Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-05-25 16:36:06    
Upigaji kura kuhusu mswada wa marekebisho wa katiba ya taifa ya Misri hautakuwa na wasiwasi

cri

Rais Hosni Mubarak wa Misri tarehe 24 alitoa hotuba mjini Cairo, akiwataka raia wajitokeze kushiriki kwenye upigaji kura kuhusu mswada wa marekebisho ya katiba utakaofanyika tarehe 25. Kabla ya hapo, vyama vingi vya upinzani nchini humo vilieleza kususia upigaji kura huo. Ushindani kati ya serikali ya Misri na vyama vya upinzani umefikia kilele wakati wa kufanya upigaji kura.

Rais Mubarak siku hiyo alipohutubia kwa njia ya televisheni alisema kuwa, kupitishwa kwa mswada huo au la kunategemea matarajio ya wananchi wote wa Misri. Aliwataka wananchi wote washiriki katika upigaji kura kwa moyo wa kizalendo na kuwajibika katika wakati wa kuamua mambo ya taifa, ili kufanikisha mchakato wa demokrasia wa Misri. Hotuba ya Rais Mubarak imefafanua zaidi msimamo wa serikali ya Misri wa kurekebisha katiba ya taifa na kuhimiza demokrasia na kuwatia moyo watu.

Tarehe 10 mwezi huu, bunge la umma la Misri lilipitisha mswada wa marekebisho kuhusu njia ya uchaguzi wa urais ya katiba hiyo. Mswada wa uchaguzi huo unasema kuwa kuanzia mwezi Septemba mwaka huu, uchaguzi wa urais utakapofanyika, rais atachaguliwa kutoka wagombea wengi kwa njia ya kupigiwa kura moja kwa moja na raia, badala ya bunge la umma kuteua mgombea mmoja pekee wa urais, halafu achaguliwe kwa upigaji kura wa raia kama hapo awali.

Mswada wa marekebisho ya katiba mpya ulipitishwa kwa kura nyingi kabisa kwenye bunge la umma, lakini ulipingwa vikali na vyama vikubwa mbalimbali vya upinzani. Vyama vitatu vya bunge kikiwemo chama cha Mew Wafd tarehe 17 vilitangaza kususia upigaji kura huo na kuchelewesha bila kikomo uteuzi wa wagombea wake wa urais wa vyama vya upinzani. Siku hiyo, jumuiya kubwa ya kiislamu ya Misri, Moslem Brotherhood iliyofutwa iliamua kujiunga na harakati za ususiaji wa vyama vitatu vya upinzani. Tarehe 21, chama cha upinzani Al-Ghad pia kilijiunga na safu ya ususiaji huo. Hadi hapo idadi ya vyama vya upinzani vinavyosusia upigaji kura ilifikia vitano.

Kutokana na kukabiliwa na shinikizo kubwa kutoka kwa vyama vya upinzani, serikali ya Misri ilichukua hatua mara moja kujibu mashambulizi hayo, ili kuhakikisha upigaji kura unaendelea bila vikwazo.

Vyombo vya habari vinaona kuwa ingawa vyama vya upinzani vilifanya harakati kubwa za kuipinga serikali kwa ajili ya kugombea madaraka makubwa zaidi, lakini kutokana na kuwa nguvu zao ni ndogo na msingi wao ni dhaifu, kwa hiyo harakati hizo hazitaathiri matokeo ya upigaji kura wa raia. Mswada wa marekebisho ya katiba uliotolewa na chama tawala cha National Democratic kinachoongozwa na rais Mubarak utakubaliwa na wananchi wa Misri na kupitishwa kwenye upigaji kura wa raia.

Idhaa ya kiswahili 2005-05-25