Spika wa bunge la umma la China Bwana Wu Bangguo alifanya ziara rasmi ya siku 7 nchini Australia kuanzia tarehe 19 hadi 25 Mei. Katika ziara yake hiyo, spika Wu si kama tu alikutana na viongozi wa serikali ya Australia, kuhudhuria ufunguzi wa Baraza la ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Australia, na kutangaza kuanzisha duru la kwanza la mazungumzo kati ya China na Australia kuhusu mkataba wa biashara huru.
Katika ziara yake hiyo, spika Wu Bangguo pia alikagua miradi ya ushirikiano kati ya China na Australia kama vile kiwanda vya gesi, mgodi na gati la mchanga wa chuma na mingineyo. Zaidi ya hayo taasisi ya Confucius katika Chuo kikuu cha Australia magharibi ilianzishwa wakati wa ziara yake hiyo, kuanzishwa kwa taasisi hiyo kunalenga kueneza utamaduni wa taifa la China. Ziara hiyo imeongeza zaidi ushirikiano kati ya China na Australia katika sekta za siasa, uchumi na utamaduni na mawasiliano ya kimitaa. Hivyo balozi wa China nchini Australia Bibi Fu Ying alisema kuwa ziara ya spika Wu Bangguo na msafara wake ilikuwa yenye pilikapilika iliyofanikiwa vizuri.
Historia ya mawasiliano kati ya China na Australia ilianzia zaidi ya miaka 2000 iliyopita, baada ya kuingia karne ya 21, nchi hizi mbili zimeanzisha uhusiano wa wenzi wa ushirikiano unaoendelea vizuri katika hali ya utulivu na kudumu. Katika miaka ya hivi karibuni mawasiliano ya kiuchumi na kibiashara kati ya nchi hizo mbili yamekuwa barabara siku hadi siku, na ushirikiano wa pande hizo mbili umeimarishwa siku hadi siku katika sekta ya nishati na maliasili ya madini.
Ziara hiyo ya spika Wu imehimiza zaidi ushirikiano kati ya China na Australia katika sekta za uchumi na biashara. Wakati wa ziara yake hiyo, duru la kwanza la mazungumzo kuhusu mkataba wa biashara huria kati ya China na Australia yalifanyika rasmi, ambayo yatasaidia kupanua na kuzidisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika sekta za biashara, uwekezaji na utoaji huduma, pia yataleta nafasi kubwa zaidi kwa ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara wa nchi hizo mbili. Aidha, spika Wu ametoa mapendekezo ya kupanua uwekezaji wa kila upande kwa upande mwingine na kuboresha mazingira ya ushirikiano, hasa ushirikiano muhimu katika sekta ya nishati na maliasili ya madini.
Katika ziara yake hiyo, spika Wu alipokutana na viongozi wa serikali, bunge na vyama na serikali za mitaa, alisisitiza mara kwa mara kuwa hivi sasa uhusiano wa China na Australia unaendelea katika kipindi kizuri kabisa, ni matumaini kuwa pande hizo mbili zitapanua zaidi ushirikiano na kusukuma mbele maendeleo ya uhusiano. Vilevile alifahamisha msimamo wa serikali ya China ambao kamwe haitavumilia shughuli za ufarakanishaji wa kuifanya Taiwan kujitenga na China. Hayo yote yameongeza maelewano na uaminifu wa kisiasa kati ya pande hizo mbili.
Jambo linalostahiki kutajwa ni kuwa uhusiano kati ya bunge la umma la China na bunge la shirikisho la Australia umeimarishwa zaidi. Spika Wu amependekeza viongozi wa mabunge ya nchi hizo mbili wangetembeleana mara kwa mara, idara husika za nchi hizo mbili zingefanya mawasiliano na kupashana habari kwa wakati, na wajumbe wa mabunge hayo wangefundishana. Mapendekezo yake yamekubaliwa na maspika wa baraza la juu na chini la bunge la Australia..
Aidha, Spika Wu alibadilishana maoni na viongozi wa Australia kuhusu hali ya kimataifa na masuala ya kimataifa na kikanda yanayofuatiliwa na pande hizo mbili na kupata maoni mengi ya pamoja. Watu wa hali mbalimbali wa jamii wa Australia wameona kuwa ziara hiyo ya wageni mashuhuri wa China hakika itasukuma mbele maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili katika sekta mbalimbali na kuleta manufaa halisi kwa wananchi wa nchi hizo mbili.
Idhaa ya Kiswahili 2005-05-25
|