Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-05-25 15:16:42    
Wataalamu wasihi vijana lazima kuwa na mtazamo wa maendeleo ya kisayansi ili kuelekeza hifadhi ya aina nyingi za viumbe

cri
    Tarehe 22 ilikuwa siku ya 11 ya kimataifa ya aina nyingi za viumbe, wataalamu wa hifadhi ya mazingira ya viumbe wa China siku hiyo walidhihirisha hapa Beijing kuwa, kuimarisha aina nyingi za viumbe kumekuwa kazi ya dharura ya hivi sasa, na China inapaswa kuwa na mtazamo wa kujipatia maendeleo kwa njia ya kisayansi katika kuelekeza hifadhi ya aina nyingi za viumbe.

    Tarehe 22 Mei, watu zaidi ya 300 wanaofuatilia na kushiriki kwenye shughuli za hifadhi ya mazingira walikusanyika katika Chuo kikuu cha misitu cha Beijing wakisikiliza hotuba zilizotolewa na wataalamu kuhusu "Aina nyingi za viumbe ni uhakikisho wa maisha ya dunia yenye mabadiliko".

    Katika mkutano wa kutoa ripoti uliofanyika hapa Beijing, wataalamu wa hifadhi ya mazingira wa China waliainisha kuwa, aina nyingi za viumbe ni muhimu sana kwa kuhakikisha maisha ya kote duniani, na pia kuna umuhimu mkubwa sana kwa kutimiza binadamu na mazingira kuishi kwa kupatana. Hivi sasa China inatakiwa kuwa na mtazamo wa kujipatia maendeleo kwa njia ya kisayansi katika kuelekeza hifadhi ya aina nyingi za viumbe; kuzifanya kazi za hifadhi ya aina nyingi za viumbe, matumizi na uoteshaji wa aina nyingi za viumbe ziende sambamba; kufanya juhudi za kuwahamasisha wananchi washiriki katika shughuli za hifadhi ya aina nyingi za viumbe; kukamilisha sheria na kanuni, kuanzisha utaratibu wa usimamizi na tathmini na kuimarisha utafiti wa kisayansi na ushirikiano wa kimataifa.

    Naibu mkuu wa Chuo kikuu cha ualimu cha Beijing Bwana Shi Peijun alitoa pendekezo kuhusu "vielelezo viwili vyenye afya nzuri kwa dunia na binadamu" akiona kuwa, hali yenye afya nzuri kwa mfumo wa viumbe duniani inafanya kazi muhimu sana kama swichi ya kufungua na kufunga kwa maendeleo endelevu ya binadamu; kuitendea vizuri dunia na mfumo wa viumbe, ndio kuwatendea vizuri na kufuatilia binadamu wenyewe.

    "Misitu ni uti wa mgongo wa mfumo wa viumbe kwenye nchi kavu ambayo inaonesha umuhimu wake pekee katika hifadhi ya aina nyingi za viumbe". Na mkuu wa chuo kikuu cha misitu cha Beijing Bwana Yin Weilun aliainisha kuwa, hivi sasa lazima kuchukua mikakati mikubwa mitatu: mikakati ya kupatia mbegu bora za miti, kutetea kubana matumizi ya maji ya viumbe na kuendeleza shughuli mpya za kazi ya misitu, ili kutumia vizuri maliasili za viumbe vinavyokaribia kutoweka.

    Mkurugenzi wa shirikisho la marafiki wa dunia ya maumbile Bwang Liang Chongcheng alisema kuwa, kufuatilia hifadhi ya mazingira na kufuatilia hifadhi ya aina nyingi za viumbe lazima kufanya kila jambo dogo kama vile kubana matumizi ya maji hata kwa kikombe kimoja, kubana matumizi ya umeme na karatasi. Shirikisho la watu wanaojitolea wa hifadhi ya mazingira la wanafunzi wa mji mkuu Beijing pia wametoa pendekezo kwa wanafunzi watekeleze kihalisi katika vitendo vya kila dakika lengo la kuhifadhi mazingira na kuhifadhi aina nyingi za viumbe, ili kufanya kazi ya hifadhi ya mazingira kila siku na kuishi maisha yenye afya nzuri.

Idhaa ya Kiswahili 2005-05-25