Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-05-25 18:22:22    
Mapishi ya vipande vya nyama ya kuku pamoja na figili

cri

Mahitaji

Figili gramu 250, nyama ya kuku gramu 100, kiasi kidogo cha mafuta, vitunguu saumu, chumvi, siki, sukari, M.S.G, pilipili hoho, na wanga.

Njia

1. osha figili, halafu ondoa sehemu yake ya juu, uikate vipande vipande. Kata nyama ya kuku iwe vipande vipande, vipakue ndani ya bakuli moja, tia wanga, chumvi na mafuta kidogo. Kata vitunguu saumu na pilipili hoho ziwe vipande.

2. pasha moto na mimina maji ndani ya sufuria, baada ya kuchemsha, tia mafuta na chumvi kidogo, halafu tia vipande vya figili ndani ya maji, baada ya sekundu 20 vipakue na iweke ndani ya maji baridi, vipakue. Tia vipande vya nyama ya kuku ndani ya maji yaliyochemka, koroga koroga ili vigawanyike, baada ya nyama ya kuku kuive, ipakue na uiweke kwenye maji baridi.

3. tia vipande vya figili na nyama ya kuku ndani ya bakuli kubwa, Tia pilipili hoho ndani ya sufuria yenye mafuta, ichanganye na mafuta kwa kurusharusha kisha ipakulie kwenye bakuli hii, tia sukari, siki, chumvi, M.S.G, koroga koroga. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.