Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-07 15:49:15    
Maendeleo endelevu ya nishati nchini China

cri

Baraza kuhusu mazingira bora na hifadhi ya maliasili lilifanyika tarehe 8 mjini Beijing. Mkurugenzi wa Kamati ya Mazingira na Hifadhi ya Maliasili katika Bunge la Umma la China Bw. Mao Rubo kwenye baraza hilo alisema kuwa maendeleo endelevu ya nishati nchini China lazima yafuate njia ya kubana matumizi na nishati iwe ya aina nyingi badala ya aina moja na hifadhi ya mazingira ipewe kipaumbele.

Bw. Mao Rubo alisema, "katika miaka 15 ijayo matumizi ya nishati nchini China yataendelea kuongezeka, kwa makadirio mwaka 2020 matumizi ya makaa ya mawe yatafikia tani bilioni 2.5 hadi 3.3." Kama tukiwa na mkakati mwafaka ongezeko hilo litapungua. Hii inamaanisha kuwa China itatumia nishati chache na kasi ya maendeleo ya uchumi itaendelea bila kupungua.

Imefahamika kuwa nishati ya makaa ya mawe nchini China ni kubwa, lakini uchimbaji wake uko nyuma kuliko mahitaji. Na 86% ya makaa ya mawe ambayo hayajachimbwa yako katika sehemu ya magharibi, mbali na sehemu ya kuyatumia, sehemu ambayo ina upungufu wa maji na ardhi ni kavu. Kwa hiyo kazi ya kuchimba na kusafirisha ni ngumu. Hii inamaanisha kuwa katika kipindi kijacho hali ya huduma za makaa ya mawe na mahitaji yake itakuwa ngumu.

Zaidi ya hayo Bw. Mao alisema, matumizi ya nishati katika ujenzi, mawasiliano na uchukuzi pia ni makubwa. Hivi sasa nishati inayotumika katika ujenzi inachukua 35% ya matumizi yote ya nishati katika jamii, na 99% ya majengo ni majengo yanayotumia nishati kubwa. Matumizi ya nishati katika mawasiliano na uchukuzi pia ni makubwa, kwa wastani wa matumizi ya sasa, hadi kufikia mwaka 2020 matumizi ya mafuta ya magari yatafikia tani milioni 176 ambayo ni sawa na mafuta asilia tani milioni 320. Matumizi hayo ni makubwa sana.

Aidha, utoaji hewa chafu umeathiri usalama wa mazingira, maendeleo endelevu yanakabiliana na shinikizo kubwa. Hivi sasa nishati yetu muhimu ni makaa ya mawe ambayo yanaleta uchafuzi mkubwa wa mazingira.

Bw. Mao anaona kuwa kutokana na shinikizo hilo kubwa, China inapaswa kuchukua mkakati wa kubana matumizi ya nishati, na nishati isiwe ya moja na hifadhi ya mazingira ipewe kipaumbele. Kitu kinachotiliwa mkazo ni kuokoa nishati yaani kuhakikisha uzalishaji mkubwa kwa kutumia nishati ndogo, hii lazima iwe njia ya kudumu katika maendeleo ya uchumi. Matumizi madogo katika ujenzi, mawasiliano na uchukuzi yawekwe katika nafasi muhimu na kuwekewa kigezo cha matumizi ya nishati, vifaa vya ujenzi viwe vya kuokoa nishati kwa kutumia teknolojia mpya, na kuharakisha ugunduzi wa nishati ya aina mpya inayoweza kutumika tena. Matumizi madogo ya nishati ya vyombo vya usafiri vya umma lazima yazingatiwe na kuendeleza vyombo vinavyotumia nishati isiyo ya uchafuzi na kupunguza utegemezi kwa nishati ya jadi.

Miundo ya nishati lazima iboreshwe, na kuongeza kiasi cha nishati inayoweza kutumika tena, licha ya kuongeza huduma za mafuta na gesi pia matumizi ya umeme wa nyuklia na umeme wa mafuta yaongezwe.

Usimamizi wa nishati na mazingira lazima uimarishwe. Katika matumizi ya nishati, kwanza lazima usafi wa mazingira uzingatiwe na kupunguza uchafuzi wa mazingira ili kuhakikisha utoaji uchafuzi unadhibitiwa. Majengo yoyote ya uzalishaji nishati lazima yapimiwe athari ya uchafuzi kabla ya kujengwa na zana za kuzuia uchafuzi lazima ziwe tayari.

Idhaa ya kiswahili 2005-06-07