Kabla ya upigaji kura za maoni ya raia nchini Ufaransa, viongozi wa Umoja wa Ulaya na Ufaransa walitoa wito wa kutaka watu wa Ufaransa wapige kura ya ndiyo kuunga mkono "mkataba wa katiba ya Umoja wa Ulaya", walisema, "Si kama mnapiga kura kwa ajili ya Ufaransa peke yake, bali mnapiga kura kwa ajili ya Ulaya." Lakini kura zilizopigwa tarehe 29 nchini Ufaransa zilikataa "mkataba wa katiba ya Umoja wa Ulaya".
Tarehe 9 mwezi Mei mwaka 1950 waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa wa wakati ule Bw. Robert Schuman alitangaza "azimio la Schuman" ambapo Ulaya ulianzisha mchakato wa umoja, kutokana na hayo, Bw. Schuman anasifiwa kuwa "baba wa Ulaya". Lakini Bw. Schuman hakutarajia kama siku ya leo baada ya kupita nusu karne, ni mfaransa ambaye amefanya mchakato wa umoja wa Ulaya kupiga breki ya ghafla. Ingawa kura ya hapana ya Ufaransa haiwezi kusimamisha kabisa mchakato wa umoja wa Ulaya, lakini pigo ililotoa dhidi ya umoja wa Ulaya ni dhahiri kabisa.
Katika miaka mingi iliyopita, Ufaransa na Ujerumani zilichukuliwa kuwa injini na kitovu cha kuhimiza ujenzi wa Ulaya. Lakini hivi sasa nusu ya injini hiyo imekuwa na matatizo. Ni kama gazeti la "The Guardian" la Uingereza lilivyosema kuwa Ufaransa ilipiga kura ya hapana dhidi ya "mkataba wa katiba ya Umoja wa Ulaya" ni kama kuwa moyo unasema "hapana" juu ya mwili. Hatua hiyo si kama tu itaathiri hadhi na umuhimu wa Ufaransa katika Umoja wa Ulaya siku za baadaye, bali pia itaathiri nguvu ya mshikamano ndani ya umoja huo. Baadhi ya wachambuzi wanaona kuwa kupiga kura ya hapana "mkataba wa katiba ya Umoja wa Ulaya" kwa Ufaransa kutachangia kuundwa "kitovu" kilichoundwa na nchi za kimaendeleo kabisa ndani ya Umoja wa Ulaya, jambo ambalo linahofiwa na nchi wajumbe wengi wa umoja huo.
Katika miaka ya karibuni, pamoja na kuendelea kwa mchakato wa umoja wa kisiasa na kiuchumi wa Ulaya, nguvu ya Umoja wa Ulaya iliimarika mwaka hadi mwaka, na Umoja wa Ulaya ulikuwa na dukuduku ya kuonesha hadhi yake iliyoinuka duniani pamoja na azma yake ya kufanya kazi muhimu zaidi kuhusu mambo ya kimataifa. Mwezi Mei mwaka jana, kupanuka kwa Umoja wa Ulaya kulichukuliwa ni kama mnara muhimu wa historia wa kutimiza lengo la kuleta umoja mkubwa wa Ulaya. Kujiunga na Umoja wa Ulaya kwa nchi kumi za wajumbe wapya kumefikisha Umoja wa Ulaya kwenye kiwango kipya katika pande za maeneo, idadi za watu na nguvu za kiuchumi. Baadhi ya mambo katika "mkataba wa katiba ya Umoja wa Ulaya", ambayo ni pamoja na kuweka nafasi za mwenyekiti wa baraza la waratibu wa Ulaya na waziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya na kuanzisha wizara ya mambo ya nje ya Ulaya, yalikuwa na nia ya kuzungumza na nje kwa sauti moja na kuongeza sifa ya Umoja wa Ulaya duniani. Hivi sasa Umoja wa Ulaya umeanzisha mazungumzo kuhusu maombi ya ujumbe ya nchi za Romania na Bulgaria, na kunuia kuzikubali rasmi tarehe 1 mwezi Januari mwaka 2007, lakini tatizo lililoko hivi sasa ni kuwa hali mbaya ya ufanisi mdogo wa mkataba wa Umoja wa Ulaya na hali ngumu ya kufanya uamuzi ya hivi sasa, ambavyo vinashindwa kuendesha vizuri shughuli za Umoja wa Ulaya uliopanuliwa.
Katika upande wa uchumi, kwa kuwa Umoja wa Ulaya ulikuwa na tahadhari kuhusu Ufaransa kupiga kura ya hapana kuhusu "mkataba wa katiba ya Umoja wa Ulaya", hivyo hatua hiyo haikuleta mgogoro kwa Umoja wa Ulaya, lakini ni kama baadhi ya wanasiasa wa Ulaya walivyoonya kuwa kura ya hapana ya Ufaransa itafanya maendeleo ya Umoja wa Ulaya kupoteza lengo lake na kupoteza imani ya wawekezaji, hali ambayo itaathiri vibaya maendeleo ya uchumi wa Ulaya katika muda mrefu ujao.
Idhaa ya Kiswahili 2005-05-31
|