Kutokana na makubaliano ya viongozi wa Palestina na Israel kwenye mkutano uliofanyika mwezi Februari mwaka huu mjini Sharm el-Sheikh, Misri, tarehe pili Juni wafungwa 398 wa Palestina waliachiwa huru. Katika siku iliyotangulia ofisi ya waziri mkuu wa Israel ilitangaza kuwa waziri mkuu wa Israel Bw. Sharon na mwenyekiti wa mamlaka ya utawala wa Palestina Bw. Abbas watakutana kwa mara ya pili tarehe 21 Juni. Mambo hayo yamevunja hali kukwama katika kipindi kilichopita na kufanya uhusiano wa pande mbili iwe na uhai mpya.
Mwezi Februari Bw. Sharon na Abbas walikubaliana kuhusu kumaliza mgogoro wa kijeshi uliodumu kwa zaidi ya miaka minne katika mji wa Sharm el-Sheikh, uhusiano kati ya pande mbili ulikuwa umeingia katika kipindi cha uchangamfu, vikundi vyenye siasa kali vya Palestina na jeshi la ulinzi la Israel kwa muda waliacha kufyatuliana risasi na wafungwa 500 wa Palestina waliofungwa na Israel waliachiwa huru, miji miwili kwenye ukingo wa magharibi wa Mto Jorden ilirudishwa tena mikononi mwa kikosi cha usalama cha Palestina na mageuzi ya kisiasa na kiusalama yaliyodaiwa na Israel kwa muda mrefu pia yalianza kufanyika nchini Palestina. Lakini kadiri muda ulivyopita hali hiyo ya utulivu ilivunjika kutokana na migogoro iliyotokea mara moja moja na pande mbili zilianza kushutumiana. Upande wa Israel ulisimamisha kipindi cha pili cha kuwachia huru wafungwa wa Palestina na mpango wake wa kuikabidhi miji miwili ya magharibi ya Mto Jorden kwa Palestina, ushirikiano wa kiusalama pia ulisimama bila kuendelea. Watu wa Palestina walianza kuwa na mashaka kuhusu sera za Abbas za mazungumzo ya amani.
Utulivu wa uhusiano kati ya Palestina na Israel bila usipoendelea ni madhara kwa pande mbili, hasa kwa Palestina. Heshima ya Abbas katika mambo ya siasa ilitiwa mashaka na hali ya siasa nchini Palestina ilikuwa na wasiwasi. Chama cha Hamas hivi karibuni kimekuwa na ushawishi mkubwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa, hali ambayo ni tishio kubwa kwa chama cha Fatah kinachoongozwa na Abbas. Kwa makadirio, Hamas pengine itapata 30% ya viti katika kamati ya kutunga sheria ya Palestina.
Kuimarika kwa Hamas sio tu ni tishio kwa mamlaka ya Abbas bali pia kutaathiri sera za Palestina kwa Israel, na hali ya usalama nchini Palestina pia itabadilika kuwa mbaya. Abbas anayeungwa mkono na Marekani na ni mtu muhimu katika mchakato wa amani ya Mashariki ya Kati, kwa hiyo kuendelea na sera zake ni muhimu sana. Kama Hamas inayopinga Marekani na yenye imani kali ya kidini ikishika uongozi wa kisiasa nchini Palestina itavuruga sera za Marekani kuhusu Palestina na Israel, na pia itakuwa ni pigo kubwa kwa mpango wa kidemokrasia wa Mashariki ya Kati. Kwa hiyo kumwunga mkono Bw. Abbas ni sera muhimu ya Marekani kwa Palestina. Ili kulinda heshima ya Abbas, Israel lazima irudi nyuma ili Palestina ipate matunda yanayotumainiwa na watu wa Palestina, kama vile kuwaachia huru wafungwa wengi zaidi wa Palestina, kukabidhi miji kwa Palestina na kulegeza masharti kwa safari ya Palestina na kuboresha mazingira ya maisha ya watu wa Palestina. Ni kwa kufanya hivyo tu ndivyo Abbas anaweza kuwa na heshima kubwa zaidi ya kisiasa na kuungwa mkono na Wapalestina.
Kwa upande wa Sharon, mpango wa upande mmoja umefika wakati wa kutekelezwa, usalama wa kuondoka kutoka Gaza kunahitaji ushirikiano wa Palestina, na kutekeleza mpango wa upande mmoja pia hakuwezi kutengana na ushirikiano wa upande wa Palestina.
Kutokana na sababu hizo zilizotajwa hapo juu, uhusiano wa pande mbili umeanza kuwa mzuri katika siku za karibuni. Lakini hata hivyo pande hizo mbili bado ziko katika kipindi cha kujenga uaminifu, na pande mbili zikitaka kutoka kwenye hali ngumu, pia zinahitaji kufanya juhudi kubwa.
Idhaa ya kiswahili 2005-06-03
|