Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-05-23 19:58:03    
Vyombo vya habari vya nchi za magharibi na sura ya Afrika

cri
    Rais Olusegun Obasanjo wa Nigeria aliwahi kuwaambia waandishi wa habari, "Watu wema watasema kuna maji nusu kwenye kikombe, lakini watu wenye nia mbaya watasema nusu ya kikombe haina maji!"

    Kongamano la 54 la waandishi wa habari la kimataifa linafanyika huko hivi sasa, ambapo mtazamo wa habari wa nchi za magharibi unakosolewa. Rais Kagame wa Rwanda alisema habari zinazotolewa na nchi za magharibi kuhusu Afrika huwa ni za kupotosha na zisizokamilika, katika habari walizotoa Afrika ni sehemu yenye maradhi, migogoro na usimamizi wa kiholela, habari hizo zinafanya watu kuwa na picha mbaya kuhusu Afrika. Ni kweli kuwa hivi sasa watu wakizungumzia Afrika, wengi wanazoea kukumbuka unyonge na mambo yasiyopendeza ya Afrika.

    Rais Kagame alisema kuwa habari mbaya zilizotolewa na vyombo vya habari vya nchi za magharibi kuhusu Afrika zimeathiri uwekezaji wa nchi za nje katika Afrika, hii ni moja ya chanzo kinachofanya Afrika kuwa nyuma kimaendeleo. Idadi ya watu wa Afrika ni kiasi cha 12% ya jumla ya idadi ya watu duniani, lakini uwekezaji wa nchi za nje katika Afrika unachukua 2% tu ya jumla ya uwekezaji duniani, ingawa taarifa iliyotolewa na Umoja wa Mataifa hivi karibuni inasema kuwa faida ya uwekezaji barani Afrika ni kubwa zaidi kuliko sehemu nyingine ambayo inafikia 25.3%. Alisema kuwa hali ya namna hiyo kwa kiwango fulani imesababishwa na "suala la sifa".

    Mwaka jana, kulikuwa na habari nyingi za kusisimua na kufurahisha kuhusu Afrika, hali ya wasiwasi na migogoro vimepungua, uchumi umeendelea vizuri na kuwa na ongezeko na umuhimu wa Umoja wa Afrika umeimarika zaidi. Taarifa ya mwaka iliyotolewa na Benki ya Dunia tarehe 19 mwezi May inasema kuwa baada ya kutulia kwa muda mrefu, hivi sasa uchumi wa Afrika unaanza kubadilika kuwa mzuri hususan katika mwaka jana, ambapo wastani wa ongezeko la pato la taifa ulifikia 5.1% kutoka 4.1% katika mwaka uliotangulia, hilo ni ongezeko kubwa kabisa toka mwaka 1996. Jambo linalosikitisha ni kuwa, vyombo vingi vya habari vya nchi za magharibi havipendi kuona maendeleo hayo. Habari nyingi kuhusu maendeleo ya uchumi wa Afrika zinafunikwa na habari nyingi kuhusu mabadiliko ya hadhi za viongozi.

    Katika kongamano la kimataifa la waandishi wa habari, rais Kibaki alitoa wito wa kutaka vyombo vya habari vitoe habari nyingi zaidi kuhusu maendeleo ya uchumi wa Afrika na jitihada ya kumaliza migogoro kwa ushirikiano wa kikanda.

Idhaa ya Kiswahili