Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-03 20:48:18    
Vyombo vya shaba nyeusi vya kale

cri

Katika mkoa wa Yunnan kuligunduliwa vyombo vingi vya shaba nyeusi vyenye ubora wa juu wa kisanaa. Vyombo hivyo vilidhihirisha maendeleo ya kila upande ya makabila ya kale ya Yunnan katika siasa, uchumi, mambo ya kijeshi, utamaduni na dini.

Silaha na vyombo vya kuhifadhia pesa ni vingi kuliko aina nyingine zote za vyombo vya shaba nyeusi vilivyogunduliwa huko. Licha ya vitu hivyo pia kuligunduliwa zana za kilimo, vitu vya matumizi ya kila siku, ala za muziki na mapambo ya shaba nyeusi.

Vyombo vya shaba nyeusi vya Yunnan vina mtindo maalumu kama ifuatayo: kwanza, juu ya vyombo hivyo kwa kawaida kulichongwa nakshi za binadamu wenye maumbo tofauti waliokuwa wakifanya vitendo mbalimbali kama kuabudu mungu, kupigana vita, kulima, kufuma nguo, kufuga mifugo, kuwinda wanyama, na kucheza ngoma. Pili, wachongaji walipochonga nakshi hizo, walifuata kwa makini ukubwa na uwiano wa watu wenyewe. Tatu, kutokana na hadithi mfululizo, wasanii walichagua sehemu za mwishoni kidogo za hadithi, ili watu waweze kuzifahamu zaidi hadithi zenyewe. Kwa mfano, wakati wa kuwinda wanyama wasanii walionyesha zaidi hali ya farasi ya kukimbia kwa haraka, huku mkono mmoja wa mwindaji ukiwa umeshika mjeledi, na mwingine ukiwa umeshika mkuki.

Ufuaji wa vyombo vya shaba nyeusi wa Yunnan ulifikia kiwango cha juu wakati wa kipindi cha Zhanguo na cha Enzi ya Han ya Magharibi. Ufundi wa utengenezaji wa vyombo pia ulikuwa ni wa mtindo maalumu. Kwa mfano ufundi wa kufua uliweza kutoa vyombo vingi vyenye maki nyembamba. Ili kuzidisha uzuri wa vyombo vya shaba nyeusi mafundi walitumia sana ufundi mpya wa kupaka dhahabu.

Idhaa ya Kiswahili 2005-06-03