Mameya wa miji zaidi ya 60 duniani wanakusanyika mjini San Francisco, Marekani kuanzia tarehe mosi mwezi Juni kushiriki shughuli za kuadhimisha siku ya mazingira duniani zinazofanywa na Umoja wa Mataifa. Katika shughuli za siku tano, mameya hao watabadilishana maoni kwa undani kuhusu suala la maendeleo ya miji na hifadhi ya mazingira na kusaini azimio la miji ya kijani linalohusiana na hifadhi ya mazingira.
Tarehe 5 mwezi Juni mwaka huu ni siku ya 32 ya mazingira duniani ya Umoja wa Mataifa. Kutokana na takwimu zilizotolewa na shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa, hivi sasa zaidi ya nusu ya watu duniani wanaishi mijini. Matumizi ya rasilmali ya watu wa mijini yanachukua asilimia 75 ya matumizi hayo yote duniani na asilimia 75 ya takataka duniani pia zinatoka mijini. Kadiri mchakato wa uendelezaji wa miji unavyoharakishwa katika nchi mbalimbali, ndivyo hali hiyo itakavyozidi kudumu, basi dunia inayotegemewa na binadamu katika maisha itakabiliwa na changamoto ya hifadhi ya mazingira na viumbe ambazo hazijawahi kuokea. Kwa hiyo, Umoja wa Mataifa unaweka kaulimbiu ya siku ya mazingira ya mwaka huu kuwa kujenga miji ya kijani na kuhifadhi dunia.
Katika siku ya kuanzisha shughuli za kuadhimisha siku ya mazingira duniani, mkurugenzi mtendaji wa shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa Bw. Klaus Toepfer alitoa hotuba akizitaka nchi zilizoendelea ziweke mfano wa kuhimiza maendeleo endelevu mijini na nchi zinazoendelea pia zingeiga uzoefu kutoka kwa nchi zilizoendelea na kuepuka kufuata nyayo za makosa ili kuhimiza kwa pamoja maendeleo endelevu ya miji.
Tangu mwaka 1972, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipopitisha azimio la kuweka siku ya mazingira duniani, huu ni mwaka wa kwanza kwa Umoja wa Mataifa kufanya shughuli za siku ya mazingira duniani katika mji wa Marekani. Umoja wa Mataifa kuchagua San Francisco kufanya shughuli hizo kuna maana mbili.
Kwanza, Umoja wa Mataifa ulizaliwa mjini San Francisco miaka 60 iliyopita. Wajumbe kutoka nchi 50 walikutana mjini humo kuitisha mkutano kuhusu jumuiya ya kimataifa ya Umoja wa Kimataifa na kusaini katiba ya Umoja wa Mataifa tarehe 26, mwezi Juni mwaka 1945. Katiba hiyo ilianza kufanya kazi baada ya miezi minne baadaye Umoja wa Mataifa ulitangaza kuanzishwa.
Pili, mji wa San Francisco umepata mafanikio makubwa katika hifadhi ya mazingira. Gavana wa jimbo la Califonia la San Francisco ambaye alikuwa mchezaji nyota wa filamu duniani Bw. Arnold Schwarzenegger pia alifuatilia juhudi za hifadhi ya mazingira na kupendekeza mpango wa barabara kasi ambazo magari yanatumia hydrogen na kutangulia kutumia magari ya kuchukua umeme unaozalishwa kwa nguvu za hydrogen uwe nishati badala ya mafuta.
Bila shaka, safari hii kufanya shughuli za kuadhimisha siku ya mazingira duniani mjini San Francisco, Umoja wa Mataifa unatumai kuwa mwito wa gavana Schwatzenegger utakuwa na mvuto wake, tena ubora wa sayansi na teknolojia wa Marekani utasaidia kuendeleza teknolojia ya hifadhi ya mazingira katika nchi mbalimbali duniani.
|