Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-07 16:57:00    
Kampuni ya LG-PHILIPS ya mpambazuko yawania nafasi ya kwanza nchini China

cri

Pamoja na maendeleo ya kasi ya uchumi wa China na kuzidi kufungua mlango, makampuni mengi maarufu ya kimataifa yanaingia China kwa njia za ubia na uwekezaji. Kampuni ya LG-PHILIPS ya Mpambazuko iliyoko Changsha, mji mkuu wa mkoa wa Hunan ni kampuni ya ubia kati ya China na nchi ya nje. Katika muda wa miaka michache tu kampuni hiyo imepiga hatua kubwa za maendeleo na kupata faida kubwa. Hivi sasa kampuni hiyo inajitahidi kupanua uzalishaji wa vioo vya televisheni(kinescope), ns kuwania nafasi ya kuongoza nchini China.

Kabla ya kuanzishwa kwa kampuni ya LG-PHILIPS ya Mpambazuko, kampuni hiyo ilijulikana kwa jina la kampuni ya mpambazuko ya LG, ambayo ilianzishwa mwaka 1994 kwa ubia kati ya China na Korea ya Kusini kwa kujenga kiwanda cha vioo vya televisheni za rangi kilichogharimu dola za kimarekani zaidi ya milioni 600. Kutokana na kuungana kwa sehemu za uzalishaji wa vioo vya televisheni za rangi za kampuni mbili za LG na PHILIPS miaka minne iliyopita, kampuni ya LG ya Mpambazuko ikiwa ni tawi moja chini yake, Kampuni ya LG ya Mpambazuko ikabadilishwa jina kuwa kampuni ya LG-PHILIPS ya Mpambazuko.

Katika muda wa miaka 9 tangu kuanzishwa kwa Kampuni ya LG-PHILIPS ya Mpambazuko mwaka 1996, kampuni hiyo imepata maendeleo makubwa ya kushangaza. Naibu meneja mkuu wa kampuni hiyo bibi Li Tongqiu alieleza mabadiliko makubwa ya kampuni hiyo akisema,

"Tangu kuanzishwa kwake mwaka 1996 hadi hivi sasa kampuni yetu imezalisha vioo vya televisheni za rangi milioni 45.1, hivi sasa uwezo wa uzalishaji wa kampuni yetu umefikia vioo elfu 32 kwa siku ukilinganishwa na vioo elfu 4 tu kwa siku wa hapo mwanzo. Licha ya hayo, mwaka 1996 tulikuwa na mstari mmoja tu wa uzalishaji, ambao ulizalisha vioo vya aina mbili tu, tofauti na sasa ambapo tumekuwa na mistari mitano ya uzalishaji inayoweza kuzalisha aina 15 za vioo."

Bibi Li Tongqiu alisema kuwa idadi ya vioo vya televisheni za rangi vilivyozalishwa na kiwanda cha kampuni hiyo mwaka jana ilizidi milioni 11 ikilinganishwa na pungufu ya laki 6 tu katika mwaka wa kwanza baada ya kuanzishwa kampuni hiyo.

Kampuni ya LG ya Korea ya Kusini ni kampuni ya kimataifa, ambayo ilianzishwa miaka zaidi ya 50 iliyopita na pato lake la hivi sasa limezidi dola za kimarekani bilioni 70 kwa mwaka. Jambo linalovutia ni kuwa kampuni ya LG ilipotafuta mshiriki wake nchini China haikutupia macho yake kwenye mikoa ya pwani ya mashariki ya China, ambayo imeendelea zaidi kiuchumi nchini China, bali ilitupia macho katika mkoa wa Hunan, sehemu ya kati ya China. Kuhusu suala hilo, meneja mkuu wa kampuni hiyo Bw. Quan Xiangyun alisema kuwa kampuni ya LG ilifanya uamuzi huo baada ya kufanya uchunguzi kwa pande mbalimbali nchini China.

"Kulikuwa na watu waliosema kuwa sababu muhimu kwa kampuni ya LG kuchagua Hunan ni kutokana na gharama ndogo ya nguvukazi, hali halisi ni kuwa hiyo ni moja ya sababu za chaguo letu. Mwaka 1994, kampuni na viwanda vilikuwa vimeanzishwa na kujengwa kwa wingi kwenye mikoa ya sehemu ya pwani ya mashariki ya China, ambapo gharama za kuingia kwenye sehemu hiyo kwa kampuni na viwanda vya nchi za nje ilikuwa kubwa mwaka hata mwaka. Ikilinganishwa na sehemu nyingine, ujenzi wa miundo-mbinu na ujenzi wa mawasiliano wa mkoa wa Hunan ulikuwa ni mbaya, hivyo tulichagua Hunan."

Kuhusu sera nzuri za kuvutia mitaji ya nchi za nje inazotekeleza serikali ya mkoa wa Hunan, naibu mkurugenzi wa kamati ya maendeleo na mageuzi ya mkoa Bw. Yuan Qianpei alisema,

"Mkoa wa Hunan unatekeleza sera zake wenyewe, serikali inafuta kodi kwa kampuni na viwanda vyenye mitaji mikubwa vinavyowekea mkoani humo"

Bw. Yuan aliongeza kuwa licha ya kufuta kodi, mkoa wa Hunan inatoa msaada mkubwa kwa kampuni na viwanda vikubwa vya ubia na vyenye mitaji ya kigeni katika matumizi ya ardhi na huduma nyingine zikiwemo umeme na maji.

Meneja mkuu wa Kampuni ya LG-PHILIPS ya Mpambazuko Bw. Quan Xiangyun alisema kuwa mwekezaji wa kampuni hiyo ameamua kuwekeza Yuan za Renminbi bilioni 2 kwa kujenga mstari wa kisasa wa uzalishaji wa vioo vya televisheni za rangi ili kuwania nafasi ya kuongoza katika sekta hiyo.

Idhaa ya kiswahili 2005-06-07