Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-05-26 18:23:58    
Maliasili za kimaumbile nchini China

cri

China ni nchi yenye maliasili nyingi na inazalisha bidhaa nyingi za maliasili duniani. Katika muda mrefu China inatimiza lengo lake la kuendeleza uchumi kwa kutegemea maliasili zake. Asilimia 95 ya nishati zinazotumika kwa mara moja, asilimia 80 ya malighafi zinazotumiwa viwandani, na asilimia 70 ya pembejeo za kilimo zinatokana na maliasili hizo. Matumizi ya maliasili ya bahari yamesukuma mbele ongezeko jipya la uchumi wa taifa. Lakini kutokana na idadi kubwa ya watu, maliasili bado hazitoshi, na uchafuzi wa mazingira bado ni mkubwa, mambo hayo yote yamekuwa sababu muhimu zinazozuia maendeleo ya uchumi na jamii ya China. Ziada ya bidhaa za madini katika baadhi ya vipindi, ukosefu wa aina kadhaa za madini, na upungufu wa ujumla wa madini viko pamoja nchini China. Kuhakikisha maliasili ya mashamba ambayo ni mahitaji ya usalama wa uzalishaji wa chakula, na kuhakikisha maliasili ya madini ambayo ni mahitaji ya maendeleo ya viwanda ni kazi ya muda mrefu.

Baada ya mkutano wa kikazi kuhusu idadi ya watu, maliasili na mazingira uliofanyika mwaka 1999, sehemu na idara mbalimbali zinajifunza kwa makini moyo wa mkutano huo, na kutekeleza kithabiti sheria na kanuni kuhusu maliasili za kimaumbile. Njia za matumizi na usimamizi wa ardhi na maliasili zimebadilishwa. Uzoefu umethibitisha kuwa, sera ya China kuhusu ardhi na maliasili ni sahihi.

Eneo la mashamba yanayotumiwa kwa ujenzi limedhibitiwa. Mwaka 1999, mashamba mapya yanaongezeka kwa kiasi kikubwa, na ongezeko hilo lilikuwa mara mbili ya ongezeko la mashamba yaliyotumiwa kwa ujenzi.

Utaratibu wa usimamizi wa ardhi na madini unaendelea kuboreshwa. Vitendo vya kutumia onyo mashamba kwa ajili ya ujenzi na kuchimba ovyo madini vimezuiliwa kwa njia ya kuimarisha utekelezaji wa sheria.

Usimamizi wa ujumla umeboreshwa. Mpango wa ujumla wa matumizi ya ardhi nchini China katika kipindi cha mwaka 1997 hadi mwaka 2010, mipango ya mikoa 31 na mipango ya miji 64 ilipitishwa na baraza la serikali ya China na kuanza kutekelezwa. Mwaka 1999 utekelezaji wa mpango wa matumizi ya ardhi ulipata mafanikio mazuri.

Utaratibu mpya wa kupanga ardhi na maliasili kwa mujibu wa mahitaji ya soko umeanza kuundwa. Mageuzi ya utaratibu wa usimamizi wa vikundi vya kutafuta madini yalimalizika kwa mafanikio. Na sehemu mbalimbali zinafanya juhudi kuendeleza masoko ya ardhi na madini.

Kazi ya upimaji wa ardhi na maliasili imeimarishwa, duru jipya la upimaji wa ardhi na maliasili lilianzishwa, na miradi kadhaa ya upimaji wa ardhi na madini imepata maendeleo.

Idaa ya Kiswahili 2005-05-24