Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-01 14:47:09    
Tripoli- Mahakama kuu ya Libya yaahirisha kutangaza hukumu ya kesi kuhusu wageni kusambaza virusi vya ukimwi

cri

    Mahakama kuu ya Libya tarehe 31 ilifanya uamuzi kuahirisha kutangaza matokeo ya hukumu ya kesi kuhusu wageni kusambaza virusi vya ukimwi, ambayo yalipangwa kutangazwa siku hiyo.

    Jaji wa mahakama kuu Bw. Ali Arushi siku hiyo alitangaza kuwa, uamuzi huo wa mahakama kuu ulifanyika baada ya rais Georgi Parvanov wa Bulgaria kufanya ziara nchini Libya. Rais Parvanov alikutana na rais Mouammer Gaddafi wa Libya, na kujadiliana naye suala kuhusu wauguzi 5 wa Bulgaria kuhukumiwa adhabu ya kifo na mahakama ya Libya.

    Wachambuzi waliona kuwa, mahakama ya Libya imeahirisha kutangaza hukumu hiyo kutokana na ziara ya rais wa Bulgaria, vile vile inaweka mazingira ya kutatua suala hilo nje ya mahakama.

    Idara ya kuendesha mashtaka ya Libya mwaka 1998 iliwashtaki wauguzi 5 wa Bulgaria na daktari mmoja wa Palestina kuwapiga sindano zenye virusi vya ukimwi watoto 426 na wanawake 19 kwa kufanya majaribio, na kusababisha vifo vya watoto 48.

    Vyombo vya habari huko vilisema kuwa, watu hao 6 wote wamekana mashtaka hayo, lakini mahakama ya Bankasi mwezi Mei mwaka 2004 viliwahukumia watu hao 6 adhabu ya kifo.