Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-07 16:48:40    
Mahakama maalum ya Iraq itamhukumu Saddam ndani ya miezi miwili ijayo

cri
    Mahakama maalum ya Iraq inayoshughulikia hukumu ya rais wa zamani wa Iraq Saddam tarehe 6 ilitangaza kuwa, mahakama yake itamhukumu Saddam ndani ya miezi miwili ijayo, na mashitaka kwake ni pamoja na kuwaua wakurd, kutoa hukumu za vifo kwa wakuu wa dini, kuwaua raia kwa kutumia silaha za kemikali, na kuivamia Kuwait.

    Habari kutoka shirika la habari la AP tarehe 6 zilisema kuwa, mahakama maalum ya Iraq inatoa mashitaka kwa Saddam kutokana na makosa 14 yakiwemo: Mwaka 1982, aliwaua wairaq wasiopungua 50, huko Dujail, kijiji cha madhehebu ya Shia kilichoko umbali wa kilomita 80 kutoka kaskazini ya Baghdad, ili kulipiza kisasi kwa shambulizi lisiloshinda dhidi ya magari ya Saddam lililotokea kwenye kijiji hicho; Mwaka 1983, kuwaua na kuwafukuza wakurd 8000 wa kabila la Barzani; Mwaka 1988, kushambulia Halabja, kijiji cha Kurd kwa kutumia silaha za kikemikali, na kusababisha vifo vya watu 5000; Wakati Saddam alipokuwa madarakani, aliwaua wanasiasa maarufu; Mwaka 1990, kutoa amri ya kuivamia Kuwait, na kuikalia Kuwait kwa miezi 7; Mwaka 1991, kukandamiza upinzani wa waislamu wa madhehebu ya Shia yaliyoko kusini mwa Iraq.

    Kabla ya hapo, msemaji wa serikali ya mpito ya Iraq Bw. Laith Kuba alisema kuwa, ingawa Saddam anakabiliwa na shutuma 500, lakini ni kupoteza wakati kutoa mashtaka kwa shutuma zote, hivyo mahakama itatoa mashtaka kutokana na makosa 12 yaliyothibitishwa. Makosa hayo 12 yanatosha kumhukumu Saddam. Bw. Kuba alisema kuwa, Saddam atahukumiwa ndani ya miezi miwili, lakini hakudokeza tarehe halisi ya hukumu yake.

    Wachambuzi wanaeleza kuwa, serikali ya Iraq inataka kumhukumu Saddam mapema, ili kupinga nguvu ya jeshi la Iraq linalopinga Marekani, na kusaidia kuboresha hali ya usalama ya Iraq. Kwa mujibu wa takwimu, watu 850 wameuawa kwenye mashambulizi tangu serikali ya mpito ya Iraq ianzishwe tarehe 28, Aprili. Ingawa majeshi ya Marekani nchini Iraq na serikali ya Iraq zilichukua vitendo ya kijeshi kupambana na mashambulizi hayo, lakini hayakupata matoeko mazuri. Tarehe 6, Polisi ya Iraq ilithibitisha kuwa, tarehe 5, na 6, wairaq 6 waliuawa huko Mosul, mji wa kaskazini ya Iraq, akiwemo askari polisi moja na watoto wawili. Jeshi la Marekani tarehe 6 lilitangaza kuwa, magari ya jeshi la Marekani yalishambuliwa tarehe 5 huko Kirkuk, na askari mmoja wa jeshi la Marekani aliuawa. Tangu vita vya Iraq ianzishwe, askari wa jeshi la Marekani waliouawa nchini Iraq wamefikia 1669.

    Serikali ya Iraq inaona kuwa, wafuasi wa Saddam na watu kadhaa wenye siasa kali wa madhehebu ya Suni wanapaswa kuwajibika na mashambulizi ya kigaidi ya kuipinga serikali ya Marekani. Watu hao wenye silaha wanajaribu kupinga serikali mpya ambayo waumini wa madhehebu ya Shia wanashika hadhi ya uongozi. Ndiyo maana, zinapaswa kuchukuliwa hatua za kisiasa kupambana na jeshi la kuipinga serikali ya Marekani. Waziri wa mambo ya nje wa Iraq Bw. Hoshyar Zebari alieleza kuwa, anaamini kuwa kumhukumu Saddam kutasaidia kuzuia nguvu za watu wenye silaha.

    Pili, waislamu wa madhehebu ya Shia na wakurd wanataka kumwadhibu vibaya Saddam kutokana na kukandamizwa vibaya wakati wa utawala wa Saddam kwa zaidi ya miaka 30. Rais wa serikali ya mpito ya Iraq ambaye pia ni kiongozi wa kundi la waKurd Bw. Jalal Talabani ni mpinzani mkubwa wa Saddam. Waziri mkuu wa Iraq ambaye pia ni kiongozi wa madhehebu ya Shia Bw. Ibrahim al-Jaafari aliwahi kukimbilia katika nchi za nje kutokana na shinikizo la utawala wa Saddam. Tarehe 17, Mei, kiongozi wa madhehebu ya Shia yenye siasa kali Bw. Moqtada al-Sadr alidai mara nyingine tena Saddam aadhibiwe vikali, na watu wengi wa madhehebu ya Shia na Kurd wanataka Saddam ahukumiwe kifo.

    Aidha, kutokana na mtazamo wa serikali ya mpito, kumhukumu Saddam kunasaidia kuzidi kuboresha uhusiano kati yake na nchi jirani hususan Kuwait, ili kutoa mazingira mazuri ya nje kwa mchakato wa ukarabati wa kisiasa na kiuchumi wa Iraq.

Idhaa ya Kiswahili 2005-06-07