Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-05-24 15:39:27    
Juhudi za kuhifadhi mazingira zianzie kwa watoto

cri

Maonesho ya kimataifa hivi karibuni yanafanyika katika wilaya ya Aichi nchini Japani. Hii ni fursa nzuri kwa wilaya hiyo kuonesha sifa zke za juhudi za kuhifadhi mazingira. Baada ya kuangalia maonesho tumepata mawazo kuwa, juhudi za kuhifadhi mazingira zinapaswa kuanzia kwa watoto.

Mada ya maonesho hayo ni "Pole na kazi dunia yetu". Kutoka michezo ya sanaa, maonesho ya vielelezo vya kuzalisha umeme kwa upepo na kwa nishati ya jua, watazamaji wamejawa na matumainio kuhusu mustakbali wa binadamu. Kwenye maonesho hayo pia yameoneshwa matatizo ya mabadiliko ya hali ya hewa duniani. Namna ya kuwahadharisha watu wawe na mwamko wa kuzingatia hifadhi ya mazingira inawavutia sana, hasa kwa wanafunzi wa shule, ambayo ni kama madarasa ya kuwaelimisha kuhifadhi mazingira.

Jumba jingine la maonesho wilayani humo lilionyesha jinsi watoto wanavyothamani mazingira. "Filamu ya Misitu" inaonesha vilivyo wanyamapori wanavyoishi, kwenye ukuta zinaoneshwa sampuli za wanyama wa aina mbalimbali zilizotengenezwa na watoto kiasi elfu 10 kutoka shule 500 kwa kutumia vitu vilivyotupwa, walitumia vipande vya nyuzi za kushonea, plastiki, makopo, vipande vya mbao, mabua ya mazao na mianzi, walitengeneza sampuli za kereng'ende, panzi, bunzi na tandu. Kutengeneza sampuli za wadudu kunahitaji kuchunguza vilivyo wadudu walivyo, kitendo ambacho kinawalea tabia yao ya kupenda maumbile. Kutengeneza sampuli za wadudu kunaweza kuwasaidia watoto wafahamu umuhimu wa kuhifadhi maliasili, watoto wanapoona sampuli zilizotengenezwa na watoto wenzao wanafurahi na kupenda zaidi viumbe.

Katika jumba hilo pia kuna maua yaliyofinyangwa na watoto kwa udongo, na baadhi ya watoto walifuma nguo kwa nyuzi za rangi tofauti na walitengneza alama njema za maonesho hayo "babu wa misitu" na "mwana wa misitu". Watoto wanaonesha furaha yao ya kuhifadhi mazingira kwa njia yao.

Wataalamu wanaona kuwa katika karne ya 20, binadamu walizalisha mali kwa kutumia maliasili nyingi sana, kufanya hivyo kumeharibu vibaya mazingira, na hivi sasa kwa kiasi fulani uharibifu huo umefikia kiwango cha mwisho. Kama tukitaka kutimiza maendeleo endelevu, kila mmoja lazima ahifadhi mazingira kwa kitendo, na juhudi za kuhifadhi mazingira zinapaswa kuanzia kwake binafsi. Watoto wa leo ni dunia ya kesho ambao watabeba majukumu makubwa ya kuendeleza uchumi endelevu katika karne ya 21, kwa hiyo ni muhimu sana kufanya juhudi za kuhifadhi mazingira kuanzia kwa watoto.

Imefahamika kuwa idara husika za wilaya ya Aichi zimeamua kuwa wanafunzi wote wilayani watakwenda kuangalia maonesho hayo katika siku za likizo. Uamuzi huo ni muhimu sana .

Idhaa ya kiswahili 2005-05-24