Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-05-27 11:46:00    
Madaktari wa China wanaofanya kazi nchini Msumbiji

cri
Katika hospitali kubwa zaidi ya taifa ya Msumbiji yaani Hospitali ya Maputo, daktari wa China anayefanya kazi katika idara ya wanawake wajawazito bibi Leifang aliyemaliza kumfanyia upasuaji mwanamke mmoja mwenyeji, alimwonesha mwandishi wa habari miwani yake mikubwa na nzito, akimwambia kuwa vitu vilivyobaki kwenye miwani yake ni usaha wa mwanamke aliyefanyiwa upasuaji, ambaye ni mgonjwa wa Ukimwi. Daktari Lei alieleza kuwa, ni hatari kuwafanyia upasuaji wagonjwa wa Ukimwi, kwa sababu katika upasuaji, madaktari wanaweza kuambukizwa virusi vya Ukimwi vinavyokuwa kwenye damu au usaha wa wagonjwa, hivyo kila anapofanya upasuaji kwa wagonjwa wa Ukimwi, anavaa nguo, kifuniko na miwani mikubwa, ili kukinga maji ya mwili wa mgonjwa kulowanisha ngozi yake, hasa ngozi yenye kidonda.

Idadi ya watu wanaoambukizwa visusi na kupatwa ugonjwa wa Ukimwi inaongezeka kwa haraka, na inakaribia milioni nchini Msumbiji, hali ya kuenea kwa Ukimwi inawatia watu wasiwasi mkubwa. Mwaka 2003, watu wenye Ukimwi na walioambukizwa virusi vya Ukimwi wameongezeka na kuwa asilimia 14.6 kati ya watu wote nchini humo kutoka asilimia 12.2 ya mwaka 2002.

Mkuu wa kikundi cha madaktari wa China nchini Msumbiji Bwana Zhou Weiliang alisema kuwa, miongoni mwa watu wanaolazwa hospitalini, wagonjwa wa Ukimwi ni wengi zaidi, ambao wamefikia asilimia 60, kwa mfano wagonjwa wenye uvimbe kwenye tumbo karibu wote ni wagonjwa wa Ukimwi, kwa sababu uwezo wa mwili wa kujikinga na maradhi kwa wagonjwa wa Ukimwi ni mdogo ukilinganishwa na watu wasioambukizwa, ni rahisi kwao kupata maradhi mbalimbali hasa ya ndani ya mwili.

Daktari Lei Fang alimwambia mwandishi wa habari kuwa, ingawa madaktari wote wako makini sana, lakini wakati mwingine bahati mbaya inaweza kutokea, mikono ya madaktari wengi wa China ilijeruhiwa wakati wakiwafanyia upasuaji wagonjwa.

Mpaka sasa jumla ya madaktari wanne wa China nchini Msumbiji waliojikata mikononi wakati wa kuwafanyia wagonjwa upasuaji, na huenda wameambukizwa virusi vya Ukimwi.

Bwana Zhou Weiliang ni mmoja kati ya wachina hao wanne. Alisema kuwa katika upasuaji uliofanyika miezi miwili iliyopita, wakati upasuaji ulipoingia katika hatua ya mwisho, mkono wake ulichomwa na sindano iliyokuwa imeshikwa na msaidizi wake. Bwana Zhou alisema kuwa aliondoa glavu yake mara moja, na kusafisha mikono mara nyingi, lakini baada ya kufanyiwa uchunguzi, alithibitishwa kuwa ameambukizwa virusi vya Ukimwi.

Bwana Zhou alitumia madawa fulani mara moja Madawa hayo yanasaidia kwa kiasi kupunguza maumivu ya wagonjwa wa Ukimwi na kuzuia watu walioambukizwa virusi vya Ukimwi wasiwe kuwa wagonjwa wa Ukimwi. Lakini madawa hayo yanaathiri vibaya afya ya binadamu, watu hujisikia vibaya sana baada ya kutumia madawa hayo, kiasi kwamba uzito wa bwana Zhou na madaktari wengine ulipungua kwa kilo zaidi ya tano.

Daktari Lei Fang alieleza kuwa, ingawa madawa hayo ni makali, wlakini madaktari hao wawili walishikilia kuendelea na kazi, na hawakuomba mapumziko hata siku moja.

Bwana Zhou Weiliang alisema, kuanzia utotoni alivutiwa na hadhithi ya daktari Norman Bethune. Bwana Bethune aliyetoka Canada alikuja nchini China kuwatib askari wa jeshi la China wakati wa vita dhidi ya wavamizi wa Japan katika miaka ya 30 ya karne iliopita. Alijeruhiwa mkononi alipofanya upasuaji na mwishowe alifariki dunia kutokana na ugonjwa wa damu. Bwana Zhou alisema kuwa, wakiwa madaktari, hawawezi kukataa kuwatibu wagonjwa wowote, hata wagonjwa wa Ukimwi.

Yan Bincheng ni daktari mwingine aliyejeruhiwa wakati wa kuwafanyia upasuaji wagonjwa, alisema, wana wasiwasi mkubwa wa kuambukizwa virusi vya Ukimwi, lakini wakiambukizwa, hawatajuta kwa sababu wanatoa mchango kwa ajili ya kuwatibu wagonjwa wa Afrika.

Katika miaka 40 ilyopita tangu kikundi cha kwanza cha madaktari wa China kufika barani Afrika, jumla ya madaktari 43 walijitoa mhanga katika bara hilo. Lakini wanaowafuata madaktari hao hawarudi nyuma hata kidogo, wanaendelea kutoa mchango kwa ajili ya wagonjwa wa Afrika.

Idhaa ya Kiswahili 2005-05-27