliwavutia sana. Dawa ya AZT sio dawa mpya bali ilikuwa ni dawa iliyotengenezwa mwaka 1964 kwa ajili ya tiba ya saratani, lakini majaribio yalithibitisha kuwa dawa hiyo haisaidii kitu kwa tiba ya saratani, lakini katika majaribio ya maabara, wachunguzi waligundua kuwa dawa hiyo ina uwezo wa kudhibiti virusi visienee haraka mwilini mwa mtu. Kisha madaktari walijaribisha dawa hiyo kwa wagonjwa kwa muda wa miezi sita, wakagundua kuwa kundi la kwanza lililotumia dawa hiyo mmoja tu alikufa, na kundi lisilotumia dawa hiyo watu 19 walikufa. Hii inamaanisha kuwa dawa ya AZT inaweza kurefusha wagonjwa muda wa uhai.

Hadi mwishoni mwa 1986, nchi 85 zilikuwa zimegundua UKIMWI na wagonjwa walifikia 38,401, miongoni hao wagonjwa 2,323 wako barani Afrika, 31,747 Latin Amerika, 84 Asia na 3858 Ulaya na 395 walikuwa wako Oceania.

Kuenea kwa haraka kwa "muuaji kimya" wa UKIMWI kuliwahadharisha watu wengi kuwa, binadamu hawapaswi kuukalia kimya UKIMWI! Shirika moja la lisilo la serikali la Marekani lilifanya maandamano makubwa, waandamanaji waliinanua mabango yakisema, "Kimya ni Kifo!"

Idhaa ya kiswahili 2005-05-23