Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-05-24 15:45:36    
CMOS chips za China zasafirishwa nchi za nje

cri
Kwenye mkutano wa taifa wa utoaji tuzo za sayansi na teknolojia mwaka 2004, kijana mmoja aliyesifiwa na serikali alifuatiliwa sana na watu. Kijana huyo mwenye umri wa miaka 36 pamoja na kundi analoongoza walifanikiwa kuvumbua CMOS chips za multimedia za teknolojia ya tarakimu, na kuvunjilia mbali ukiritimba wa makampuni ya kimataifa katika eneo la utafiti na uzalishaji wa CMOS chips. Kijana huyo ndiye mkurugenzi mkuu wa kampuni ya elektroniki ya Zhongxing Bw. Deng Zhonghan.

Bw. Deng Zhonghan mwenye sura kama ya mtoto, na anaonekana kama ni msomi. Miaka 13 iliyopita Bw. Deng Zhonghan alikwenda kusoma nchini Marekani, kutokana na mafanikio aliyoyapata katika masomo, baada ya kuhitimu masomo yake katika chuo kikuu alipata ajira katika kampuni moja maarufu ya teknolojia ya mawasliano (IT) nchini Marekani.

Kabla ya miaka 6 iliyopita Bw. Deng Zhonghan alionana wenzake aliosoma pamoja nao nchini Marekani na kuamua kurejea China na kuanzisha shughuli zao. Wakati huo, serikali ya China ilitoa sera kadhaa za nafuu za kuvutia wanafunzi wanaosoma katika nchi za nje. Hivyo, Bw. Deng Zhonghan na wenzake waliacha mazingira bora ya kazi na pato kubwa nchini Marekani, wakarejea nchini na kuanzisha kampuni yao katika eneo la ustawishaji la Zhongguancun. Bw. Deng Zhonghan alisema,

"Mwaka 1999, kampuni yetu ilipoanzishwa kwenye eneo la Zhongguancun ilipata uungaji mkono kutoka kwa idara husika ya Beijing, na shughuli zote za uandikishaji zilimalizika ndani ya wiki moja."

Kutokana na uungaji mkono wa idara husika ya serikali ya Beijing Bw. Deng Zhonghan na wenzake walianzisha kampuni ya elektroniki ya Zhongxing. Kutokana na elimu aliyopata Bw. Deng Zhonghan wakati alipoishi Marekani, anaona kuwa kampuni yao haitakuwa na nafasi ya kushinda katika ushindani wa kimasoko bila kuwa na teknolojia muhimu. Hivyo mara tu baada ya kampuni yao kuanzishwa, waliweka lengo la maendeleo la kuzalisha CMOS chips za multimedia. Bw. Deng Zhonghan alimwambia mwandishi watu wa habari kuwa teknolojia ya CMOS chips za multimedia ya tarakimu ni teknolojia mpya muhimu 3C ambazo ni pamoja na Computer, Communication, na Consumer Electrics. Ikilinganishwa na teknolojia nyingine za CMOS chips ambazo zimehodhiwa na kampuni za nchi za nje, ushindani wa teknolojia ya CMOS chips za multimedia za tarakimu sasa hivi unaanza kukua duniani, hivyo CMOS chips za multimedia za tarakimu zinaweza kuchukuliwa ni bidhaa za CMOS chips za China zinazosafirishwa katika soko la kimataifa.

Ili kufanya utafiti wa CMOS chips wa China uendane na wa kimataifa, kampuni ya Zhongxing ilianzisha matawi yake huko Silicon Valley ya Marekani na Hong Kong na kuanzisha maabara ya Qinghua Zhongxin kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Qinghua. Kutokana na kuwa na idadi kubwa ya wataalamu na uwezo mkubwa wa uvumbuzi, katika muda wa mwaka mmoja tu baada ya kuanzishwa kwa kampuni ya elektroniki ya Zhongxing, walifanikiwa kuzalisha CMOS chips za "Xingguang" yenye maana ya mwangaza wa nyota zenye hataza za China. Bw. Deng Zhonghao alisema,

"Mwezi Machi mwaka 2001, tulifaulu kuvumbua CMOS chips za "Xingguang" yenye hataza za China, ambazo ni CMOS chips zenye circuit milioni moja, si kama tu tulivumbua teknolojia hiyo muhimu katika muda wa miezi 10, bali pia tulifanikiwa kuzizalisha kwa wingi."

Bw. Deng Zhonghan alisema kuwa CMOS chips zinahumika katika video kamera za kompyuta, simu za mikononi na televisheni zenye picha za kiwango cha juu, lakini namna ya kuvutia wanaviwanda wa nchini na wa nchi za nje kutumia CMOS chips za China lilikuwa si jambo rahisi. Baada ya kufanya uchambuzi kuhusu hali ya masoko, kampuni ya Zhongxing ililenga shabaha za kampuni za wastani na ndogo. Wazo lao lilifanikiwa kabisa, pamoja na kuongezeka kwa kampuni zinazotumia CMOS chips za Zhongxing, China, jina la kampuni hiyo ikajulikana hatua kwa hatua.

Dr. Zhang Hui alisoma pamoja na Bw. Deng Zhonghao katika chuo kikuu cha Berkeley kwenye jimbo la California, Marekani. Mwaka ule alirejea nchini na kuanzisha kampuni ya Zhongxing pamoja na Bw. Deng Zhonghan, na hivi sasa yeye ni naibu mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Zhongxing. Alipoeleza shida walizokabiliwa nazo wakati wa kuwafahamisha wateja bidhaa zao, alisema,

"Tulikabiliwa changamoto kubwa katika kuvutia wateja. Mwanzoni soko la dunia halikuwa na imani na China kama ingeweza kuwa na uwezo wa kuzalisha CMOS chips za multimedia, hivyo tulifanya kazi ya kuwafanya watuamini hatua kwa hatua kwa kuonesha teknolojia na nguvu zetu za ushindani na kuonesha bidhaa zetu bora na za bei nafuu."

Baada ya kufanikiwa kuzalisha CMOS chips za aina ya kwanza, kampuni ya Zongxing ilifanikiwa kuzalisha CMOS chips za kizazi cha tano, ambazo zinatumiwa kwa wingi na makampuni ya SAMSUNG, PHILIPS, HP na FUJITSU.

Idhaa ya kiswahili 2005-05-24