Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-05-27 16:13:43    
Ziara ya Mahmood Abbas nchini Marekani ina mafanikio gani?

cri

Tarehe 26, mwenyekiti wa mamlaka ya Palestina Bw. Mahmood Abbas alikutana na rais George Bush wa Marekani na kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini Marekani. Kabla ya kwenda nchini Marekani Bw. Abbas alieleza kuwa, katika ziara yake ataitaka Marekani iahidi hadharani kuunga mkono kuanzishwa nchi kwa Palestina, kuongeza misaada ya uchumi kwa Palestina na kufanya uratibu kuhusu mpango wa upande mmoja wa Israel kuondoka katika sehemu ya Gaza. Basi Je, ziara hiyo ya Bw. Mahmood Abaas nchini Marekani imekuwa na mafanikio gani?

Bw. Mahmood Abbas ni kiongozi wa juu kabisa wa Palestina aliyekutana na rais Bush wa Marekani kwa mara ya kwanza mjini Washington tangu mwezi Desemba mwaka 2000 alipochaguliwa kuwa rais wa Marekani na kumsusia kiongozi wa zamani wa Palestina marehemu Yasser Arafat. Baada ya mkutano huo, kwenye mkutano na waandishi wa habari rais Bushi alisisitiza kuwa Marekani bado inashughulika na mpango wa amani ya Mashariki ya Kati na kujitahidi kuijenga nchi ya Palestina iliyo huru, amani na demokrasia. Aliendelea kusema, Wapalestina wana uwezo wa kuendesha nchi yao na kuishi kwa amani na nchi jirani, tena nchi ya Palestina iliyo ya amani pia inaambatana na maslahi ya Israel. Bush pia aliwataka viongozi wa Israel na Palestina wajitahidi kuboresha hali ya kibinaadamu ya Palestina, kuondoa makazi ya Wayahudi yasiyoruhusiwa na kusimamisha ujenzi wa makazi mengine ya Wayahudi.

Bw. Mahmood Abbas alieleza kwenye mkutano huo kuwa anafuatilia sana Israel kuendelea kujenga makazi ya Wayahudi, Palestina inapenda kujadiliana na Israel kuhusu mpango wa upande mmoja, kwani hii ni sehemu moja ya kumaliza ukaliaji wa Israel, na pande mbili Palestina na Israel zinapaswa kufanya mazungumzo mara moja kuhusu hadhi ya mwisho ya Jerusalem ya mashariki, makazi ya Wayahudi, wakimbizi wa Palestina na mpaka kati yao.

Wachambuzi wanaona kuwa ziara hiyo ya Abbas imepata mafanikio fulani. Kwanza, Bush alimsifu Abbas kuwa ni kiongozi anayeweza kushirikiana na kuaminiwa. Bush alipomkaribisha Bw. Abbas kwenye Ikulu, alipongeza juhudi alizofanya Abbas katika kupambana na makundi yenye msimamo mkali ya Palestina, kuharakisha mageuzi, kuondoa ufisadi na kustawisha uchumi.

Pili, Bush alisisitiza msimamo wa Marekani wa kuunga mkono mpango wa amani na kuunga mkono kuanzishwa nchi kwa Palestina. Zaidi ya hayo, Rais Bush aliahidi kuipatia serikali ya Palestina msaada wa dola za kimarekani milioni 50.

Jambo linalostahili kufuatiliwa ni kuwa msimamo wa rais Bush kuhusu mpango wa amani haujabadilika sana na Marekani haichukui msimamo mkali zaidi kwa Israel. Hivi sasa baadhi ya wabunge wa Marekani bado wana wasiwasi kuhusu ufisadi uliopo katika serikali ya Palestina. Kwa hiyo si rahisi kutekeleza ahadi ilizotoa Marekani kwa Abbas.

Idhaa ya kiswahili 2005-05-27