Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-06 14:42:34    
Historia ya UKIMWI (3)

cri

Januari mwaka 1987, waziri wa huduma za jamii wa Marekani alipozuru San Francisco aliwahi kupeana mkono hadharani na mgonjwa wa UKIMWI. Kitendo hicho kingetokea hivi sasa kisingeshitusha, lakini wakati huo kitendo hicho cha ofisa huyo mwandamizi kilikuwa kimedhihirisha nini msimamo wa serikali ya Marekani kuhusu wagonjwa wa UKIMWI na kuwaonesha watu.

Uingereza ni moja ya nchi zilizotangulia kufanya harakati za kueneza ujuzi kuhusu UKIMWI. Mwaka 1986 serikali ya Uingereza ilichapisha matangazo mengi kuhusu kinga na tiba ya UKIMWI katika magazeti. Mwaka 1987 Uingereza kwa mara nyingine tena ulifanya harakati za uenezi wa kinga na tiba ya UKIMWI, na licha ya magazeti, vituo vya redio na televisheni pia vilishiriki katika harakati hizo. Nchini Uingereza kila familia ilipewa karatasi kuhusu UKIMWI. Mke wa mwanamfalme Diana wa Uingereza alipozuru wodi za wagonjwa wa UKIMWI alipeana mikono na wagonjwa bila glovu. Kitendo hicho kilitangazwa sana na vyombo vya habari na kwa kiasi fulani kiliwaondolea hofu watu wengi.

Kinyume na Uingereza, serikali ya Marekani ilikosolewa. Mwezi Juni mwaka 1987 kwenye mkutano wa tatu wa kimataifa uliofanyika Washington, rais George Bush alipozungumzia sera kuhusu UKIMWI alizomewa. Kupitia matangazo ya televisheni, watu wote duniani walishuhudia askari polisi waliovaa glovu ndefu wakiwakamata waandamanaji waliopinga sera ya Marekani kuhusu UKIMWI. Watu walisema, habari hiyo ilizidi kuwaogopesha watu UKIMWI.

Kutokana na hofu watu wanajihadhari sana na UKIMWI. Na kutokana na kuenea haraka kwa UKIMWI, watu walizidi kuwanyenyepaa wagonjwa hao. Watoto watatu wa familia moja katika jimbo la Florida, kusini mashariki mwa Marekani, walikuwa na virusi vya UKIMWI kutokana na kuchangia damu. Kwa sababu walikataliwa kusoma shuleni walihamia jimbo jingine, lakini pia walibaguliwa, isitoshe tishio na ghasia zisizo na mwisho ziliifanya familia hiyo isiweze kupata utulivu. Mwishowe nyumba zao zilimwagiwa petroli na na kuchomwa moto.

Mwezi Mei mwaka 1987, mkutano wa WHO ulipitisha mkakati wa mapambano dhidi ya UKIMWI, na kutoa lengo la udhibiti wa UKIMWI kwa nchi zote na ulitaka nchi zote zifanye juhudi kujenga jamii ya kuwasaidia wagonjwa bila unyenyepaa. Mwezi Oktoba mwaka huo kongamano kuhusu UKIMWI lilifanyika katika Umoja wa Mataifa kwa mara ya kwanza, na lilitaka vyombo vyote vya umoja huo vianze mapambano duniani dhidi ya UKIMWI chini ya uongozi wa WHO.

Mwishoni mwa mwaka huo wagonjwa wa UKIMWI duniani walifikia 71,751. Marekani iliongoza duniani kwa kuwa na wagonjwa 47,022, na nchi nyingine zilizozidi wagonjwa 2,000 zilikuwa ni Ufaransa, Uganda na Brazil; zilizozidi 1,000 zilikuwa ni Tanzania, Ujerumani, Canada, Uingereza na Italia.

Mwaka huo, 1987, mgogoro wa hataza kuhusu ugunduzi wa virusi vya UKIMWI kati ya Ufaransa na Marekani uliisha. Pande mbili zilipatana kufaidika pamoja kutokana na hataza za ugunduzi wa virusi. Lakini watu wengi wanaona kuwa kabla ya Marekani kupata virusi vya UKIMWI, Ufaransa ulikuwa umekwisha vipata mapema kwa mwaka mmoja.

Mwaka 1988 dunia nzima iliamka kupambana na UKIMWI, wajumbe kutoka nchi 148 walishiriki kwenye mkutano uliofanyika mjini London kujadili suala la UKIMWI. "Taarifa ya London" iliyotolewa baada ya mkutano ilisisitiza kueneza elimu ya UKIMWI na kuimarisha mawasiliano ya uzoefu na kulinda heshima ya wagonjwa na wenye virusi vya UKIMWI.

Kutokana na shinikizo kutoka pande mbalimbali serikali ya Marekani pia ilianzisha harakati za kueneza ujuzi kuhusu UKIMWI na ilichapisha kijitabu kimoja kiitwacho "Fahamu UKIMWI" na kilisambazwa kote nchini Marekani kwa nakala milioni 107.

Tarehe mosi Desemba, mwaka 1988, "siku ya UKIMWI duniani" kwa mara ya kwanza iliadhimishwa kote duniani kwa kauli mbiu ya "Dunia nzima ifanye juhudi".

Idhaa ya kiswahili 2005-06-06