Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-05-31 15:54:34    
Wasikilizaji washindi

cri

Tunapenda kuwaambia wasikilizaji wetu kuhusu matokeo ya shindano la chemsha bongo kuhusu ujuzi wa miaka 55 ya China mpya.

Bwana Xavier L Telly Wambwa wa sanduku la posta 2278, Bungoma Kenya amepata tuzo maalum katika shindano hilo, ambaye amealikwa kuja a kuitembelea China.

Bwana Ras Fraz Manko Ngogo wa sanduku la posta 71, Tarime Mara Tanzania amepata nafasi ya kwanza, tutamtumia kadi ya ushindi, na zawadi ndogo ambayo tumemwomba Bwana Wambwa aichukue na kumpelekea.

Na waliopata nafasi ya pili ni wasikilizaji watatu kama wafuatao:

Bwana Kaziro Dutwa wa sanduku la posta 209 Songea Ruvuma Tanzania, Bwana Mbarouk Msabah Mbarouk wa sanduku la posta 52483, Dubai, United Arab Emirates na Bwana Mogire O.Machuki wa Nyankware Village sanduku la posta 646, Kisii Kenya.

Waliopata nafasi ya tatu ni wasikilizaji 6 kama wafuatao:

Bwana Epafara S. Deteba wa sanduku la posta 79912, Dar es Salaam, Tanzania, Bwana Adison Jn. Gamba ambaye barua zake huhifadhiwa na Eunice Chankaga sanduku la posta 1256, Arusha Tanzania, Bwana Daniel Chacha wa sanduku la posta 156, Tarime Mara Tanzania, Bwana Gulam haji Karim wa sanduku la posta 97, Zanzibar Tanzania, Bwana Stephen Magoye Kumalija wa Kiliwi Primary school sanduku la posta 1421, Mwanza Tanzania, na Bibi Happynes Julius ambaye barua zake huhifadhiwa na Mwalimu Mlemwa wa shule ya msingi Naura sanduku la posta 1340, Arusha Tanzania.

Tunapenda kuwaarifu kuwa hivi karibuni tutawatumia kadi za ushindi na zawadi nyingi ndogo ndogo.

Na msikilizaji wetu Xavier L Telly Wambwa aliyepata ushindi alialikwa kuja Beijing, ambapo alikuwa mgeni wa Radio China kimataifa, alitembelea sehemu mbalimbali hapa Beijing, na kwenda Xian kutembelea maonesho ya sanamu za askari na farasi wa Mfalme wa zamani Qingshihuang, tarehe 26 ameondoka Beijing na kurudi nyumbani Kenya. Kabla ya kuondoka kwake tulizungumza naye na alitueleza jinsi alivyoiona safari yake ya hapa China. ( Tafadhali msome habari halisi kutoka kwa " Bw. Telly Wambwa aliyekuwa Beijing" )

Idhaa ya kiswahili 2005-05-31