Kutokana na milipuko mfululizo inayotokea nchini Iraq, jeshi la Marekani nchini Iraq tarehe 23 lilitoa taarifa likisema kuwa, kuanzia tarehe 22, majeshi ya muungano ya Marekani na Iraq yameanza kusaka watu wenye silaha huko Baghdad. Katika kitendo hicho cha usakaji, watuhumiwa 285 wa makundi ya kijeshi walikamatwa. Msemaji wa jeshi la Marekani amesema kuwa, hiki ni kitendo kikubwa zaidi kinachoanzishwa kwa pamoja na jeshi la Marekani na jeshi la usalama la Iraq.
Wakati msako unaofanya Majeshi ya muungano ya Marekani na Iraq unaendelea, mpango wa Jeshi la Marekani nchini Iraq ulitangazwa kwa mara ya kwanza tarehe 22: Jeshi la Marekani litaondoka kutoka vijiji na miji ya Iraq, na kujikusanya kwenye vituo vinne vikubwa vya kijeshi vilivyoko sehemu za kaskazini, magharibi, kati na kusini, na litatoa misaada ya huduma kwa jeshi la uslama la Iraq wakati serikali ya Iraq itakapohitajika.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bibi Condoleezza Rice na waziri wa ulinzi Bw. Donald Rumsfeld wameeleza mara nyingi kuwa, hatua za kuondoka kwa jeshi la Marekani nchini Iraq ziliamuliwa na hali ya usalama ya Iraq, hivi sasa tarehe halisi ya kuondoka kwa jeshi lake bado haijapangwa. Kutokana na hali hiyo, wachambuzi wanaona kuwa, mpango wa kuanzisha vituo vinne vikubwa vya kijeshi unafichua jaribio la jeshi la Marekani la kukaa nchini Iraq kwa muda mrefu.
Wachambuzi hao wameeleza kuwa, raia wa Iraq wanataka kupata uhuru na mamlaka ya nchi mapema, na wanaona kuwa, madhumuni ya jeshi la Marekani ya kukalia Iraq ni kutaka kunyang'anya maliasili ya mafuta ya nchi hiyo, na kupata maslahi ya kiuchumi; kuzuia nguvu za Iran na Syria zinazochukua msimamo imara dhidi ya Marekani, ili kutoa uhakikisho thabiti zaidi wa usalama kwa Israel, na kutimiza mkakati wake wa kudhibiti sehemu ya Mashariki ya Kati. Ndiyo maana, raia wa Iraq hakika wanapinga nia ya jeshi la Marekani ya kukaa nchini Iraq kwa muda mrefu.
Kwanza, jeshi la Marekani kuwepo Iraq ni kisingizio kikubwa cha watu wenye silaha cha kufanya mashambulizi, mazingira mabaya ya usalama yataweka vikwazo kwa mchakato wa ukarabati wa Iraq. Makundi ya kijeshi hayakubali serikali ya mpito ya Iraq ambayo waziri mkuu wake Bw. Ibrahim al-Jaafari alichaguliwa kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika wakati jeshi la Marekani linapoikalia Iraq, na yalifanya mashambulizi mengi ya milipuko. Watu wapatao 600 wameuawa tangu serikali ya mpito ianzishwe mwishoni mwa mwezi Aprili. Kiongozi wa kundi la Al-Qaeda la Iraq ambaye pia ni mkuu wa nambari 3 wa kundi hilo Bw. Abu Musab al-Zarqawi ametangaza mara nyingi kuwa, ikiwa jeshi la Marekani litaendelea kubaki nchini Iraq, mashambulizi ya kuipinga Marekani hayatasimamishwa. Anaona kuwa, maofisa wa serikali na jeshi la polisi la Iraq kushirikiana na maadui, na kuwaweka kwenye malengo ya kufanya mashambulizi.
Pili, shughuli mfululizo za kimabavu za kuipinga Marekani zinahimiza migogoro kati ya madhehebu mbalimbali ya kidini ya Iraq kuongezeka juu zaidi. Shirikisho la wataalamu wa waislamu wa madhehebu ya Suni linalaani jeshi la Marekani na serikali ya mpito inayoongozwa na madhehebu ya Shia kuwakamata na kuwaua ovyoovyo wasuni, na mkuu wa madhehebu ya Shia Bw. Moqtada al-Sadr alilaani Jeshi la Marekani kuchochea kwa makusudi uhusiano kati ya madhehebu ya Shia na Suni, na kulitaka jeshi la Marekani iondoke kutoka Iraq.
Tatu, Marekani siku zote inapendelea Israel katika suala la Mashariki ya Kati, na kutekeleza Mpango mkubwa wa kidemokrasi wa Mashariki ya Kati katika sehemu ya Mashariki ya Kati katika miaka ya hivi karibuni, na kuzihimiza nchi za kiarabu kwenye sehemu hiyo zinfanye mageuzi kufuatana na mpango huo. Aidha, Jeshi la Marekani kuikalia Iraq pia kunaleta malalamiko kutoka kwa waamini wa dini kwenye sehemu hiyo. Wanaona kuwa, jeshi la Marekani limechafua ardhi ya waarabu, na kanuni ya nchi ya Magharibi ya "Demokrasi na Uhuru" inayoenezwa na jeshi la Marekani nchini Iraq, ni uchokozi dhidi ya dini ya kiislamu. Pia watu wengi kati yao wanaitikia mwito wa kundi la Bw. Zarqawi ya kufanya mapambano nchini Iraq. Jaribio la Jeshi la Marekani la kukaa Iraq kwa muda mrefu litasababisha watu wengi zaidi wenye silaha kutoka nchi za nje kuingia nchini Iraq, ili kupambana nalo, na kufanya hali ya usalama ya Iraq iwe ya vurugu zaidi.
Nne, mchakato wa ukarabati wa Iraq unahitaji mazingira mazuri. Endapo jeshi la Marekani linataka kukaa nchini Iraq kwa muda mrefu, litatishia nchi jirani za Iraqj, Iran na Syria. Lakini, ni vigumu kwa serikali ya Iraq kuzuia watu wenye silaha wa nchi za nje kuingia nchini Iraq bila ya ushirikiano wa nchi jirani hizo mbili katika nyanja ya usalama.
Wachambuzi wanaona kuwa, raia wa Iraq na watu wote wa kanda hiyo wanapinga Jeshi la Marekani kukaa nchini Iraq kwa muda mrefu. Serikali ya mpito inayodhibitiwa na Shirikisho la mshikamano la madhehebu ya Shia pia inatumai kupata uhuru na mamlaka ya nchi. Kutokana na hali hizo, jeshi la Marekani litakabiliwa na matatizo mengi katika siku za baadaye.
Idhaa ya Kiswahili 2005-05-24
|