Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-01 20:44:51    
Kupika nyama ya ng'ombe pamoja na asparaga

cri

Mahitaji

Nyama ya ng'ombe gramu 200, asparaga gramu 150, mvinyo wa kupikia gramu 20, kiasi kidogo cha sukari, chumvi, mchuzi wa sosi, M.S.G, unga la hamira, pilipili manga, maji ya wanga, vipande vya vitunguu maji, na tangawizi, mafuta gramu 500.

Njia

1. nyama ya ng'ombe uikate iwe vipande uiweke ndani ya bakuli moja, tia unga la hamira, mchuzi wa sosi, pilipili manga, maji ya wanga, vipande vya tangawizi na kiasi kidogo cha maji, korogakoroga halafu mimina mafuta koroga mpaka zichanganyike sawa. Kata asparaga iwe vipande.

2. tia mafuta ndani ya sufuria pasha moto mpaka iwe nyuzi ya asilimia 60, tia vipande vya nyama ya ng'ombe koroga mpaka viwe rangi ya mweupe vipakue na ondoa mafuta.

3. tia mafuta kidogo ndani ya sufuria, halafu tia vipande vya vitunguu maji na tangawizi, sukari, mchuzi wa sosi, M.S.G, tia vipande vya asparaga na chumvi, korogokoroga, tia vipande vya nyama ya ng'ombe, na mimina maji ya wanga,korogakoroga. Vipakue na kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.