Kuanzia mwezi Aprili mwaka huu, Marekani na Umoja wa Ulaya zilitangaza kufanya uchunguzi wa "dhamana maalum" na hatua maalum za vizuizi kwa bidhaa za nguo za China zinazouzwa katika nchi za nje kutokana na kifungu cha 242 cha ripoti ya kikundi cha kazi cha China kujiunga na WTO, ili kuwalinda wafanyabiashara wadogo na wa kiasi wa nguo wa nchi zao. Katika hali ya Marekani na Umoja wa Ulaya kushikilia kuweka vizuizi kwa bidhaa za nguo za China baada ya China kurudi nyuma mbali, China ilitangaza kufuta hatua ya kuongeza ushuru wa forodha kwa baadhi ya bidhaa za nguo za China iliyopangwa kutekelezwa kuanzia tarehe mosi mwezi Juni. Wachambuzi wanaona kuwa kutokea kwa mgogoro katika biashara ya kimataifa ni jambo la kawaida, lakini haifai kutumia vigezo viwili na kufuata msimamo wa kujinufaisha tu.
Watu mashuhuri wa sekta ya nguo waliainisha kuwa kutokana na kanuni zinazohusika za WTO, mgogoro huo uliochochewa na Marekani na Umoja wa Ulaya una makosa mengi katika programu na uthibitisho wa madhara kwa bidhaa za nguo zilizoagizwa na Marekani na Umoja wa Ulaya.
Ili kujiunga na WTO, katika ripoti ya kikundi cha kazi cha China kujiunga na WTO, China ilitoa ahadi maalum kuhusu biashara ya bidhaa za nguo, yaani kifungu cha 242. Kutokana na kifungu hicho, kama nchi moja mwanachama ya WTO inaona kuwa bidhaa za nguo za China zimevuruga soko au kuwepo tishio kwenye soko, nchi hiyo inaweza kuitaka China zifanye majadiliano. Kuhusu jambo hilo, watu mashuhuri kadhaa wa Marekani na Umoja wa Ulaya wanaona kuwa yaliyomo kwenye kifungu cha 242 si ya haki. Hata hivyo, kifungu hicho hakiwezi kuzizuia Marekani na Umoja wa Ulaya zisifanye matata dhidi ya China katika jambo hilo.
Kutokana na makubaliano yaliyofikiwa na pande mbalimbali za WTO, kuanzia tarehe mosi mwezi Januari mwaka huu, vikwazo vya kiasi cha biashara ya bidhaa za nguo duniani vilifutwa. Jambo hilo linaonesha kuwa soko la bidhaa za nguo duniani limetimiza umoja baada ya kufanya biashara ya vikwazo kwa zaidi ya miaka 40. Jambo litalostahili kufuatiliwa ni kuwa baada miezi mitatu na zaidi tu tangu ulipoondolewa mgao wa biashara, Marekani na Umoja wa Ulaya zimeweka vizuizi kwa bidhaa za nguo za China kutokana na hesabu zisizo sahihi na zilizofanywa kwa muda mfupi.
Kuhusu jambo hilo, waziri wa biashara wa China Bw. Bo Xilai aliainisha kuwa Marekani na Umoja wa Ulaya zimetumia ovyo vifungu vya WTO kuweka vizuizi kwa bidhaa za nguo za China zinazouzwa katika nchi za nje, jambo ambalo limeharibu usawa na uhuru wa mfumo wa biashara duniani. Gazeti maalum la fedha la Ujerumani liitwalo Handelsblat lilichapisha makala likiainisha kuwa kuhusu suala la kufunguliwa kwa soko, Umoja wa Ulaya na Marekani huwa zinatangulia mbele, lakini sasa zimechukua rungu la kujilinda kibiashara katika suala kuhusu bidhaa za nguo za China, ni dhahiri kuwa hatua hiyo ni utekelezaji wa vigezo viwili.
Idhaa ya kiswahili 2005-06-02
|