Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-06 20:37:07    
China yatoa muswada wa maelekezo wa kuingilia vitendo vyenye hatari vya watu walioambukizwa virusi vya Ukimwi

cri

Wizara ya afya ya China tarehe 6 hapa Beijing imetoa "muswada wa maelekezo wa kuingilia vitendo vyenye hatari" unaowalenga watu walioambukizwa virusi vya Ukimwi. Muswada huo umewafanya watu walioambukizwa virusi vya Ukimwi na magonjwa mengine ya zinaa kuwa watu watakaoingiliwa vitendo vyao.

Muswada huo unazitaka idara husika za sehemu mbalimabli kuchukua hatua husika za uingiliaji kutokana na umaalum wa kuenea kwa watu hao waliolengwa, na kuweka mkazo katika kudhibiti ugonjwa wa Ukimwi usiambukizwe kwa njia ya ngono. Imefahamika kuwa, hatua za uingiliaji ni pamoja na upashanaji habari, kuhimiza matumizi ya kondom, na kuratibu huduma za matibabu ya magonjwa ya zinaa.