Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-02 20:43:35    
Mji wa Guangzhou

cri

Mji wa Guangzhou ni mji mkuu wa mkoa wa Guangdong na ni kituo cha siasa, teknolojia na utamaduni cha mkoa huo. mji huo uko kusini mashariki mwa mkoa huo, na kaskazini mwa delta ya Mto Zhujiang. Unapakana na bahari ya kusini, Hongkong na Macao.

Urefu kutoka usawa wa bahari wa sehemu ya kaskazini mashariki ya mji huo ni mkubwa kuliko sehemu ya kusini magharibi. Sehemu za kaskazini na kaskazini mashariki ni sehemu za milima, sehemu ya kati ni sehemu ya milima midogomidogo, na sehemu ya kusini ni tambarare ya delta ya Mto Zhujiang. Hali ya hewa huko ni ya pepo za msimu ya ukanda wa nusu tropiki. Hakuna joto kali katika majira ya joto wala baridi kali katika majira ya baridi. Mvua ni nyingi, na maua yanachanua mwaka mzima.

Hivi sasa aina zaidi ya 50 za madini zimegunduliwa mjini humo. Kuna aina elfu kadhaa za mimea na wanyama pori zaidi ya aina 210.

Eneo la mito na maziwa mjini humo ni hekta elfu 74.4, ambalo linachukua asilimia 10 ya eneo lote la mji huo. Mpunga ni nafaka muhimu ambayo linavunwa mara mbili kwa mwaka. Mazao ya kiuchumi ni pamoja na mboga, matunda na maua. Mji huo unazalisha matunda kw wingi. Na pia ni maarufu kwa maua yaliyopandwa kwenye bustani na maua yaliyopandwa kwenye vyungu. Bidhaa za maua yaliyopandwa kwenye vyungu zinauzwa nchini China na Ulaya na Marekani.

Mandhari ya mji wa Guangzhou ni nzuri. Kuna vivutio makumi kadhaa vya utalii. Mlima Baiyun, Mto Zhujiang, Mlima Yuexiu, uwanja wa Dongzhan, hekalu la ukoo wa Chen na makaburi ya mashujaa ya Huanghuagang ni maarufu zaidi mjini humo.

Mji wa Guangzhou ulikuwa mji uliostawi katika Enzi za Qin na Han, na ulikuwa mwanzo wa njia ya hariri baharini tangu Enzi za Han na Tang, pia ni sehemu ya biashara na nje iliyoanzishwa mapema zaidi ambayo haikufungwa hata kwa siku moja nchini China.

Mji wa Guangzhou ni moja ya sehemu inayoanza mapema zaidi kutekeleza sera ya mageuzi na ufunguaji mlango. Baadaye mabadiliko makubwa yalitokea mjini humo. Nguvu ya ujumla ya mji huo inachukua nafasi ya tatu katika miji mikubwa kumi nchini China,

Mjini humo kuna mabaki mengi ya kale. Hivi sasa masalio ya dola la Yue ya Kusini yakiwemo mabaki ya kasri, kaburi la mfalme na mabaki ya mlango wa bwawa yameomba kuwekwa kwenye orodha ya urithi wa kihistoria na kiutamaduni duniani na Umoja wa Mataifa.

Mji wa Guangzhou ni mji maarufu kwa wakazi wa mji huo kuwa na jamaa wengi katika nchi za nje. Takwimu zimeonesha kuwa, wakazi wa mji huo wana jamaa milioni 1.06 walioko katika nchi na sehemu mbalimbali duniani.

Idhaa ya Kiswahili 2005-06-02