Mwenyekiti wa Baraza la mashauriano ya kisiasa la China Bwana Jia Qinglin tarehe 20 alimaliza ziara yake rasmi ya kirafiki katika nchi 4 za Latin Amerika. Katibu mkuu wa bara hilo Bwana Zheng Wantong aliyeambatana na Bwana Jia katika ziara yake alisifu sana ziara hiyo ya Bwana Jia na kusema kuwa ziara hiyo imetia nguvu mpya kwa maendeleo ya urafiki na ushirikiano kati ya China na Latin Amerika katika sekta zote.
Kuanzia tarehe 9 had 20 Mei, Bwana Jia Qinglin alifanya ziara rasmi ya kirafiki katika nchi 4 za Mexico, Cuba, Colombia na Uruguay. Katika ziara yake hiyo, Bwana Jia Qinglin alikutana na kuwa na mazungumzo na viongozi wa serikali, mabunge na mitaa wa nchi hizo 4, ambapo walibadilishana maoni kuhusu uhusiano wa pande mbili mbili na masuala yanayozihusi, na wamepata maoni mengi ya pamoja. Bwana Jia Qinglin na msafara wake pia walifanya mawasiliano na watu wa sekta za viwanda, biashara na utamaduni, mawasiliano hayo yameongeza maelewano, kuzidisha urafiki na kuhimiza ushirikiano. Bwana Zheng Wantong alisema kuwa, mafanikio makubwa ya ziara hiyo ni kuwa uaminifu wa kisiasa umeongezwa sana kati ya nchi hizo 4, na kusukuma mbele maendeleo ya uhusiano wa pande mbili mbili katika sekta mbalimbali. Viongozi wa nchi hizo 4 wote wameahidi kufanya juhudi kusukuma mbele maendeleo ya uhusiano na China ulio wa muda mrefu, utulivu na wa kudumu, na kufanya juhudi za pamoja na China katika kujenga uhusiano wa China na Latin Amerika.
Katika miaka ya hivi karibuni, maendeleo ya uhusiano wa kiuchumi na kibiashara wa China na Latin Amerika yamewavutia watu. Mwaka 2004 thamani ya jumla ya biashara kati ya China na Latin Amerika iliongeza kwa zaidi ya mara 3 kuliko mwaka 2000, na ongezeko hili lilifikia asilimia 50 kwa miaka miwili mfululizo. Bwana Jia Qinglin alisema mara kwa mara katika ziara yake hiyo ya nchi 4 kuwa, China na Latin Amerika zinaweza kusaidiana katika sekta za uchumi na biashara, na zina nguvu kubwa za kufanya ushirikiano. Na maendeleo ya kila upande kati ya China na Latin Amerika yanaweza kuleta fursa ya maendeleo kwa upande mwingine, China inapenda kuimarisha mawasiliano na ushirikiano na nchi za Latin Amerika na kutimiza lengo la kupata maendeleo kwa pamoja. Mapendekezo ya Bwana Jiang Qinglin yaliitikiwa na nchi hizo 4 za Latin Amerika. Viongozi wa nchi hizo 4 wana matarajio makubwa juu ya maendeleo zaidi kati ya China na Latin Amerika katika sekta za uchumi na biashara, na wameahidi kuchuua hatua halisi za kuimarisha ushirikiano na China katika sekta mpya mbalimbali, na kuanzisha ushirikiano wa muda mrefu wa kunufaishana ili kupata maendeleo kwa pamoja.
Katika ziara yake hiyo, Bwana Jia Qinglin pia alizifahamishia nchi mbalimbali hali ya maendeleo ya uchumi na jamii ya China, na alisisitiza kuwa China itashikilia daima njia ya kujiendeleza kiamani, daima haitajidai umwamba. Wakati huo huo Bwana Jia Qinglin alifanya mawasiliano na ushirikiano na viongozi wa mabunge ya nchi hizo 4, ambapo walibadilishana maoni kuhusu kuongeza urafiki kati ya wananchi, na kusukuma mbele maendeleo ya uhusiano kati ya pande mbilimbili, na wamepata maoni mengi ya pamoja, na kuongeza zaidi mawasiliano na ushirikiano kati ya bunge la umma la China na mabunge ya nchi hizo 4, pia kupanua njia za mawasiliano kati ya China na nchi za Latin Amerika.
Kuimarisha uhusiano na nchi zinazoendelea zikiwemo nchi za Latin Amerika ni msingi wa mambo ya kidiplomasia ya China.
Idhaa ya kiswahili 2005-05-23
|