Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-05-30 15:16:58    
Maskani ya Tiara za China

cri

Mji wa Weifang uko mkoani Shandong, pwani ya mashariki ya China. Tukitaja Weifang, watu wengi wa China kwanza wanaweza kupata picha ya tiara za huko. Watu wakifika huko, mara moja watavutiwa na hali nzito ya tiara ya huko, ambapo popote wanapokwenda wanaweza kuona tiara za aina mbalimbali zinazopeperuka angani, na kando mbili za njia kuna vibanda vingi vidogo vidogo vya mauzo ya tiara, hata makao makuu ya Shirikisho la tiara la kimataifa pia yako mjini humo. Kwa kawaida watu wakifika Weifang hununua tiara kadhaa kwa ajili ya kuwazawadia jamaa na marafiki.

Kuanzia mwaka 1984, kila ifikapo mwishoni mwa mwezi Aprili, siku ya tiara ya kimataifa hufanyika huko Fuyanshan kwenye kitongoji cha mji huo, ambapo wataalamu wa tiara kutoka sehemu mbalimbali duniani hukusanyika huko kuonesha ustadi wao wa kutengeneza tiara na kupeperusha tiara. Katika siku hiyo, watalii wanaona kama wanakaa katika bahari ya tiara, ambapo wanaweza kuona tiara nyingi za aina mbalimbali kubwa na ndogo, tiara ile kubwa hata ilikuwa na uzito wa kilo 3000 na urefu wa mita 1500, na tiara ile ndogo hata iliweza kuwekwa ndani ya kikasha cha kibiriti. Lakini kama watalii hawakufika huko Weifang wakati wa siku ya tiara, vilevile wanaweza kupata fursa nzuri ya kuangalia na kutafiti kwa makini tiara.

Mwalimu wa Chuo kikuu cha Weifang Bwana Duan Yong alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa, mjini Weifang kuna Jumba la makumbusho ya tiara za duniani, ambapo zimehifadhiwa na kuoneshwa tiara nyingi adimu za China na nchi za nje pamoja na nyaraka za kale kuhusu tiara, watalii wangekwenda kutembelea kwa makini. Bwana Duan alisema:

Katika jumba hilo la makumbusho ya tiara, kuna tiara za aina mbalimbali zilizotengenezwa zamani sana ambazo ziliwahi kupewa tuzo, watu wakitembelea ndani wataongeza sana ujuzi pia kuelewa utamaduni wa jadi wa taifa la China, na kujua jinsi tiara ilivyotengenezwa na kuboreshwa siku hadi siku. Na hivi sasa baada tiara zinatengenezwa kwa njia ya kisayansi na kiteknolojia ya juu, hata vifaa vya utengenezaji vinabadilika siku hadi siku.

Mbali na jumba la makumbusho, vibanda vidogo vidogo vya mauzo ya tiara vilivyotapakaa mitaani pia vinaweza kuwasaidia watalii kuelewa utamaduni wa tiara. Katika kibanda kimoja, mwandishi wetu wa habari aliambiwa kuwa, kibanda chake kinauza hasa tiara za kisasa, na vifaa vya kutengeneza tiara hizo ni hariri za kukinga mvua na plastiki ngumu zilizotengenezwa kuwa vifaa vigumu vinavyosifiwa kuwa ni chuma na chumba cha pua cha kioo, tiara zilizotengenezwa kwa vifaa hivyo zikilinganishwa na tiara za jadi zinaonekana ni ngumu na imara zaidi, tena zina bei nafuu zaidi, hivyo zinanunuliwa na watu wengi zaidi. Mwendeshaji wa kibanda hicho Bibi Xing Xiangyan alisema:

Tiara zilizotengenezwa kwa mtindo wa kisasa kwa kawaida zilipita taratibu za kikazi zaidi ya 10 hata 20. Aina za tiara hizo ni nyingi sana, kwa mfano tiara za "vipepeo" zina aina zaidi ya kumi kadhaa, tiara hiyo ndogo kabisa ni kama kikasha cha kibiriti, na tiara hiyo kubwa inaweza kutengenezwa kutokana na ombi la wateja bila kujali mita ngapi.

Idhaa ya kiswahili 2005-05-30