Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-05-31 14:52:35    
"Baraza la Fortune" lafuatilia maendeleo ya uchumi ya China

cri

Kongamano la 9 la Baraza la Fortune lililofanyika kwa siku tatu, lilimalizika hivi karibuni hapa Beijing. Wakurugenzi wakuu kutoka makampuni ya kimataifa zaidi ya 70 yaliyochukua nafasi za 500 za mwanzo duniani pamoja na wanaviwanda na maofisa wa China wapatao mamia kadhaa walishiriki kwenye majadiliano kuhusu maendeleo ya China na nchi za sehemu nyingine za Asia na masuala mengine likiwemo nafasi zinazotolewa na China kwa makampuni makubwa ya kimataifa.

Baraza la Fortune duniani lilianzishwa na jarida la "Fortune" la kampuni ya Time Warner nchini Marekani mwaka 1995, baraza hilo linafanyika mara moja kila mwaka kwenye sehemu inayovutia zaidi duniani, ambalo linaalika wakurugenzi wakuu na viongozi watendaji wa makampuni za kimataifa, wanasiasa na wasomi mashuhuri duniani kujadili masuala yanayoikabili sekta ya biashara duniani. Kongamano la mwaka huu lililofanyika hapa Beijing ni la tatu lililofanyika nchini China likifuatia makongamano mawili yaliyofanyika mwaka 1999 na mwaka 2001 kwenye miji ya Shanghai na Hong Kong nchini China.

Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Time Warner Bw. Richard D. Parsons alipoeleza sababu ya kuitisha kongamano la "Baraza la Fortune" duniani kwa mara tatu nchini China katika miaka 6 iliyopita, alisema,

"Mwaka 1999 ulikuwa wa mara ya kwanza kwa "Baraza la Fortune" kufanya kongamano nchini China, katika miaka michache iliyopita, tunaweza kuona mabadiliko yaliyotokea mara kwa mara nchini China, ambayo kasi yake inashangaza watu. Hakuna nchi au sehemu nyingine ambazo zinaweza kupata maendeleo kwa kasi kama ya maendeleo ya China. China imekuwa sehemu moja isiyoweza kukosekana duniani na inafanya kazi, ambayo nchi yoyote nyingine inaweza kufanya katika utandawazi wa uchumi duniani."

Maendeleo ya kasi ya uchumi wa China yamefuatiliwa na dunia nzima, jarida la "Fortune" limeweka "Karne ya China na Asia mpya" kuwa ni kaulimbiu ya kongamano la mwaka huu. Njia ya maendeleo ya viwanda, maendeleo ya viwanda vya magari, soko la simu za mkononi, soko la mitaji, nishati pamoja na masuala mengine ya China yalifuatiliwa sana na kongamano la mwaka huu. Kampuni na viwanda vya China na nchi za nje vilivyoshiriki kongamano hilo vilizidi 400 na idadi ya watu walioshiriki kongamano ilizidi 800. Maneno mengi yaliyozungumzwa na viongozi wa sekta ya biashara duniani kwenye kongamano hilo yalikuwa ni kuhusu maendeleo ya kasi ya China, ambayo si kama tu kuwa yameleta ustawi na maendeleo kwa China yenyewe, bali pia yameleta nafasi nyingi kwa dunia.

Mkurugenzi wa idara ya kimataifa aliye kiongozi mtendaji wa kampuni ya Wall-mart, ambayo ni ya kwanza kwa ukubwa katika uuzaji bidhaa wa rejareja duniani, Bw. John B Menzer alisema,

"Hivi sasa tumekuwa na matawi 46 yenye wafanyakazi elfu 25 tangu tulipoanzisha tawi la kwanza la kampuni yetu nchini China miaka 9 iliyopita. Soko la biashara ya rejareja nchini China limeendelezwa haraka sana katika kipindi cha sasa, mwaka huu tunatarajia kufungua matawi 12 hadi 15 nchini China."

Kama ilivyo kwa kampuni ya Wall-mart, makampuni mengine ya kimataifa pia yamekuwa na ushirikiano na China kwa miaka mingi, yanaona kuwa maendeleo ya China yanatokana na dunia, maendeleo ya dunia pia yanaihitaji China."

Machoni pa viongozi wa seta ya biashara duniani, China imekuwa moja ya soko linalokua haraka na lenye kivutio kikubwa duniani. Ni kweli kuwa China imekuwa nchi ya kwanza kwa ukubwa duniani katika matumizi ya televisheni, majokofu na simu za mkononi, ni ya tatu katika matumizi ya magari, hivi sasa China imejenga mfumo wa kwanza kwa ukubwa duniani wa simu za mezani, mtandao wa mawasiliano ya simu za mkononi na wa pili kwa Internet ya umma. Hivi sasa uhimizaji wa uchumi wa China wenye maendeleo ya kasi kwa maendeleo ya uchumi wa dunia ni dhahiri. Waziri wa biashara wa China Bw. Bo Xilai kwenye kongamano alisema,

"Hivi sasa China inafanya kazi muhimu ya kuhimiza ongezeko la uchumi wa dunia. Mwaka jana China, ambayo pato lake linachukua 4% la pato la dunia, ilitoa mchango wa 10% kwa ongezeko la uchumi wa dunia; na ilitoa mchango wa 12% kwa ongezeko la biashara ya kimataifa ambapo thamani ya biashara ya nje ya China inachukua 6% ya dunia."

Viongozi wa sekta ya biashara duniani walioshiriki kwenye kongamano la mwaka huu walisema kuwa ushirikiano kati ya China na kampuni za aina mbalimbali duniani utapanuliwa zaidi na maendeleo ya amani ya China hayataweza kutishia nchi nyingine.

Idhaa ya kiswahili 2005-05-31