Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-05-25 19:47:42    
Mazungumzo ni njia bora ya utatuzi wa mgogoro wa biashara

cri
    Wasikilizaji wapendwa, mjumbe wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia mambo ya biashara Bw. Peter Mandelson tarehe 24 huko Brussels alikuwa na mazungumzo na naibu waziri wa biashara wa China Bw. Gao Hucheng, ambaye aliwasili huko kwa lengo la kutatuta mgogoro wa biashara ya nguo uliotokea hivi karibuni. Taarifa fupi iliyotolewa na kamati ya Umoja wa Ulaya baada ya kumalizika kwa mazungumzo hayo, inasema kuwa kwa jumla, mazungumzo hayo ni ya kufuatilia utatuzi, ambayo yanaonesha kuwa Umoja wa Ulaya na China zimepiga hatua ya kwanza katika njia ya kutatua mgogoro wa biashara kwa mazungumzo.

    Tokea mwaka huu uanze, pamoja na kuondolewa mgao wa bidhaa za nguo duniani, nguo zilizosafirishwa na China kwa nchi za Ulaya na Marekani ziliongezeka kwa kiwango kikubwa. Baada ya kuingia mwezi Aprili, Marekani na Umoja wa Ulaya zilitangaza kwa nyakati mbalimbali kuweka kikomo cha biashara na kufanya uchunguzi kuhusu "Kinga maalumu" ili kulinda maslahi ya wafanyabiashara wadogo na wastani wa nguo wa nchi zao. Marekani kati ya tarehe 13 na 18 mwezi May iliweka kikomo mara mbili kuhusu aina 7 za nguo za China, hatua ambayo imezusha mkwaruzano wa biashara ya nguo kati ya China na Marekani.

    Ni jambo la kawaida kutokea mgongano na mgogoro katika biashara ya kimataifa. Kitu muhimu ni katika kukabiliana na migogoro na migongano hiyo, nchi inajichukulia uamuzi na kuweka vikwazo tu au kuitatua ipasavyo kwa njia ya mashauriano na mazungumzo. Waziri mkuu wa China Bw. Wen Jiabao tarehe 11 mwezi huu alipokuwa na mazungumzo na waziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya alisema kuwa kupunguza migongano iliyopo hivi sasa kuhusu biashara ya nguo, kunataka pande zote mbili kufanya juhudi, China na Ulaya zinatakiwa kuweka mbele uhusiano wa pande zote wa kiwenzi, kuimarisha mazungumzo na kutafuta utatuzi wake. Maneno hayo ya waziri mkuu Wen Jiabao yameonesha msimamo wa siku zote wa serikali ya China. Aidha, ukweli wa siku za nyuma umeonesha kuwa njia yoyote ya kujaribu kutatua mgogoro wa biashara kwa kujichukulia uamuzi, si kama tu haitaweza kusaidia utatuzi wa matatizo, bali ni kinyume chake kuwa itazidisha mgongano hata kuzusha vita vya biashara.

    Ili kupunguza mgongano wa biashara kati ya China na Marekani na kuhakikisha kuwa utandawazi wa biashara ya nguo duniani kuendelea kwa utulivu, China imechukua hatua kadha wa kadhaa zikiwemo za kuongeza ushuru wa usafirishaji bidhaa kwa nje na kupunguza kiwango cha ushuru unaorudishwa. Tarehe 20 mwezi huu, China ilitangaza tena kuongeza ushuru wa aina 74 za nguo zinazosafirishwa kwa nchi za nje tokea tarehe 1 Juni mwaka huu na kuongeza sharti kwa nguo zinazosafirishwa kwa nje. Katika hali ya hivi sasa hatua hizo zinaonekana kuwa na maana kubwa na kuonesha msimamo wa kuwajibika wa China katika biashara ya kimataifa.

    Endapo Marekani na Ulaya zitatekeleza uamuzi wa kuweka kikomo kwa nguo za China, basi siyo China peke yake itakayoathiriwa, hatimaye Marekani na Ulaya pia zitaathirika wakiwemo wafanyabiashara wao wanaoagiza bidhaa, na wauzaji wa rejareja pamoja na wawekezaji nchini China na wanunuzi wa nchini mwao. Katika muda mrefu uliopita, ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani na kati ya China na Ulaya ulipata mafanikio makubwa, hali hiyo inaonesha kuwa uhusiano kati yao ni wa kunufaishana, ambao si kama tu umehimiza maendeleo ya uchumi wa pande mbili, bali pia umeleta manufaa kwa watu wa nchi mbili.

    Kwa ujumla, kutokea kwa baadhi ya matatizo katika ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya china na Ulaya ni hali ya kawaida. Pande zote husika zingefahamu na kufanya uchambuzi kuhusu chanzo chake na kutafuta njia nzuri ya utatuzi na kulinda kwa pamoja maslahi ya biashara kati yao.

Idhaa ya Kiswahili