Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Bw. Michel Barnier, waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Bw. Joschka Fischer na waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Bw. Jack Straw tarehe 25 walifanya mazungumzo na mwakilishi mkuu wa mazungumzo wa Iran kuhusu suala la nyuklia la nchi hiyo Bw. Hassan Rohani kwa muda wa saa 3 huko Geneva, na kuamua kuwa mazungumzo kuhusu suala hilo yataendelea. Hivyo, hali ya wasiwasi ya mazungumzo hayo hivi karibuni imelegezwa kwa muda.
Kutokana na kuwa baada ya tarehe 30 mwezi Aprili, Iran ilitangaza kwa mara nyingi kuwa, hata kama mazungumzo hayo ya mawaziri yatafanikiwa au la, Iran itafufua shughuli za kusafisha Uranium. Hivyo, mazungumzo ya tarehe 25 mwezi huu ni fursa ya mwisho kwa kuokoa mazungumzo kuhusu suala la nyuklia la Iran. Kama mazungumzo hayo yakisimamishwa, suala la nyuklia la Iran litafikishwa kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.
Kwenye mazungumzo hayo, Umoja wa Ulaya uliahidi kutoa pendekezo kamili kwa Iran, ili kuvunja hali ya kukwama kwa mazungumzo kuhusu suala hilo kabla ya mwezi Julai. Pendekezo hilo la Umoja wa Ulaya linahusu kusaidia Iran kujenga na kutekeleza mpango wa nyuklia kwa matumizi ya amani, kuimarisha ushirikiano wa pande zote na Iran na kuanzisha majadiliano kuhusu Iran kujiunga na WTO. Pande hizo mbili zitafanya majadiliano ya ziada huko Teheran. Bw. Hassan Rohani aliona kuwa, inawezekana kwa pande hizo mbili kufikia makubaliano kamili katika muda mfupi, na kabla ya hapo, Iran itatekeleza ahadi zake kuendelea kusimamisha shughuli za kusafisha uranium.
Zaidi ya mwaka mmoja uliopita, ili kuinua athari ya Umoja wa Ulaya wenye kanda ya Mashariki ya Kati, na kutoipa Marekani kisingizio cha kuingilia kati ya mambo hayo, nchi tatu za Ufaransa, Ujerumani na Uingereza zilianza kusuluhisha suala la nyuklia la Iran. Ingawa nchi hizo zilikabiliwa na matatizo mengi, lakini juhudi zao zimepata mafanikio ya mwanzo. Umoja wa Ulaya unapinga suala hilo litatuliwe kwa nguvu za kijeshi, au lifikishwe kwenye baraza la Usalama. Kama Marekani ikianzisha mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Iran, itavuruga zaidi hali ya kanda ya Mashariki ya Kati, hata itaathiri usalama na utulivu wa Ulaya. Kudumisha uhusiano wa kirafiki na Iran kunalingana na maslahi ya kiuchumi ya Umoja wa Ulaya. Aidha, Umoja wa Ulaya unachukua fursa hii kama uzoefu wa kutekeleza diplomasia ya amani.
Kuhusu suala hilo, Iran inataka kutumia fursa hii kuendeleza uhusiano kamili wa ushirikiano na Umoja wa Ulaya, na kupata manufaa ya kiuchumi. Hivyo, Iran inafanya usuluhishi kwenye mazungumzo, lakini haitavunja mazungumzo hayo.
Lakini suala la nyuklia la Iran bado ni la utatanishi na itachukua muda mrefu kulitatua suala hilo. Kutokana na hali ya hivi sasa, maendeleo ya suala hilo yanategemea kuwa, kama pendekezo litakalotolewa na nchi za Ufaransa, Ujerumani na Uingereza litapokewa na Iran au la, na kama Iran itaweza kutekeleza ahadi zake kuendelea kusimamisha shughuli za kusafisha Uranium au la. Wachambuzi wa Ulaya wanaona kuwa, kutoka mwanzoni hadi hivi sasa, Iran imeshikilia siku zote haki yake ya kuendeleza na kutumia nishati ya nyukila kwa amani. Lakini msimamo huo haukubaliwi na kupokewa na nchi za magharibi. Hivyo, bado ni mapema kukadiria suala hilo litatatuliwa kwa njia gani.
Idhaa ya Kiswahili 2005-05-25
|